Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Waziri Masha na Kashfa ya Vitambulisho

Mimi nadhani itakuwa haina maana kama mtamshitaki Masha na Membe akaachwa na wakati yeye nae alishiriki katika dili hili kipindi wakati ni Naibu Wazir , Kwanini hili swala limenyamaziwa kimia?
 
Nyani Ngabu, jamaa anaboa sana, sijui ndio miongoni mwa waliotegemea kufaidika na mgao? Duuh... kweli njaa mwana haramu, unaweza kuuza mwanao Albino hivi hivi.

Ni haki ya Kuhani kuhoji msimamo wetu. Ni vizuri akituhoji ili tuwe na uhakika zaidi ya tunayoyasema. Kwa kuhoji kwake kumesaidia kuweka wazi chain of command serikalini. Kuna wengine tumefaidika na hilo. Kwa kuhoji anatufanya tuangalie upya kile tunacho take for granted. Hajakosea kuhoji. Ikiwa wote tunakubaliana basi hapatakuwa na mjadala. Na hata tukifika mwisho wa mjadala si lazima tukubaliane.

Amandla.....
 
FM,
Nakubali maswali ya Kuhani yanasaidia kutuweka wazi. Lakini kuna wakati yanakera:- lol
 
Kuhani hapa umekosea. Mtendaji mkuu wa wizara ni Katibu Mkuu na si waziri. Ndiyo maana barua zote zinazoandikwa kwenda kwenye wizara zinakuwa addressed kwa Katibu Mkuu na si waziri. Na barua zote rasmi katika wizara zinaandikwa kwa niaba ya katibu Mkuu na si waziri. Mawaziri, waziri Mkuu na Rais si watumishi wa serikali ( civil servants) wao ni political appointees. Kiutendaji basi, bosi wa watumishi wote wa serikali ni Katibu Mkuu Kiongozi. Huyu ndiye bosi wa Katibu Mkuu na si waziri. Katibu Mkuu Kiongozi ni mshauri mkuu wa serikali kiutendaji. Kwa bahati mbaya kwa muda mrefu makatibu wakuu walikubali kufunikwa na mawaziri kiasi cha mawaziri kujisahau. Masha amempelekea malalamiko Pinda kwa sababu yule ndiye bosi wake. Pinda nae atamshauri Rais ambae ndiye bosi wa wote hawa. Mwenye makosa hapa ni waziri Masha na si Luhanjo. Ingawa inauma lakini yeye si Mtendaji Mkuu wa Wizara.

Fundi Mchundo, the self-taught humble servant, shepherd of many, brother of all. Legend is pervasive that as a little boy he hated the morning dew, as such he didn't attend formal schooling. How he rose to become a leader of men, a humble voice of reason, the quintessence of patriotism, is an enduring mystic to many a historian.

Fundi, huyu Masha hana rekodi nzuri ya uongozi. Inawezekana kabisa alitaka kufanya ufisadi hapa.

Lakini nakuomba unifanyie hisani moja mzalendo. As hard as it may be, hebu assume kwamba Masha sio fisadi, assume hana rekodi ya erratic pronouncements wala uchafu wowote ule. Let's hypothesize briefly kwamba hapa pia nia yake ilikuwa ni nyeupe kama mwana kondoo, yani kuhakikisha mzabuni atakaeshinda tenda ni wa haki na kweli. Halafu tuangalie, je, alotenda ni sawa? Okay? Thank you.

"Katibu Mkuu ndie mtendaji mkuu wa wizara" maana yake nini kama sio kutumwa na somebody, most practically na Waziri? Hivi on a day to day basis Luhanjo anawatuma kazi Makatibu wakuu wa kila wizara?

Hilo la "Katibu Mkuu ni mtendaji mkuu katika wizara" hilo mimi sijalisema kinyume na hivyo hata kidogo. Ninachosema ni hiki: maana yake nini hasa huu utendaji mkuu huu? Kwamba hasikii la waziri?

Nani ni muwajibikaji wa mwisho katika wizara? Wizara ikivurunda kazi nzito fulani Waziri hatapata political fallout, au administrative na hata legal liabilities? Waziri akiona Katibu Mkuu ana screw up akae tu anaangalia? Nani ni msimamizi mkuu wa kazi za wizara?

