Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Nimesikia katika advert moja ITV leo usiku, kuna gazeti la SEMA USIKIKE ambalo lina habari kuwa Mh. Masha alikutana na kampuni anayoikingia kifua huko Geneva Uswisi siku za nyuma kuhusiana na Tender ya Vitambulisho vya Taifa.

Kama ni kweli basi ipo kazi.

Mods: ikishachanganya mnaweza mkaiunganisha na thread kuu.
 
Masha...Kanumba...Wema...Masha...Kanumba..Wema...Masha...Kanumba...Wema...Mwaka huu magazeti na vijarida vina kazi!...
 
Kwa waliosoma article ya Yahaya Charahani kwenye Mwananchi ya leo anaweza kuangalia jambo hili katika mtazamo mpana zaidi. Hebu jiulize ni kwanini Magazeti ya Mengi ndo yapo mstari wa mbele kuandika kuhusu Masha. Tangu wameanza hakuna jambo lolote jipya walilotuambia zaidi ya kuzunguka na kurudiarudia yaliyopo kwenye barua ya Masha kwa PM. Mengi nasikia amenunua gazeti la majira pia, kwa lengo hilo hilo. Nadhani hili suala ni zaidi ya Vitambulisho.
 
Mkuu Keil,

I wish we had more people of your reasoning caliber; Nasikia kuwa documents za kampuni moja ya kitanzania ilikuwemo kwenye kabrasha la Sagem (nina ambiwa tayari wajanja wameshalichomoa huko kwenye tender committee na huenda likamfikia dr. Slaa na hata JF muda wowote). Nasikia Sagem walimtaja hiyo kampuni kam sub-contractor na wala siyo partner. Sasa issue ni hiyo, kamati inasema huyu ni partner na lazima uwe na agreement ya Joint Venture; Sagem wanasema huyu ni sub-contractor na kwa sub-contractor siyo lazima kuwa hiyo JV agreement. Nasikia Sagem wanayo policy ya kutotumia ma-partners baada ya scandal ya Nigeria walipolizwaa na local partner (ingawa eventually waliifanya project minus the local partner), kwa hivyo since then wakaamua kuwa watatumia ma sub-contractors and not partners.

Sasa wajanja wa mjini wanasema kuwa tender board walivyoona hilo ni la msingi ndiyo maana wakagwaya kwenda PPRA kwa vile kutokuwa na JV agreement siyo kigezo cha kumwengua mzabuni at this pre-qualification stage, kwa hivyo waka-utilize issue ya waziri kuingilia mchakato na kumwandikia CS. Kwa hivyo unaona wazi kuwa kila mwamba ngoma anavutia kwake. Tender comitte inajua imechemsha inajihami kwa kuingiliwa na waziri, waziri anajua hana mamlaka ya mojakwamoja therefore anataka PPRA wasuluhishe who are legally mandated to solve such disputes.

But all in all thanks for you open-minded "un-spinned" observation.

ZalendoHalisi

1.Tatizo ni kuwa hatuna namna ya kupima "good intentions" ndiyo maana tunakazania taratibu na kanuni. Hebu tuseme bodi ingekubali ushauri wa Waziri na kumrudisha mzabuni. Halafu mzabuni huyo ashinde. Kwa vile tunajua kuwa hakuna siri kwenye bodi, je hiyo haitawapa sababu wazabuni wengine kudai kuwa mzabuni huyo amebebwa? Hawa wakija na ushahidi wa yote haya, nani angeamini kuwa ni "good intentions" tu zilizomsukuma waziri? Kwa vyovyote vile mradi ungekuwa slammed na court injuction na wakina IMMA wangeanza kuvuta! Nia nzuri inawezekana alikuwa nayo lakini alivyofanya ndiyo kumemharibia.

2. Kwa bahati mbaya wengi wetu tunaimani kuwa civil servants wote ni hamnazo, loosers kwa jina lingine. Tunaamini kuwa kama wangekuwa nazo wasingebaki huko kwenye vumbi bali wangeingia kwenye private sector na kuvuta mamilioni. Naamini Waziri kwa upande anafikiri hicho. Kuna ka-superiority complex hapa. Mfano ni huku kudai kuwa hiyo tenda board haikuweza kutofautisha kati ya Sub-contractor na Joint Venture partner. Kuamini kuwa hawana uwezo wa kusoma na kutafsiri tender conditions. Hatuwatendei haki.

