Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Issue ya Loliondo iliyochimbuliwa na Stan Katabalo ina tetesi za kuhusika na bwana mmoja wa Arusha hukohuko miaka hiyo ambaye baadaye alikuja kuwa mkuu wa chama fulani cha mchezo unaopendwa sana. Huyo bwana huko michezoni aligomabana sana na serkali na hatimaye akaondoka kwa uchaguzi tena kwa mbinde.

Mwingine wa Arusha hukohuko enzi hizo anayesemwasemwa ni yule anayetuhumiwa sana kungo'a tembo meno, baadaye akawa kampeni manager wa cha fulani na baadaye tena akawa katibu mkuu wa chama hicho alihokiokoa kutoka shimoni.
Huyo si ni Bwn Ndolanga na Mhs Kinana??
Wafadhiri wakubwa wataguswa??
 
Na hawata ondoka kwa chuki binafsi za udini.
Hata huyo kingwangada atapigwa stop hajui taifa linanufaika vipi na taxes za hawa jamaa.
Hao makelele yenu ya kichaga Rais hawezi kuyasikiliza.
Anafahamu kuwa mnataka poachers wavamie hilo eneo .
Khaaa! Umehamisha gori mkuu, unataka uipeleke kidini sasa hii inshu
 
Yetu macho...
Nikiikumbuka Symbion kabla yake alikuja Mwarabu na kanzu (Dowans), kelele zilipozidi akaja Mzungu na tai.... kimyaaaaa mpaka leo.
Wenyewe ni walewale walichobadili ni mshono wa nguo tu.
Yataka moyo!
Nimecheka peke yangu kwenye gari mpaka aibu aiseee
 
CCM wanajikosha tu kwa wananchi,hiyo mikataba waliingia wenyewe na hao wawekezaji..
Tukikalia haya ya kuilaumu ccm, tutakuja kushtukia kimekua chama tawa milele, kwani watakuwa na sababu nyingi za kuchaguliwa na wanainchi.

Am sure, kama tutaendelea hivi 2020 itakuwa dhoruba kubwa kwa upinzani.

Ikumbukwe mtenda dhambi aki kili na kutubu tena na kujirekebisha upendo wa Mungu juu yake huongezeka mara dufu, tusishangae kama sisiemu wameamua kujirekebisha na kujisahihisha wakiwa bado madarakani wataishika hii nchi kwa kipindi kilefu mno.

Upinzani hasa vijana mnapaswa na nyinyi m badili mbinu za kutafuta dola na sio hizi za kuihukumu ccm kwa makosa waloyatenda ambayo wameamua kuyarekebisa wenyewe.
 
Waziri wa Maliasili asili na utalii Mh. Kigwangala akiwa katika ziara yake wilayani Ngorongoro pamoja na kuagiza kuvifuta vibali vyote vya uwindaji nchi nzima ikiwamo vya kampuni ya ORTELLO BUSINESS CORPORATION (OBC) ya Loliondo, ameagiza kampuni hiyo ya MWARABU kujiandaa kurudi walikotokea, kwasababu hata kama wakibaki mchakato mpya wa ugawaji vitalu vya uwindaji utakapoanza hautawahusu.

Ikumbukwe kampuni ilipewa eneo hilo miaka ya 1990 kwa mkataba wa miaka 99.
Yetu macho tu! kuna msemo "mdomo uliponza kichwa".
 
Hii yote ni CCM ,

Milpo ambiwa mlete mikataba yote Bungeni ipitiwe upya mlikataa..

Sasa mnakuja na story kama hizi za Bwana Saidi Bagaire...(kigwangala)..
 
Kwa hiyo serikali za CCM waliuza kila kitu.
Mwl Nyerere na Ujamaa wake watu wakampa za uso?
Hatuwezi kwenda mbele bila kwanza kuwadhibiti CCM
Kwa haya tumuogope Mungu.
CCM sio mfano mzuri ni madudu kwa kwenda mbele.
Loliondo CCM
IPTL CCM
Buzwagi CCM
Mwadui CCM
Geita Mines CCM
Kilimanjaro Hotel CCM
Air Tanzania CCM
EPA CCM
Kahama Gold Mines CCM
Song Gas CCM
Mtwara Gas Pipe Line CCM
Statiol CCM
Tecs CCM
Bagamoyo Port Complex CCM
Reli ya Kihindi CCM
TIPPER AGIP CCM
Merelani Tanzanite CCM
Escrow CCM
Dowans CCM
Gati no 6 CCM
Twiga KIA CCM
Faru John CCM
Mikopo hewa CCM
Wafanyakazi hewa CCM
Vyeti hewa CCM
Kuuzwa NBC CCM
Kuuzwa TTCL CCM
Kigamboni new city CCM
Flow meter za TPA CCM
ISSUE inakuja, .
Wameamua kujisahihisha na kujirekebisha. Sasa tuliobaki tunachukua jukumu gani??
 