Halafu umesema "Kiutendaji bosi wa watumishi wote wa serikali ni Katibu Mkuu Kiongozi." Halafu kutoka "bosi…kiutendaji" ukaipanua, bosi jumla jumla "huyu ndie bosi wa Katibu Mkuu na si waziri. Kwa hiyo umenichanganyia habari ya bosi wa kiutendaji na bosi wa jumla jumla.

Fundi, kama sheria inasema Masha hatakiwi kugusa huu mchakato, basi Luhanjo hatakiwi kuingilia either maana na yeye hayumo katika mchakato isipokuwa kusikiliza appeals tu. Lakini kama Luhanjo amejiingia kwa kigezo cha ubosi, assuming yeye ni bosi wa Katibu wa Wizara, basi Masha nae ameingia kwa mtaji wajibu wake kusimamia mambo yote ya Wizara yake.

Lingine, ukisema wakina Pinda na Masha na Kikwete sio civil servants nadhani unakosea. Pinda na Masha ni political appointees au political leaders, ndio, lakini ni watumishi wa umma nonetheless. Wote wanatumikia umma. Kati ya hao, kuna political leaders.

Iwapo uko convinced na hilo la utumishi wa umma angalia hiki: Katibu Mkuu Kiongozi officially ni "Mkuu wa Utumishi wa Umma." Hicho ndio cheo chake officially ( Luhanjo mwenyewe alikaririwa akisema hivyo kwenye uzinduzi wa Tume ya Utumishi wa Umma, 2007) na siyo "Mkuu wa Watumishi wa Umma." Ukuu wa Utumishi wa Umma sio sawa na Mkuu wa Watumishi wa Umma. Huyo ni Rais.

Sasa bosi wa Katibu wa Wizara ni nani? Well, kwani huo utendaji huo, maagizo anayapata kwa nani? Anatekeleza na kutenda mipango na mwongozo wa nani? Nadhani sio jibu bovu nikisema ni waziri! Luhanjo haamki asubuhi kutuma daily projects kwa makatibu wakuu wa wizara. Na ukikubali kwamba Masha ndio msimamizi na mwongozaji mkuu wa kazi zote za wizara, huoni kwamba Masha yuko sahihi kuulizia na kufuatilia kazi zinazofanywa na wafanyakazi wake, akiwemo mtendaji mkuu, Katibu ? Halafu Masha akiulizia kitu akaona kuna tenda zinaenda kimizengwe (nilikuomba u-assume kwamba Masha alikuwa ana moyo mweupe) halafu akajaribu kuziwahi kabla tenda hajapewa Richmond mwingine wa vitambulisho hapo kosa litakuwa lake au ni mfumo mbovu wa itifaki?

Wewe unaona hakuna tatizo, unasema Makatibu Wakuu walikuwa wamefunikwa na mawaziri. Well, under your model, or the prevailing model, mimi naona ni mgongano wa majukumu kwa sababu organizational entity yeyote lazima iwe na itikafi, mfumo wa ngazi ya utawala, liwe kanisa, liwe duka la wachaga, iwe nchi, uwe msikiti, iwe familia ya kimafia.

Timu yetu ya uchochoroni ilikuwa na kapten, mweka hazina, na katibu. Wote tulikiwa chini ya mwenyekiti.
 
Last edited:
Hivi wajumbe wa kamati ya BUNGE ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ni kina nani?
 