3. Kingine ni kuwa tunaamini kuwa civil servants wote ni corrupt. Kwa hiyo mtu akisema kuwa nilikuwa nazuia hujuma za makusudi tunamwamini. Si hao wote wana njaa? Hii nayo si kuwatendea haki. Bila shaka Wako walio corrupt pengine hata ni majority. Lakini wako ambao wanachotaka ni kufanya kazi kwa kadri ya utaalamu wao na ujuzi wao. Hatuwatendei haki kwa kuwatuhumu wote kuwa wala rushwa.

Amandla........
 
- Habari za dataz nilizozipata sasa hivi toka Dodoma ni kwamba hii ishu sasa ni official kuwa imekufa na waziri hana makosa. Barua ya waziri kwa Waziri Mkuu ili-leakishwa kwa makusudi na kambi inayomsafisha waziri, matokeo ni wasomi wengi walioiona hii barua wamekataa kabisa kwua waziri ana makosa, infact hata wale viongozi wa juu waliokuwa wakitaka waziri asulubishwe wamebadili mawazo, mpaka Spika pia.

- Mwenyekiti wa kamati ya bunge hakujua kwamba sheria yetu inasema kwamba mchakato wa tenda za serikali huwa hautakiwi kuingiliwa na yoyote mpaka mwisho, kwa hiyo hata kitendo cha kamati yake ya bunge hivi karibuni kuingilia kati ilikuwa pia ni kuvunja sheria hiyo, kwa hiyo nasikia na wao wameambiwa sasa wakae pembeni.

Wakuu nimezifikisha kama nilivyopewa hizi, ni kwamba ishu imekufa rasmi na waziri hana makosa na hata mkuu wa kaya amekubali hilo.


Ahsante Wakuu and Out!
 
alisema pinda mwana wa mizengo mkaona anatetea uovu,mh.waziri mkuu alisema Dr,Slaa umewahi sana kuileta hii issue,ungesubiri mambo yaisha kwanza then tungehukumu vyema

sasa kama kweli imekufa sijui waliokurupuka itakuwaje? tusubiri tuone?

I always emphasize that speed in worung direction is irrelevant
 
- Habari za dataz nilizozipata sasa hivi toka Dodoma ni kwamba hii ishu sasa ni official kuwa imekufa na waziri hana makosa. Barua ya waziri kwa Waziri Mkuu ili-leakishwa kwa makusudi na kambi inayomsafisha waziri, matokeo ni wasomi wengi walioiona hii barua wamekataa kabisa kwua waziri ana makosa, infact hata wale viongozi wa juu waliokuwa wakitaka waziri asulubishwe wamebadili mawazo, mpaka Spika pia.

- Mwenyekiti wa kamati ya bunge hakujua kwamba sheria yetu inasema kwamba mchakato wa tenda za serikali huwa hautakiwi kuingiliwa na yoyote mpaka mwisho, kwa hiyo hata kitendo cha kamati yake ya bunge hivi karibuni kuingilia kati ilikuwa pia ni kuvunja sheria hiyo, kwa hiyo nasikia na wao wameambiwa sasa wakae pembeni.

Wakuu nimezifikisha kama nilivyopewa hizi, ni kwamba ishu imekufa rasmi na waziri hana makosa na hata mkuu wa kaya amekubali hilo.


Ahsante Wakuu and Out!

Thanks Sauti za umeme!!

Masha kama kachomoa na hii basi huyu waziri kijana na mwanasheria mahiri ni balaa. Masha for presidency 2015!!

Masa
 
Last edited:
Nimesikia katika advert moja ITV leo usiku, kuna gazeti la SEMA USIKIKE ambalo lina habari kuwa Mh. Masha alikutana na kampuni anayoikingia kifua huko Geneva Uswisi siku za nyuma kuhusiana na Tender ya Vitambulisho vya Taifa.

Kama ni kweli basi ipo kazi.

Mods: ikishachanganya mnaweza mkaiunganisha na thread kuu.

Hii inakumbusha lile sakata la kusaini mkataba wa Buzwagi, London. Karamagi kwanza alipinga kabisa lakini baada ya kugundua Dr Slaa na Zitto wamemshika pabaya basi ikabidi aumbuke hadharani kwa kutaka kuudanganya umma wa Watanzania.

