Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Kwa hiyo nami nikisema tukivunja mkataba huu itatugharimu nitakuwa mchochezi? Huoni wachochezi ni wale walioingia mkataba huu?
Hutokuwa mchochezi na hivyo ndivyo tunapaswa kuwa, lakini tujiandae kugawana maumivu ya vitu hivyo

Lakini ikitokea mianya hiyo ikitumiwa na watu wanaonufaika na mambo hayo hatutafika.

Ikumbukwe kutakuwa na watanzania walioajiriwa na makampuni hayo
 
Nampa hongera Kigwangala kama akifanikisha hili, ila namwambia, wizara hii ndio huwa anguko la kisiasa la mawaziri wengi, kwa kumbukumbu zangu toka mwaka 1988 ni Zakia Megji pekee aliedumu kwa mda mrefu, wengine wote yaliwakuta yaliyowakuta, hebu tujikumbushe kidogo hapa chini;

Arcado Ntagazwa
Alilaumiwa kwa kubinafsisha kiholela Hotel zilizokuwa zinamilikiwa na wizara hiyo, hotel hizo ni Soronera, Lake Manyara, lobo na Ngorongoro, pia aliuza hotel Ya Mount Meru. Alidumu miaka miwili tu 1988-90.

Abubakar Mgumia
Alidumu miaka mitatu 1990-93. kipindi chake nusura nchi iwe jangwa, miti ya asili ilivunwa kwa kasi ya tsunami kwa biashara ya mbao.

Juma Hamad Omar
Alidumu miaka miwili 1993-95. Hapa ndipo ilipoibuka kashfa ya Loliondo ambayo ilishikiwa sana bango na akina Stan Katabalo na mbunge wa Loliondo kipindi kile bw Lepile Ole Moleimet(Sijui yuko wapi siku hizi). Hapa ndipo majina ya akina Mateo Qares yaliibuka na Mzee wa FAT Muhidin Ndolanga ilibidi aachie ukurugenzi wa wanyama pori.

Juma Ngasongwa
Nae alidumu kwa miaka miwili 1995-97. Ilimlazimu kujiuzulu kwa kashfa ya minofu ya samaki kuuzwa nje bila kulipiwa kodi. Idd Simba ndiye aliibua madudu hayo.

Zakhia Meggji
Huyu ndiye aliyedumu mda mrefu wizarani hapo, alikaa miaka nane toka 1997-2005. Labda kuuzwa kwa kilimanjaro hotel ndio ilikuwa mbaya kwake, hakuwa na kashfa kama wenzake.

Anton Dialo
Ilimchukua miaka miwili kusalimu amri toka kwa watendaji wake wa chini maana ilikuwa haelewani nao kabisa, uuzwaji wa vitalu na biashara ya magogo ndio vilimuondoa pale. alidumu miaka miwili 2005-07.

Prof Jummanne Maghembe
Alidumu kwa mwaka mmoja tu 2007-08. Kupandisha kwake bei ya vitalu ilimtengenezea vita kali na wawindaji pamoja na watendaji wake kutomuunga mkono, nakumbuka hapa hat yule mchambuzi maarufu wa mpira dr Leakey alijitokeza hadharani kupunga upandishwaji wa gharama za vitalu.

Shamsa Mwangunga
Huyu mama alifanikiwa kudumu kwa miaka miwili 2008-2010. Alikumbwa na kashfa ya kuongeza kiholela mda wa uwindaji vitaluni kinyume na maagizo ya bunge, pia alikuwa hana maelewano kabisa na katibu wake wa wizara bi Blandina Nyoni mpaka kupelekea mmoja wao kufanyia kazi za selikari nyumbani kwake.

Ezekiel Maige
2010-12, Bwana mdogo sana kipindi hicho, kibarua kigumu cha kupambana na uuzwaji holela wa vitalu hakikuendana na umri wake, kashfa ya uuzwani wanyama hai na kujipatia mali kuliko kipato chake, hasa lile jumba la mil. 600 vilifanya aachie ngazi kwa maagizo ya bunge. Hapa ndipo nyota ya Deo Philikunjombe ilipoanza kuchomoza.

Khamisi Kagasheki
2012-13. Mwaka tu chali. Operation tokomeza na kutangaza Loliondo kuwa pori tengefu havikumwacha salama.

Lazaro Nyalandu
2013-15. Licha ya kashfa nyingi haza zilizoibuliwa na akina Manyerere Jackton, pia inadaiwa alikuwa mtu wa kujirusha sana na totoz mpaka kusahau majukumu yake. Nadhani akina Aunt Ezekiel waliionja Marekani kwa mlungula wa wizara kwa madai wanaenda kutangaza utalii.

Prof Jummanne Maghembe
2015-17. Kwa mara ya pili anaondolewa tena wizarani hapo akiwa hajatimiza hata hiyo miaka miwili kamili, Kipindi hiki ndio nilijua kumbe na faru nao hubatizwa. Faru John(anko), Faru fausta walipata umaarufu kipindi hiki.

Dr Khamis Kigwangala
2017-. Anaanza na mfupa uliomshinda fisi. kila la kheri mnyamwezi.
 
CCM makosa hayarekebishwi kwa jazba. Mligawa maliasili ovyoovyo na bwerere, kuweni wapole msituingize kwenye faini, acheni wafaudu tu. Mmetughalimu sana, we must pay the price!!
 
uzalendo siyo kufanyaambo kijinga. Siwezi kuunga mkono. Hawa wako kihalali. Serikali iliwapa kihalali. Mtawalipa mahela ya miaka 99

Tutakaa nao mezani watulipe Bakhshish(token money for goodwill) then tunaanza ubia nao 50/50
 
tunaweza kulipa fidia huku tukilipwa fedha za uaminifu ili mambo yaishe!
Kila siku tunauliza humu hivi walioingia hiyo mikataba ya umilikishaji na ubinafsishaji hawapo hapa nchini ama hawajulikani?

Alisema hatafukua 'makabuli' au hukusikia mkuu?
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Hahaha, Waziri mpenda Sifa...wacha ajionee tu wanyama na kula vyakula bure kwenye hotel za Wazungu tumbo lijae arudi zake mjini, absolute toilets, clueless wind bag!
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
aaaahhh ssa hisitaleta shda nchi
 
aaahh kwn bdo mwako kwny mkataba wakitaka kulibwa hitakua shda
 
Back
Top Bottom