wakuu wana jf, id deal haina tofauti na twin tower project, id za wapiga kura na kadhalika, mkuu wa medani na wengine mimi ninapenda kujiridhisha juu ya utaratibu wa cs kuwasiliana na accounting officer wa wizara eti kwa nia ya kuepusha ushawishi/maslahi yanayohisiwa juu ya lawrence fortu masha!!! Mimi naamini hapa kuna suala la msingi la kumtizama kwa jicho la uchunguzi mnyalu luhanjo, ninaona kuna game ya kuuficha ukweli wa makusudi kuwa cs naye ana agenda binafsi juu ya hii project, yeye ktk deal ya namna hii ni lazima awe invisible lakini si kwa wale anaowachukulia minutes ktk kikao na rais wetu, najaribu kumuangalia luhanjo zaidi hapa kuliko mtu yeyote yule na ninashauri hawa akina fmes na wenzake wamungalie mzee luhanjo kimaadili na tuanzia pale alipokuwa maliasili akiwa na zakhia then foreign na sasa ikulu yetu, kumbukeni kilichompata mrithi wake salehe pamba na tycoon star tv kwa kumgusa tu kijana severe!!! Marsha ameingia ktk mpambano ambao nadhani alitegewa na akaingia aliposituka ameamua kuwa jasiri kupigana kwa kila aina ya silaha aliyo nayo, ninachokiona hapa ni mkono mrefu wa mengi na genge lake ambalo limejizolea umaarufu usiowastahiki ktk jamii, inanifadhaisha sana ninapoona ikulu ikimbeba mengi ktk hadhara kama ndiye mlipa kodi kiongozi tanzania. Kijana mwenzetu haitaji sisi vijana kughiribiwa kuwa hatufai bali ni msaada wa dhati wa kupambana na maadui ambao sasa wanaleta hoja kuwa eti sisi vijana si lolote!! Marsha anapaswa kusimama ktk kweli na siyo kinyume, ktk hili anaweza akawa shujaa au muhanga. Nini nafasi yetu sisi wana jf ktk sakata hili la kumuangamiza kijana huyu mchanga ktk siasa ila anayeonekana tayari purukushani zinamkomaza?? Je sisi ni sehemu ya kushabikia fitina na kuiasi kweli?? Najutia kuiona jf ikihukumu watu eti kwa sababu kila kukicha magazeti ya mtu fulani yamemng'angania marsha? Nimeona mabandiko ya magazeti yetu humu mbona hatupendi wala hakuna ktk yenu ninyi wakulu tunawaowaheshimu humu aliyethubutu kubandika rai ya leo na viambatanisho vyake?!!! Mungu atubariki na sasa tuanze kuwa wakweli rohoni mwetu kabla hatujafanya chukizo kwa wenzetu.
FDR ukweli uliosema hautaeleweka leo, lakini nakuhakikishia kuwa katika muda mfupi ujao utaeleweka.

Marsha pamoja na matatizo yake, kwenye hii issue ya IDs anatetea ukweli na kama waziri mhusika ni yeye mwenye dhamana hatimaye kuwajibika kwa lolote lile litakalotokea wala siyo Luhanjo. Tena la ajabu nu kuwa katibu mkuu wake ana amua makusudi kumwandikia CS kisirisiri bila ya kumhusisha waziri wake, na issue ambayo anailalamikia ni kwamba waziri hakukubaliani na double standards zilizotumika kuengua wazabuni wengine wakati huo huo kuna wengine waliokuwa na short-commings more serious waliopewa nafasi za kuzirekebisha. Anachotetea Marsha ni double-standards zilizotumiwa!

Waziri Marsha baada ya kutokubaliana na katibu mkuu wake (wa wakati huo) akatoa wao kuwa PPRA iliangalie hilo swala kwa undani na watoe uamuzi kama hiyo evaluation process ilikuwa fair kwa wazabuni wote. PPRA ndicho chombo cha juu kuliko vyote kisheria kwenye mambo ya zabuni. Katibu mkuu wake akalikwepa hilo na kumwandikia Luhanjo waraka ambao ulimfanya Marsha naye amwandikie bosi wake, waziri mkuu.

Kwenye hili swala FDR Jr. umegusa raw-nerve; hebu kumbuka ni nani alianzisha mchakato huu - Mungai! Mungai + Luhanjo = 1; Tena la kuchekesha ni kuwa huyo katibu mkuu aliyemwandikia Luhanjo barua sasa hivi hayupo tena wizarani hapo, ila bado ana watu wake ambao waliinyofoa barua hiyo na kumpa Slaa. Hili dili lilisukwa na Mungai na agents wake ambao bado wapo wizarani na hata wengine wao wapo kwenye idara yenyewe ya vitambulisho ya Mr. Dickson Mwaimu (mlarushwa ile mbaya) pamoja na IT expert wake aliyetimuliwa/demoted Immigration akapelekwa Mbeya baada ya kupokea rushwa kwenye tenda ya passport - baadaye akaenda Uingereza - Oxford - akasomea MSc na aliporudi Mungai akamhamishia kwenye hiyo agency. Kwenye hili wanaoomba Marsha lizwe wako kibao; payroll hiyo ni ndefu ingawa wengine wataambulia bia tu!