Kama hili ni kweli basi kuna haja ya Masha kuwekwa kiti moto ili ajibu alikuwa na mazungumzo yapi alipokutana na hiyo kampuni, Geneva. Je, mkutano huo ulikuwa officially au ulikuwa wa pembeni pembeni.
 
Mkuu Keil,

I wish we had more people of your reasoning caliber; Nasikia kuwa documents za kampuni moja ya kitanzania ilikuwemo kwenye kabrasha la Sagem (nina ambiwa tayari wajanja wameshalichomoa huko kwenye tender committee na huenda likamfikia dr. Slaa na hata JF muda wowote). Nasikia Sagem walimtaja hiyo kampuni kam sub-contractor na wala siyo partner. Sasa issue ni hiyo, kamati inasema huyu ni partner na lazima uwe na agreement ya Joint Venture; Sagem wanasema huyu ni sub-contractor na kwa sub-contractor siyo lazima kuwa hiyo JV agreement. Nasikia Sagem wanayo policy ya kutotumia ma-partners baada ya scandal ya Nigeria walipolizwaa na local partner (ingawa eventually waliifanya project minus the local partner), kwa hivyo since then wakaamua kuwa watatumia ma sub-contractors and not partners.

Sasa wajanja wa mjini wanasema kuwa tender board walivyoona hilo ni la msingi ndiyo maana wakagwaya kwenda PPRA kwa vile kutokuwa na JV agreement siyo kigezo cha kumwengua mzabuni at this pre-qualification stage, kwa hivyo waka-utilize issue ya waziri kuingilia mchakato na kumwandikia CS. Kwa hivyo unaona wazi kuwa kila mwamba ngoma anavutia kwake. Tender comitte inajua imechemsha inajihami kwa kuingiliwa na waziri, waziri anajua hana mamlaka ya mojakwamoja therefore anataka PPRA wasuluhishe who are legally mandated to solve such disputes.

But all in all thanks for you open-minded "un-spinned" observation.

ZalendoHalisi

Zalendohalisi.............
Prequalification exercise kuna kuwa na General Instruction na Special (wengine huita particular) instruction to bidders

sasa basi usually unaitumia special instruction to suit your tender needs.......

Kwenye specialised project kama hii.....main Contractor anatakiwa aeleze kinagaubaga ana-subcontract kitu gani na vile vile kiwango/amount cha kazi ya huyo subcontractor inakuwa limited to certain %ge inayokuwa stated ktk special instruction

In our case
1. kama SAGEM.....wali-mention subcontractor...then walitakiwa wapewe conditional pre-qualification pending substitution of a subcontractor....ONLY IF....the subcontractor does not meet/suit the technicalities of the project.......however,..........Je, intention letter ya ku-subcontract ilikuwepo.............was this the only kigezo kilichowatoa..........only kamati knows this fact

2.kama SAGEM.......wali-mention partner.........then hawana jinsi....bali walitakiwa ku-submit JVA........again only Kamati knows this fact

3. Waziri hakutakiwa kuingilia whatsoever hili zoezi......naona precedence iliyowekwa na Lowassa inafanya kazi yake......huu ni UTOVU WA NIDHAMU dhidi ya kanuni/taratibu/sheria tulizojiwekea

4.Unless wamekuwa acquitted na corruption charges kule Nigeria.....sijui hii room ya kufikia hatua ya pre-qualification waliitoa wapi.........

5.Ukifuatilia track record ya project ilizokwishafanya SAGEM......says a lot of inferior products and very shaky in project implementations........and hence open room for a lot of boo boo to be done......check projects walizofanya Honduras, Malaysia na nchi zingine..........

...........umesema kuwa "unasikia" SAGEM wana policy ya kutokuwa na partners baada ya kulizwa kule Nigeria.......hivi SAGEM alilizwa au SAGEM waliwaliza Nigerians na substandard product................

.......kule Nigeria.........kipindi hicho binafsi nikiwa huko....SAGEM ranked 5th in the bid process.....na ilibidi serikali ya Nigeria ilipe pesa kibao kwa kampuni ilyokuwa potential ktk kupata tender hiyo
 
Last edited:
Zalendohalisi.............

5.Ukifuatilia track record ya project ilizokwishafanya SAGEM......says a lot of inferior products and very shaky in project implementations........and hence open room for a lot of boo boo to be done......check projects walizofanya Honduras, Malaysia na nchi zingine..........

