kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Huko Ngorongoro kuna wawekezaji wa kitalu cha uwindaji wa miaka mingi wanaitwa Ortello. Hii kampuni inahusisha vigogo wa kifalme wa falme za kiarabu. Inasemekana kigogo fulani wa ccm na serikalini wana maslahi na wamekua wanaibeba kampuni hiyo. Kila mwaka kunakuaga na kutangazisha vitalu ila kitalu cha ortello hapo loliondo ni sawa na mali yao tu.
Huko nyuma imedaiwa ortello wakiendesha uwindaji wanyama bila kufuata taratibu na hata kusafirisha nje ya nchi wanyama hai kupitia kiwanja walichojenga Loliondo.
Migogoro na wenyeji eneo hilo la uwindaji huko nyuma ilidaiwa kusababishwa na kampuni hiyo ya waarabu wa uae. Lengo likiwa kutaka kupatiwa maeneo zaidi kwa kuondolewa wenyeji.
Leo hivi waziri mkuu ameelezea bunge kuhusu mgogoro unaoonekana kuanza Ngorongoro na kusema kwa wepesi tu wachochezi watashughulukiwa.
Hadi speaker ilibidi kumsisitizia waziri mkuu kuhusu umuhimu wa wachochezi kujulikana na kuchukuliwa hatua.
Wasiwasi mkubwa tulionao baadhi yetu ni hawa wawekezaji wa arabuni toka UAE.
Huenda ndio wachochezi kwa hivyo uchunguzi uanzie kwao. Hawa ortello wako kwa miaka mingi wananchi wa kawaida hawajui wana faida kwa nchi au kwa vigogo binafsi nchini.