Marsha alichofanya cha kuuliza na kutoa option ya kuhusisha PPRA ni sawa. Motive zake za kufanya hilo, who knows ila la uhakika nitakalo lisema milele ni kuwa huu mradi ulisha sukwa mapema mno na walaji walishajiweka tayari na pesa wanazo, Marsha kachafua hali ya hewa. Kuna katibu mkuu mstaafu aliyeteuliwa kuwa consultant kwenye huo mradi hadi leo wamemweka kando kwa vile haeleweki eleweki!

La kuchekesha ni hilo kampuni la Sagem (nime-Google) mbona limepata matenda ya vitambulisho mengi tu Africa (over 15 projects) na hata huko Nigeria walikohonga eventual walipewa kazi. Hata huku majuu FBI, FBI certifies Sagem Sécurité's new MorphoTopTM biometric sensor - find BIOMETRICS , Secret Service, Interpol na idara nyingi nyeti ulimwenguni wanawatumia. Labda inawezekana kuwa wanazaipata kazi zote kwa kuhonga! Or they are just good technically kwa hivyo inawezekana wazabuni wenzao kwenye zabuni la vitambulisho bongo waliwashtukia na kuamua kuwaengua kimafya! Kama ni hivyo basi wamezidiwa kete kijanja na wangojee kwingine.

La mwisho ni kwamba kuna issue ya kutumia model ya Malaysia katika utoaji wa vitambulisho vyetu ambalo linzaungumziwa mara nyingi; hivi hawa wa Malaysia wa utaalamu kweli au ni madalali wa Sagem; Nimekumbana na article hii nikabaki mdomo wazi, inawezekana hao hao Sagem tukawa tunawakubali through the back door! Just a thought. Soma hili; ThirdFactor | Sagem Sécurité selected by Malaysia for new biometric ID system

ZalendoHalisi
 
- Mkuu Zalendohalisi, mbona ulipotea sana bros kulikoni?

- Tunasema hivi jina la ndugu Lau limechafuka sana ni distraction kwa mkuu wa kaya na taifa kwa ujumla, cha muhimu ni vyema akakaa pembeni tu na wakati muafaka ni sasa.
 
ZalendoHalisi na FDR Jr.

Mimi binafsi hii issue ya Masha kwa taarifa ambazo ninazo lakini kwa kuzingatia kuwa hadi sasa mamlaka halali zinapitia shauri hili niliamua kukaa kimya ili niendelee kuona nini kinafanyika.

Sitasema hasa yale ambayo ninayajua juu ya vitambulisho kwa sasa hivi lakini kinachoendelea zaidi ni kujaribu kum-eject Masha katika system. Na hii suala ya vitambulisho imekuja just by the way lakini vita iliyopo kati yake na baadhi ya 'vingunge' ni kubwa sana. Masha kwa wao anaonekana kuwa ni threat na potential katika siasa za sasa na za baadae. Kinachotafutwa ni kuhakikisha anakuwa-marginalized kwa kiwango chochote na kwa gharama yeyote ile. Katika watu ambao wametumwa kummaliza Masha si Mengi pekee the list is long. Nadhani Masha kwa sasa hana kitu cha kupoteza ni vema akapigania kuonesha maovu yaliyojijenga kwani katika hili la ID wengi wanahusika na ni kweli linafanana kabisa la 'Twin Tower'. Nina hakika huko mbele ya safari kuna wazito watakuja kupanda kizimbani kujibu tuhuma dhidi yao.
 