...........umesema kuwa "unasikia" SAGEM wana policy ya kutokuwa na partners baada ya kulizwa kule Nigeria.......hivi SAGEM alilizwa au SAGEM waliwaliza Nigerians na substandard product................
QUOTE]

Mkuu Ogah

Cha ajabu kwangu pamoja na sub-standard workmanship accompanied by a ton of "boo boo" bado wanafanikiwa ku-roll out projects all over the place, Europe, USA, Asia na Africa. They have implemented ID and AFIS projects in 10+ countries in Africa na bado kila kukucha wanapata kazi left right and centre, I wonder how do they do that!

Huko Malaysia bado wapo pamoja na "boo boo" zao what is happening? ThirdFactor | Sagem Sécurité selected by Malaysia for new biometric ID system

Labda hawa jamaa wana kaujanja kama kale ka "Bill Gates na Microsoft" they are smart enough to wade muddy waters au wanahonga ile mbaya.

Naona sasa wameamua kumnunua competitor Printrak owned by IBM
Sagem to buy Motorola's biometrics business @ Biometrics SecurityInfoWatch.com

My personal view ni kuwa hivi ni vita vya wakubwa - these are multinational corporations fighting for another shot at our money, wanapambana on our grounds and the locals just pawns, incidentally Tanzania ni uwanja this time!

Good day mkuu - Over and OUT!

ZalendoHalisi
 
Kwa waliosoma article ya Yahaya Charahani kwenye Mwananchi ya leo anaweza kuangalia jambo hili katika mtazamo mpana zaidi. Hebu jiulize ni kwanini Magazeti ya Mengi ndo yapo mstari wa mbele kuandika kuhusu Masha. Tangu wameanza hakuna jambo lolote jipya walilotuambia zaidi ya kuzunguka na kurudiarudia yaliyopo kwenye barua ya Masha kwa PM. Mengi nasikia amenunua gazeti la majira pia, kwa lengo hilo hilo. Nadhani hili suala ni zaidi ya Vitambulisho.


Nafikiri ingekuwa vyema kama ungejaribu kutupatia ufanunuzi hapo, isije ikawa ni porojo tu za magazeti ya UDAKU. Lete uthibitisho kuonyesha Bw. Mengi kanunua gazeti la Majira. Udaku hauna nafasi hapa, ni nondo tu. Sogeza NONDO hapa kuthibitisha hayo madai kabla hayajawa UDAKU.
 
😎
Kitambulisho Cha Taifa2.JPG
 

Attachments

  • Kitambulisho.jpg
    Kitambulisho.jpg
    152.1 KB · Views: 82
Nimesikia katika advert moja ITV leo usiku, kuna gazeti la SEMA USIKIKE ambalo lina habari kuwa Mh. Masha alikutana na kampuni anayoikingia kifua huko Geneva Uswisi siku za nyuma kuhusiana na Tender ya Vitambulisho vya Taifa.

Kama ni kweli basi ipo kazi.

Mods: ikishachanganya mnaweza mkaiunganisha na thread kuu.

nimejaribu kuiweka hiyo nakala hapa jamvini ( ya sema usikike) kwa pdf,(kumradhi mie sio mtaaalam sana wa haya mambo ya kuweka mabandikoni),lakini ukisoma inanikumbusha mzee karamagi na buswagi,
na ukimsikiliza mnyika wa chadema(haliyoyasema kwenye TV) na ukipima,mie nahisi hivyo vinasa sauti avikuwa nguvu ya waziri kijana hila vyombo usika wakijaribu kujua nani kavujisha barua aliyoandikiwa mzee wa pushbeki(pinda),maanake walikalipiwa sana watunza siri wetu na mzee wa pushbeki,hila kazi professional unproffesional,

duh! ebwana heeee!!!
 

Attachments

Pundamilia,

Kwa hiyo ndugu yangu unanambia hizi power grab kati ya Chief Secretary, the Minister, and Principal Secretary hazikuanza leo wala jana? Of course!

