Kigwangalla na Bashe wamuomba Rais Samia kuanzisha mkoa mpya wa Nzega

REJESHO HURU

JF-Expert Member
Mar 6, 2014
4,451
9,375
Kigwangala anaomba Rais aipe Nzega hadhi ya mkoa baadaye anakuja Bashe anasema mama tunaomba unapoondoka 2030 basi wilaya ya Nzega iwe mkoa.

Anakuja Rais anasema nimepokea maombi ya MBashe kuwa kabla sijaondoka 2030 Nzega iwe mkoa.

Akili za kuambiwa changanya na zako Kigwangala huna chak0 2025.

Huyo ndio Bashe kasuku wa siasa ambaye video yake analia anatakiwa kutekwa bungeni haipo popote pale mitandaoni kama unayo, post hapa usaidie taifa.

---
Mbunge wa Nzega vijijini Hamisi Kigwangalla amemuomba Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwapatia wananchi wa Nzega Mkoa mpya kabla ya muhula wake kutamatika

Ombi hilo ni muendelezo wa ombi lililotolewa jana na Waziri wa kilimo ambaye pia ni Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe

Kigwangalla ametoa ombi hilo wakati wa Ziara ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan alipo simama kuwasalimia wananchi wa Puge Nzega mkoani Tabora.

Amesema wananchi wa Bukene wanapata tabu ya umbali mrefu kufika katika halmashauri yao kutokea eneo hilo la Puge ambapo ni umbali wa takribani kilometa 180 hivyo angeomba kabla ya ombi la Nzega kufanywa mkoa basi kupatikane Halmashauri ya wilaya ya Nzega pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Bukene.

''Bado tutabaki katika maombi yetu, ambayo jana pia tuliyasema kwamba tungependelea wakati unamalizia muda wako tafakuri yako ikupelekee kutupatia mkoa mpya wa Nzega '' Alisema Hamisi Kigwangalla


Chanzo: EATV
 
Uyo ndio bashe kasuku wa siasa ambaye video yake analia anatakiwa kutekwa bungeni haipo popote pale mitandaoni kama unayo post hapa usaidie taifa

images - 2023-10-17T194119.254.jpeg
 
Back
Top Bottom