Niliwahi kusema na naomba niseme tena kwamba, kama kuna kosa katika vitambulisho liliwahi kufanywa na mawaziri waliotangulia (Mungai, Mapuri, Ali Ameir na wengineo), watendaji ama hata wanasiasa wengineo nje ya wizara ya mambo ya ndani, makosa hayo hayahalalishi Masha ama yeyote yule. Wala ugomvi kati ya yeyote yule akiwamo Masha na yeyote yule hauhalalishi kufanya makosa. Niliwahi kusema na ninasema tena, kwamba ni UJINGA mkubwa kwa mtu kutumia UGOMVI kati yake na mtu yeyote kama KINGA ya kufanya makosa na tusidhani WATANZANIA NI MABWEGE, Watanzania wa leo SI MABWEGE tena.

Huwezi kusema kwamba kwa kuwa Mr. Simba ana ugomvi na Mr Yanga, basi Mr. Yanga akiiba Mr Simba akamshitaki, polisi watasema "aaah bwana huyo Mr. Simba si ni adui wa Mr. Yanga!!! Achaneni naye na huo wizi ni halali na hata hizo doc alizotuletea Mr Simba ni za siri na zimenyofolewa chumbani kwa Mr Yanga na lazima tumkamate yule Housegirl wa Mr Yanga atuambie zimetokaje chumbani."

Kwa mantiki hiyo kama kuna kashfa ndani ya vitambulisho tusipoteze muelekeo kwa kudai kwamba kuna mkono wa kisiasa. Mbona Dk. Kitine, Sumaye, Ngasongwa, Mbilinyi, Dk. Kigoda, Iddi Simba na wengineo waliponzwa na malengo yao ya kisiasa na yaliyotolewa baadhi yalichukuliwa kwa uzito uliostahili kulingana na ushahidi, yale ambayo yalikuwa ni majungu yaliyeyuka na mengine yalifika mahakamani na kuamuliwa kwamba yalikuwa ni UZUSHI.

Tujibu HOJA kwa HOJA na si HOJA kwa bla blah na visingizio vya kijinga
 
Hapa Masha katokosa big time! Itahitajika nguvu ya ziada kulinyamazisha hili, vinginevyo kiungwana bila kutaka ''kumvunjishia heshima ''bosi wake JK ajiengue mwenyewe.
 
- Mkuu Zalendohalisi, mbona ulipotea sana bros kulikoni?

- Tunasema hivi jina la ndugu Lau limechafuka sana ni distraction kwa mkuu wa kaya na taifa kwa ujumla, cha muhimu ni vyema akakaa pembeni tu na wakati muafaka ni sasa.
tunakowenda siko yani tu Mengi akiwa hamtaki mtu basi anamzushia uongomalafu anajiuzuru.....Nasema Masha ataibuka mshindi kwenye hili na wote mtaaibika.
 
tunakowenda siko yani tu Mengi akiwa hamtaki mtu basi anamzushia uongomalafu anajiuzuru.....Nasema Masha ataibuka mshindi kwenye hili na wote mtaaibika.

Fisadi, hapa Mengi anahusika vipi Mkuu? Mbona uko biased namna hii? Hii issue imetemwa Bungeni na Mbunge mmoja mbele ya Waziri Mkuu na akadai anayo hiyo barua ya Mh. Masha kwneda kwa Waziri Mkuu. Sasa hapo Mengi anahusika vipi na issue za ndani ya Bunge? Jamani Mnyonge mnyongeni lakini haki zake mpeni!
 
tunakowenda siko yani tu Mengi akiwa hamtaki mtu basi anamzushia uongomalafu anajiuzuru.....Nasema Masha ataibuka mshindi kwenye hili na wote mtaaibika.

Labda ushindi wa pale Joli club,kwa sura yake tu MWIZI lakini samahanini sina ushahidi mnaoutaka
 
Mbabe Masha​

i27_slaa.JPG

i28_slaa1.JPG

FDR, you are not doing justice to JF and to your self in your analysis above.
a) Luhanjo & Mengi: Hii ni myth kubwa kuwa hawa wanashirikiana. Luhanjo inafahamika wala hapokei simu za Mengi, na Mengi akiwa na shida Ikulu anamwingia JK moja kwa moja, haangaishani na Luhanjo.