Utaratibu wa kazi ya Katibu Mkuu Kiongozi uko fuzzy. On the one hand kuna wachangiaji wengine wanasema siku zote makatibu wakuu walikuwa "wanafunikwa" na mawaziri waliozoea vibaya. On the other, you have this Masha situation ambapo Waziri ndio anakataa "kufunikwa," anaangalia kazi yake kama ni dhamana ya mwisho juu ya kazi zote za Wizara, anajaribu ku push back against this backdoor paper dealing between the secretaries at Ikulu and one right under his nose. Sasa sidhani kama tunaweza kusema kwa uhakika nani kamuingilia mwenzake, lakini suffice is to say that hii itifaki ina mushkeli na inachanganya wengi.

Katibu Mkuu Kiongozi, inadaiwa, ni mkuu, ni bosi, wa watumishi wa Umma. Definition za "mtumishi wa umma" zimetolewa nyingi humu. Moja imesema ni wote ambao sio "political appointees" au wabunge. Kwa nadharia hiyo, Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, ambae sio mwanasiasa, sio Mbunge, na yeye bosi wake ni Chief Secretary! Au kuna exception kwamba mwanajeshi sio mtumishi wa umma? Na Mkuu wa TISS je? Au ma-spy nao wako exempted from this model? Jaji Mkuu nae anaripoti kwa Chief Secretary? Au the judiciary iko excepted? I mean, at some point you gonna have to say somebody come up with a newer definition of Mtumishi wa Umma, cause this just ain't working, it's got too many exceptions, don't ya think? Ungependa kusikia defition yangu ya "Mtumishi wa Umma"? Mtu yeyote anaepokea paycheck ya serikali ni mtumishi wa umma. Every last one of them! Which makes Chief Secretary the boss of everybody! Outta whack, ain't it? Ndo maana nasema Luhanjo si bosi wa mtu!

Nadhani Masha ameeleza vizuri sana role ya Chief Secretary: "Ninatambua kwamba Katibu Mkuu Kiongozi anayo mamlaka na madaraka makubwa ya kuingilia maamuzi ndani ya Wizara yoyote pale anapoona maagizo ya Baraza la Mawaziri hayatekelezwi."

Kwangu mimi hapo maana yake huyu Chief Secretary anaweza kuingilia chochote kile kinachofanywa na yeyote yule, katika wakati wowote ule akifuatilia maagizo ya Barazala la Mawaziri. Including ya Waziri. Lakini hii haimaanishi ni bosi wa Waziri au Katibu Mkuu. Ila, "...ingefaa Waziri ahusishwe kwa kuwa mwisho wa siku mimi ndiye nitakaewajibika kwa maamuzi yoyote ambayo yatafanyika Wizarani kwangu pasipokujali kwamba maamuzi hayo yalipata baraka za Katibu Mkuu Kiongozi au hapana."

Waziri anasema Katibu Mkuu Kiongozi hawezi akamvuta chemba Katibu wa Wizara. Wizara ni lazima iwe ukurasa mmoja katika kutekeleza maagizo ya kuingiliwa na Katibu Mkuu Kiongozi. Mkuu wa Utumishi wa Umma sio Mkuu wa watumishi wa umma. Tusichanganye.

Nadhani Waziri Masha hakukosea kukataa kufanywa second banana wa Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo.

Capo di Tutti Capi Kuhani.

Bado unachanganya mambo. Unafanya literal translation la mtumishi wa umma kumainisha mfanyakazi yeyote anayelipwa kutokana na kodi ya wananchi. Hapa unakosea. Tena sana. Ili kuweka wazi mfumo wa utendaji serikalini nitatumia kiingereza inapotakiwa. Badala ya utumishi wa umma, nitatumia Public ( awali ilikuwa Civil) Service na mtumishi wa umma Public ( awali ilikuwa Civil) servant.

1. Public servant ni mtumishi aliyeajiriwa kwa mkataba wa kudumu unaongozwa na kanuni na taratibu za Civil Service Department ( Awali ilikuwa Civil Service Commission). Wengi wao ni wale walioajiriwa na Serikali Kuu pamoja na Executive Agencies zake. Mtumishi Mkuu katika hawa ni Katibu Mkuu Kiongozi.

2. Watumishi wa ngazi ya chini serikalini ( madereva, wahudumu n.k.) si Public Servants. Watumishi walio katika mikataba maalum nao si Public Servants.

