Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 65
Kuhani, elewa yafuatayo:
Method ya Open Tender inampa nafasi bidder kuuliza sababu za kuenguliwa baada ya kupewa official notice toka kwa Client. Kwanini Sagem wasisubiri muda huo ufike ndio wapeleke malalamiko yao?
Kwa sababu akisubiri, narudia tena, akisubiri itatokea irreversible damage.
PPRA ni kifupi cha Public Procurement Regulatory Authority. Kazi yao ni kusuluhisha migogoro kati ya Bidder na Client.
Si ulisema Luhanjo ndio hakimu wa hizi appeals, unakumbuka unachokiandika lakini?
Hakuna hata sehemu moja inayomtamka Waziri ktk mchakato wa manunuzi.
Wapi imetaja kwamba Luhanjo aingilie kabla ya appeals?
Masha kalalamika kwa Pinda kwamba mchakato unaoendelea chini ya wizara yake hauendi kama unavyotakiwa. Angekuwa ame-influence process angemuingiza Pinda?
Serikali inaendeshwa kwa karatasi, hapa hatupo ktk kitchen party.
Mtu akipata leak ya official improprieties na ufisadi akaripoti, Waziri atamwambia nitumie hiyo tip kwenye signed, sworn and sealed affidavit?
Kama Sagem walimwambia Masha kwa mdomo, kwanini yeye aliyaweka kwa maandishi kwa Pinda?
Kwa sababu Masha alijua akimwendea Pinda kwa mdomo ataambiwa "hapa hatuko katika kitchen party."
Mpaka sasa hivi hatujui ni wangapi wameenguliwa na wangapi wamebaki. Hii bado ni siri ya Bodi ya Manunuzi ya Wizara ya Ndani ambayo ilikula kiapo kwa kazi hiyo.
Hamjui wewe nani?
Wewe umetuambia, I hope and pray kwamba unakumbuka unachoandika, umetuambia Masha aliomba faili kwa Katibu Mkuu wake, akaona kinachoendelea, akatuma malalamiko kwa Pinda. Yani Masha anajua kwamba SAGEM wameenguliwa. Kwa hiyo tunajua SAGEM wameenguliwa!
Hakuna political responsibility ktk technical issues, huu ni uongo mtupu. Kuna haja gani ya kuwa na Makatibu Wakuu ktk wizara?
Kwa hiyo Waziri aangalie tu Katibu Mkuu wa wizara yake ana screw up?
Hapa Masha kalikoroga, kumsaidia ni kumwambia ukweli tu.
Kwa stori uliyoileta leo inaonekana ni Luhanjo kaingilia.