b) Issue ya tender ya ID ni suala la ulaji, tatizo ni kuwa UWT wako ndani sana katika hili kwa ajili ya usalama. Masha kaingia mkenge kwa kuchukua taarifa za siri (briefings toka kwa PS wake) na kujaribu kuzitumia 'kuwasaidia' wazabuni. Angesubiri hizo taarifa zikatoka rasmi, wala tusingesikia kelele hizi. Tatizo ni kuwa kama angesubiri pia, window of opportunity ya kuwasaidia wazabuni wake ingekuwa haipo. Na pia hakujua (au alijua akapuuzia) kama taarifa alizopewa na PS pia ziliishafika Ikulu kwa mkondo wa UWT.

c) Mengi na magazeti yake hapa ni kama tai kaona mzoga. Hakuna kipya walichokitengeneza, ila madudu yote wanayanasa na watu wengine wengi tu wa magazeti. Ni wachache wenye ubavu wa kuandika jinsi ilivyo. Magazeti hayatengenezi matukio. Masha anatengeneza matukio, na wajanja wanayatumia hayo matukio kuonyesha udhaifu wake.

Huu uwezo finyu (myopic view) wa Masha hauukuanza leo (toka TOL, IMMA, Uchaguzi 2000 Sengerema, Vurugu 2005 Nyamagana, etc) ila wakati huo hakuna aliyekuwa na shida naye sana. Sasa ukiweka hayo yote plus Mengi Siku Saba, Mauaji ya Albino, Keko Mramba/Yona, Mademu Rose Garden, Watoto Vifo Tabora, Barua kwa Pinda, etc hata watetezi wake wanakosa nguvu. Utazuia kipi? Masha anawapa silaha mahasimu wake, kummaliza mwenyewe.

Kiungani Mkuu umesema briefly to the point. Kila mahali Masha uongozi au kazi si mfanisi. Anzia hata ndani ya Ndoa yake!!!!!! Tabia zake zinamfanya aweke wazi weak side of him na watu na media ina take advantage!!! Hapa hakuna cha Mengi ila ni Wengi watammaliza!!!! Arudi tu IMMA akaendelee na proffession yake na mademu wa Intern kwa wingi!!!! Kama kuna ambaye alishafanya internship IMMA (lawyers) atakuwa na la kusema kuhusu Masha. Naona mengine ni aibu mno kuyasema cha msingi AJIUZULU. Hata kama ataonekana innocent kwa hili, but ameshaonekana so negatively kwa jamii so aondoke tu kwenye ungozi wa chama chetu Mapinduzi abaki tu kuwa member wa chama kama bado ana hamu ya kuendelea nacho. Poleni sana wale ambao wanajitahdi kumtetea kwa udi na uvumba. Hatukatai kwamba kuna mazuri ambayo ameshayafanya but mabaya yame outweight mazuri. Kila la heri Masha na maamuzi yako mikononi mwako mwenyewe. Sidhani kama utasema ngoja ukashauriane na mkeo kwa hili maana hapo alipo anachekelea kwani ulishamfikisha mahali ambapo upendo ni kapuni. Masha fanya auchambuzi wa maisha yako na kupaka ukweli wa unachokitaka. Naamini anatembelea humu jamvini au vijana wako wapo hapa so mpeni habari, au compile info mpelekeeni aone mawazo yetu sisi Watanzania tuliomo humu ndani ya JF na ambao wengi tuna uchungu na jinsi taifa letu linavyoangamizwa na ulafi wa wachache. Gereza la Guatamano (sijui spelling sawa hapa au??) lihamie hapa ili tuwahifadhi huko walarushwa wa ten percent, mafisadi, n.k na list ipo wazi. Na hapa ili kuwa fair na list ya gereza hilo ni lazima the President awe fair katika kushughilia mafisadi pale inapothibitika kuwa ni fisadi au mlarushwa na si kushughulikia wachache of his choice!!!! Aluta continue!!!!
 
OMG! That's real...

DO NOT Download the attachment if you're not a JF member... It's STRICTLY Confidential.

Comments are allowed, but do not disclose what's it. The stuff will close in few days.

Someone has to resign...

===NOTHING ATTACHED HERE====
 
Back
Top Bottom