3. Wanajeshi si watumishi wa umma maana ajira zao haziko chini ya Civil Service Department.

4. Waajiriwa wa mashirika ya umma kama Tanesco, ATCL, NHC, Dawasa n.k. si watumishi wa umma.

5. Wabunge si watumishi wa umma. Hawa na wafanyakazi wengine wa bunge ajira zao ziko chini ya Ofisi ya Bunge.

6.Mawaziri si watumishi wa umma maana wao kama wabunge wengine ajira zao ziko chini ya Bunge.

7. Majaji si Public Servants. Kwa hali hiyo Jaji Mkuu si mtumishi wa umma.

8. Rais na makamu wake nao si watumishi wa umma nao kwa sababu hiyo hiyo. Ajira zao haziko chini ya Civil Service Department.

Public Servants ni a-political. Hawatakiwi aslani kuwa wanasiasa. Utendaji wao unatakiwa uongozwe na taaluma zao pamoja na kanuni na taratibu za ajira yao. Hawa wanatakiwa kuhakikisha utekelezaji wa maagizo ya wanasiasa ( mawaziri n.k.) hayavunji miiko ya utendaji bora na hatawaliwi na sababu za kisiasa. Kwa mfano. Waziri akitaka Public Servant ahamishwe kutoka sehemu yake ya kazi kwa sababu ni mfanya kazi hodari na anapofanyia kazi ni jimbo la upinzani, Katibu Mkuu anawajibu wa kukataa kumhamisha. Waziri akisema bara bara isijengwe kwenye jimbo la upinzani, Katibu mkuu ana wajibu wa kumpinga kwenye hilo. Kusema kuwa Waziri akizuiwa ku-meddle kwenye utendaji wa kila siku wa wizara atakosa la kufanya si kweli. Akiamua ku-twiddle his/her thumbs na ku-sit on his/her fanny ni uamuzi wake na utaonyesha udhaifu wake.

Tunachosahau wengi ni kuwa mawaziri ni wabunge. Kazi yao kubwa ni ubunge na si uwaziri. Akipoteza ubunge, uwaziri nao anaukosa. Lakini akipoteza uwaziri haina maana na ubunge nao anaupoteza. Kwa sababu hii hawatarajiwi kufanya kazi ya uwaziri na kuacha au kudharau majukumu yake kama mbunge. Ndiyo maana uchaguzi unapokaribia mawaziri wanaweza kushinda jimboni mwao bila kuathiri utendaji wa wizara yake. Waziri ni kama Chairman of the board asiye na board. Wajibu wake na kazi yake ni kuhakikisha kuwa ahadi zilizompeleka yeye na chama chake bungeni zinatekelezwa. Ni msimamizi wa policy issues, sio administration.

Mimi nashindwa kukuelewa unapomtetea Waziri kwa kukataa kuwekwa pembeni na kufanywa ndizi ya piki na Katibu Mkuu Kiongozi. Kwani malalmiko yake yalipuuzwa na Katibu Mkuu wake? Si mwenyewe amekiri kuwa KM aliyapeleka tenda bodi na jibu la tenda bodi akapewa. Ni kutokana na kushinikiza kwake kuwa yale yalikuwa ni maagizo na si ushauri, ndipo KM akaenda kwa bosi wake KMK. Hawa kila juma wanakutana, Ikulu, chini ya KMK. Sasa waziri alitaka Katibu Mkuu wake aombe baraka zake kwa lolote atakalopeleka kwa kikao cha wenzake? Akikataa kwa vile kinamhusu? KMK ametumia mamlaka aliyonayo na kwa kuangalia context ya ishu yenyewe. Alichomwagiza KM wake ni kuwa asifuate maagizo ya waziri na aachie bodi ikamilishe kazi yake. Alichokosea nini? Au ulitaka KMK amwamrishe KM afuate maagizo ya waziri ( ambayo yalikiuka taratibu za tenda) na aimrishe tenda bodi yake iwarudishe wazabuni wote walioenguliwa? Kwa kufanya hivyo si itakuwa kuingiliwa kwa taratibu za tenda na kufanya tenda yote iwe batili?

Hata Marekani ambako mawaziri ni Public Servants, kuna understanding kuwa career public servants wasiingiliwe. Ndiyo maana Attorney Genera Gonzales alilaumiwa sana alipoanza kuingiza siasa katika uajiri wa watumishi wa ofisi yake!