Nilijua tuu kuwa baada ya mambo kuwa poa ,na mzee prof. kutumbuliwa sasa ni zamu ya maliasili na utalii. Kanaanza kamoto kidogo kama utani lakini baadaye utakuja kulipuka kila mtu atashangaa NAIONA TANZANIA MPYA YA NDOTO YANGU HIYOOO!! BIG UP PRESIDENT lazima rasilimali za taifa zisaidie taifa na sio wanyonyaji wachache
Hakuna mtumishi mzuri wa kama alieanza na dhambi akamaliza na haki tena akiwa hai, huyu kwa Mungu ana thawabu kubwa mno,

Kuliko

Aliyeanza kwa haki sasa anamaliza kwa dhambi huyu anastaili adhabu kubwa mnoo.


Naikumbuka stori ya yule mwana mpotevu aseeee
 
Ivi watz wote tukiziunga mkono jitihada za serkal, tutafanikiwa fasta, bt serkal inatupigania while kunawatu wengine kazi yao ni kupinga na kuupotosha ukweli.
Sikiliza wewe zumbukuku sisi hatuna shida na kinachofanywa na serikali tatizo njia inayotumika inatupeleka kwenye janga kubwa! Kifupi kwa wewe usioelewa yule mwarabu ana mkataba wa kupewa eneo hilo
 
Kama wao hawatuheshimu hakuna haja ya kuwaheshimu!! Niambie mtanzania anayemiliki rasilimali huko arabuni kwa mkataba wa 99years! Siipendi ccm ila kwa hili nipo na yeyote mwenye kuonyesha nia ya kuwaondoa hawa ngedure nchini mwetu!
 
Sijaamini kabisa, Mkuu Kigwa anabadilisha chanel, kama alivyofanyiwa Maalim Seif kwa Mfalme wa Oman.
Pipe zije straight badala ya kuzunguka!!
Ipo kazi hapoo!!
 
Hii ni vita kubwa sana.tumuombee mheshimiwa waziri aishinde.anapambana na watu wenye nguvu sana za kifedha.ni zaidi ya wauza unga hawa jamaa.hakuna waziri aliingia wizara hii akashindwa kubadili maisha yake jumla kwa fedha za kununuliwa .yaani ukiktaa kuchukua hela wewe naibu wako anachukua au katibu au mkurugenzi halafu unahujumiwa mpaka Raisi anakuona wewe fala.ndiyo manaa naiona dhamira ya mheshimiwa kuweka wanajeshi kuanzia katibu mkuu mpaka mwenyekiti wa TANAPA

Mwenyekiti wa TANAPA ni mjeshi!?
 
Unajibu kwa uhalisia au kwa hisia zako za kuipenda CCM,watalamu wa saiklogia wanasema unapotoa uamuzi wakati unahisia fulani mara nyngi uamuzi wako unakuwa sio sahihi...
Tatizo unatumia hasira,
Hakuna dhambi kwangu kuipenda ccm
Na sidhani kama ni haki yako kunipangia cha kujibu mkuu
 
Tukikalia haya ya kuilaumu ccm, tutakuja kushtukia kimekua chama tawa milele, kwani watakuwa na sababu nyingi za kuchaguliwa na wanainchi.

Am sure, kama tutaendelea hivi 2020 itakuwa dhoruba kubwa kwa upinzani.

Ikumbukwe mtenda dhambi aki kili na kutubu tena na kujirekebisha upendo wa Mungu juu yake huongezeka mara dufu, tusishangae kama sisiemu wameamua kujirekebisha na kujisahihisha wakiwa bado madarakani wataishika hii nchi kwa kipindi kilefu mno.

Upinzani hasa vijana mnapaswa na nyinyi m badili mbinu za kutafuta dola na sio hizi za kuihukumu ccm kwa makosa waloyatenda ambayo wameamua kuyarekebisa wenyewe.

Maneno yako yana nguvu sana,kitu ninachokiiona mimi hapa kwa hao waliokiri kuwa wamefanya kosa,wanafanya mambo yao kwa kutafuta "KIKI"...

Kama kweli huyu mwekezaji ana hati ya kumiliki hilo eneo kwa miaka 99,basi haiwezekani aondolewe kiholela,kirahisi rahisi kama hivyo..lazima mwekezaji atahami atatafuta njia ya kurejeshewa haki yake..
 
Back
Top Bottom