Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Tatizo unatumia hasira,
Hakuna dhambi kwangu kuipenda ccm
Na sidhani kama ni haki yako kunipangia cha kujibu mkuu
Mkuu sikukupangia wala sina uwezo wa kukupangia, mimi ni mtu ninaeamini haki ya mtu kuwa na uwezo wa kuamua na kuchagua anachokitaka.

Hilo hapo juu ni swali....,mimi mwenzako sina chama ninachokipenda,mimi napenda sera za chama sio chama,,,kwa maana hiyo naweza kubadilika nikaipa kura yangu chama chochote nichoona kina sera nzuri kwa wakati husika...
 
Siamini maendeleo endelevu ya nchi kwa kukumbatia wawekezaji wa nje kwa kiwango hiki.Nchi zote zilizoendelea zimefanya hivyo kwa nguvu zao wenyewe (wakiwemo wawekezaji wa ndani)Tukisimama wenyewe tunaweza.Mikataba yote ina kipengele vya namna ya kuiingia na namna ya kutoka,uvunjaji wa mikataba(ambayo haina maslahi kwetu) na namna mojawapo ya kujiondoa ktk makucha ya unyonyaji.Hongera viongozi wetu wote mnaoliona hili kwa maslahi ya watu wetu wote wa Tanzania.
 
Hili limekaa vizuri. Mikataba ya kikoloni au kimangungu haina nafasi tena.
Lakini approach iwe tofauti. Wakae nao na kuwaeleza ukweli huo
waliotoa vibali hivyo wapo tu wanakula gawio lao
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Hivi huu mtataba uliingiwa wakati wa 'sultani yupi'??
 
Kukifanya kipande cha nchi ya Tanzania kuwa kipande cha nchi yao ni kukiuka Mkataba wa Ardhi kwa mujibu wa sheria ya ardhi.
Wanyanganywe tuu.
Naenda kuvhukua kadi ya ccm mpya nikilikuta neno "mpya" kwenye kadi.
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Kwa hiyo nami nikisema tukivunja mkataba huu itatugharimu nitakuwa mchochezi? Huoni wachochezi ni wale walioingia mkataba huu?
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Kwa hili, nampongeza Kigwangala! Nilidhani na huyu nae mtamwogopa kama wengine walivyomwogopa! Ila ongeza Ulinzi wako, kwa ufahamu wangu mdogo tu kuhusu huyo Mwarabu (MwanaMfalme wa Abudhabi) syndicate aliyonayo kwenye Idara Nyeti za hii nchi, hususani katika Wizara yako, sii mtu mzuri!
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Walioingia kwenye hiyo mikataba ni hao hao ambao leo wanatoa matamko. Kwa miaka yote hii zaidi ya 50 ambao ni hao hao hawakuyaona hayo.? Leo with no guts unasema wanakupigania.?
 
Hii kampuni imepigiwa kelele miaka lukuki ....tunapaswa kuunga mkono kila hatua nzuri ....siasa kwenye vitu vya msingi kama hivi vinafanya wananchi wazidi kuwapuuza wanasiasa ....
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Nani aliuza nchi yetu na kwa kibali gani?? Na jinsi gani ya kuzui ya vitu Kama hivi??
 
Ninavo fahamu hawa jamaa akishuka tu KIA wanalipa landing charges na pia wanalipa landing charges za loliondo strip.
Na wakifika hulipa Tanapa sio chini ya $100,000 kila trip
Loliondo yenyewe wanalipa land taxes.
Wamewekeza visima vya maji kila kilomita moja ukitoka ndani eneo
Tuache uchoyo....hao watu wa vijiji hawakuwepo mpaka walipo shawishiwa na wana siasa ambao wanalitaka wao hilo eneo kwa faida binafsi zaidi
Eti Wananchi hawakuwepo? You must be sick kwakweli! Wamaasai wapo Loliondo, na Ngorongoro kwa Ujumla wake Enzi na Enzi kabla babu yake babu wa Babu yako hajatoka kwenye viuno vya Mzazi wake! Acheni kupotosha Historia ili kujustify uwendawazimu uliofanywa na CHAMA CHA MAJAMBAZI ya Rasilimali za Nchi!
 
Nachoshangaa na kinanisikitisha sana ni kuona watu wakipinga jitihada za kumkomboa mtanzania mnyonge, na hao wanaopinga ni vijana watz tena wasomi, then baada ya siku utawasikia wakitaka kugombea nafas za uongoz , na wakipata nyazifa hawana msaada wowote kwa serkal ili kurudisha mali zilizobiafsishwa kwa mikataba mibovu au ardh na viwanda visivyoendelezwa, utaskia wakibwabwaja tu ooohhh sheria ya mkataba itatufungs, ooohh sheria ya mkataba tutalipa pesa nyingi, ivi hiyo sheria ya mikataba inaruhusu mwenyemali aibiwe na kumlinda mwizi/ mnyanyasaji. Tusiwe na mihemko isiyo na tija. Penye ukwel tuitetee tanzania yetu.
Mkuu, kwa uelewa wangu hakuna MTU hata mmoja anayepinga hatua zinazofanywa na serikali za kurejesha raslimali zilizokuwa zimeporwa kwa kutumia mikataba isiyokuwa na tija. Tunachoshauri muda wote ni kwamba ziko taratibu za kisheria ambazo zinatakiwa kufuatwa ili kuongoza utaratibu mzima wa kuvunja mikataba mibovu. Kinacho pigiwa kelele ni utaratibu wa kibabe usiokuwa na hata chembe ya kistaarabu unaotumiwa na watawala wetu. Utaratibu huu wa kibabe unaweza kupelekea nchi kuadhibiwa kisheria na atakayelipa adhabu hii ni mwananchi maskini.
 
Mkuu sikukupangia wala sina uwezo wa kukupangia, mimi ni mtu ninaeamini haki ya mtu kuwa na uwezo wa kuamua na kuchagua anachokitaka.

Hilo hapo juu ni swali....,mimi mwenzako sina chama ninachokipenda,mimi napenda sera za chama sio chama,,,kwa maana hiyo naweza kubadilika nikaipa kura yangu chama chochote nichoona kina sera nzuri kwa wakati husika...
Bora wewe unalijua hilo na hivyo ndivyo wa tz tunapaswa tuwe mkuu
 
Back
Top Bottom