Kudai kuwa ni lazima Waziri ahusishwe kwa sababu yeye ndiye atakae wajibika mambo yakienda ovyo ni kuwa disingenous. Kukamilika kwa mchakato wa tenda si hatua ya mwisho. Baada ya mchakato, ripoti inatolewa ambayo ni lazima KM wake angemkabidhi. KM asingeweza kuingia mkataba na yeyote, hasa kwenye mradi sensitive kama huu, bila kupata baraka za wanasiasa. Waziri angekuwa na nafasi ya kuwasilisha ripoti ya tenda bodi pamoja na misgivings zake kwa mawaziri wenzake kwenye Cabinet. Huko kutoa duku duku zake kwa uwazi zaidi. KMK nae kama mshauri wao nae angeweza kuelezea msimamo wa KM wake. Uamuzi wa mwisho ungetolewa na Kabineti. Kama wangeona kuna kamchezo kachafu kamefanyika, wahusika wangechukuliwa hatua na tenda kufutwa na kuanza upya. Kwa vile sababu za kufutwa kwake zingewekwa wazi, basi integrity ya the whole process ingebakia. Kwa kufanya alivyofanya Waziri, hiyo integrity imepotea.

Amandla.....
 
Uhusiano wa karibu baina ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, na kampuni ya Sagem Securite inayodaiwa kuenguliwa kwenye mchakato wa zabuni za vitambulisho vya Taifa na kumfanya waziri huyo ataharuki, umegundulika.

Vyanzo vya habari ambavyo Nipashe imevipata vimethibitisha kwamba Waziri Masha alisafiri hadi jijini Geneva Uswisi, mwishoni mwa mwaka jana kukutana na wawakilishi wa kampuni hiyo.

Masha akiwa jijini huko baada ya kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, alikutana na watendaji wakuu wa Sagem na ni baada ya hapo ndipo mvutano ndani ya wizara yake ulipoanza kuhusu kampuni hiyo ambayo iliacha matatizo makubwa nchini Nigeria ambako ilidaiwa kuhonga mawaziri watatu na kusababisha wafutwe kazi na Rais Olusegun Obasanjo na kufunguliwa kesi ya kula mlungula.

Nusanusa za Nipashe zimebaini kwamba Waziri Masha alisafiri kwenda Geneva Oktoba mosi mwaka jana, kuhudhuria mkutano wa wakimbizi kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi (Swiss Air) akitokea Dar es Salaam.

Kabla ya Waziri huyo kuanza safari hiyo ya kikazi, alikwisha kufanya mawasiliano ya jinsi ya kukutana na wawekezaji hao atakapofika Geneva.

Waziri Masha baada ya kuhudhuria mkutano wa wakimbizi, alifanya kikao jijini Geneva na uongozi wa Sagem wakiongozwa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo na Mtendaji Mkuu, JeanLin Fournereaux.

Taarifa za ndani zinasema kwamba kikao hicho kati ya Masha na Sagem kilifanyika Oktoba 5, 2008 kuanzia saa 12.00 jioni hadi saa 2.00 usiku katika chumba cha wageni mashuhuri (suite) chenye namba 0306, hoteli ya Mandarin Oriental.

Vyanzo vyetu vimepasha kwamba katika hoteli hiyo Masha na maofisa wawili wa Sagem walipata chakula cha usiku pamoja.

Kikao hicho kinachoelekea kuwa cha mkakati, kilidumu kwa saa mbili, na kinaelezwa kuwa kilijenga hoja ya kuhakikisha Sagem inashinda zabuni hiyo ya kutengeneza vitambulisho vya Taifa inayotarajiwa kugharimu zaidi ya Sh bilioni 200.

Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinasema kwamba siku iliyofuata, Masha alitembelea zilipo ofisi za Sagem za Geneva huko Max, Schmidheiny, Strasse 202 CH 9435 Heerbrugg, Uswisi kwa mwaliko wa Sagem.

Baada ya kazi hiyo pevu ya maandalizi, Waziri Masha alirejea jijini Dar es Salaam, Oktoba 11, 2008 saa 12.00 jioni.

Hivi karibuni Waziri Masha ameamsha taharuki kubwa nchini baada ya kuvuja kwa taarifa za siri kuhusu mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa.

Nyaraka zilizovuja zinaonyesha jinsi Masha alivyoingilia mchakato huo, kiasi cha kuilazimisha timu ya zabuni ya wizara yake kurudia kazi ya utathmini, na kuilazimisha kukata rufaa kwa Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA).

Waziri Masha pia amenukuliwa katika waraka wake binafsi kwenda kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimlalamikia vilivyo Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kuwa anaingilia kazi za wizara yake bila hata kumjulisha.

Sakata la Masha kuijitosa katika mchakato huo, lilimfanya Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, kuwasilisha hoja binafsi akitaka Bunge kushughulikia kashfa hiyo inayoonyesha wazi kwamba Waziri anavunja sheria ambazo zimetungwa na Bunge.

Hoja ya Dk. Slaa kuhusu Waziri Masha, imepelekwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na hadi mwishoni mwa wiki, Mwenyekiti wake, Wilson Masilingi (CCM), alisema kazi ya kuishughulikia hoja hiyo bado inaendelea.

SOURCE: NIPASHE 09.02.2009
 
Waandishi wa Nipashe wakati mwingine wanafanana na wale wa Global publishers (Shigongo Eric, aka Prof wa Udaku) kama ni kweli basi tutasikia mengi sana mwaka huu na kabla ya uchauguzi 2010
 
Last edited:
Ukisoma gazeti la sema usikike la leo utaona habari hiyo pia ipo lakini inanukuu mtandao wa jamiiforums hili gazeti linamilikiwa na ippmedia pamoja na nipashe na mengine
 
Huu ndiyo utandawazi jamani. Huwezi ficha kitu siku hizi. Huyu mtu anamfahamu Masha vilivyo...na wala hakuna spin hapa.....maana ni kweli Oktober Masha alienda kwenye EXCOM ya UNHCR Geneva..Duh! Nachoka..

Ni yale yale ya Karamagi..alisaini mikataba hotelini akidhani ni siri! Information siku hizi zinasafiri kuliko kitu chochote.

All in all, I just warn watendaji wetu..siku hizi dunia imebadilika sana..nothing you do, will ever be a secret. To me Masha sioni kosa lake kukutana na hawa watu (though wajuvi wa sheria might tell us otherwise)..lakini walioitoa hii habari ni kutaka kumuhakikishia kwamba kijana tulia..we know you than you might think!

Ukweli ni kwamba hata zamani habari watu walikuwa nazo za haya madudu..lakini siku hizi we no longer operate on those outdated laws in our books..siku hizi ni mwendo wa google! Now unafikri Masha au yeyote yule atapambana na uwezo wa google? ataweza? Thats why somebody can confidently print the letter adressed to the Prime Minister here...bila consequences! Solution? We just have to adjust our way of doing business, tuwe transparent na tuache kufanya mambo yanayopingana na majukumu yetu. na wala siyo kuwaogopesha na kuwatisha watu... with "siri za serikali"

Hii ndo faida mojawapo ya utandawazi....
 
Jamani hizo ndizo habari yakinifu. Ni kitu gani tena tunataka tuambiwe ili tuamini kuwa Masha hana interconnection na Sagem??? Ujue moja ya kazi za vyombo vya habari (print and electronic) ni kuibua masuala ya utata katik jamii. Na pia vyombo vyote vya habari haviwezi vyote kwa pamoja vikapata deal ya jambo la kuandika, ni lazima kuwe na mwibuaji wa jambo na wengine wanafuata katika kuandika habari zake. Kwa mantiki hiyo vyombo vya IPP media wamekuwa kirongora (refer sakata la Richmond -mmoja wa mawarizi implicated alisema -- PM alikuwa kirongora i.e mfuangua njia ya kujiuzulu so aliwafungulia njia ya kujiuzulu). Tusianze kupiga bakora au mawe IPP media kama ambavyo ninaona wengine wanasema. Cha msingi tumeshukuru uovu umeonekana katika kazi nyeti ya Usalama wa Taifa, tena dili la bill 200, cha mtoto EPA. Pole Masha.
 
Ah wapiii! Masanja mkuu, sikubaliani na wewe kwamba hakuna ubaya ye kukutana na Sangem. there is a problem. Kama ni kweli basi angetakiwa afanye full disclosure katika ile barua aliyomwandikia Pinda. Aseme alionana nao na alitembelea kampuni huko Uswisi. Like this... SORRY! Ni masuala ya kupanga mikakati na rushwa tena Grand corruption! Kwa nini asingekutana na makampuni yote 29 or whatever? Hii haijakaa sawa!
 
Back
Top Bottom