Waziri Kigwangalla aagiza kampuni ya Uwindaji ya OBC ya Loliondo kurudi walikotokea kabla ya Januari 2018

Kwa hili naunga mkono. Afanye kweli sio matamko tu! Mikataba ifutwe. Utakujaje kuwekeza halafu ugeuze kama ni kwako? Timua warudi kwao tuanze upya. Magu hili je halikuhusu au mfupa mgumu kutafuna?
 
Mikataba mingi ni mibovu, lakini ipo kisheria, tuivunje kisheria. Hata hivo, maliasili kumejaa nyama, na mifupa kwa ajili ya fisi. Wengi uzalendo uliwashinda. Nahisi hajatupiwa pande lake.
 
Huyo mwarabu ndo tunaambiwa huku JF kuwa hilo eneo lake ana mtandao binafsi wa simu?
Na hii ishu ndo iliondoa uhai wa Stan Katabaro?
pasco

Mkuu sio mtandao wa simu tu kuna hata bendera ya UAE hata magari yana plate namba za kwao hahaha akifika mwenyeww wanapandisha bendera hiyo na kila atakaekatiza kutoa huduma za vinywaji, kupiga expell eneo alilokaa na kubadilisha maua mezani hata kupokea wageni anakula USD 100 mpaka 200 papo kwa papo
 
hawa watu wamepata vibari kutoka kwenye serikali kufukuza tu na wana hati miliki sio kitu kidogo , tunarudi kwenye azimio la Arusha inavyoonekana
Majitu ya aina yako ni ya kupiga risasi hadharani. Wewe unajua uharamia wanaofanya hao mabedui wenzako? Ndugu zangu Wamasai wanapoteza maisha kila kukicha katika ardhi yetu ya Asili.
Pathetic swine!
 
Tumetunga sheria mpya nzuri ya maliasili za nchi yetu (national natural resources). Ukiacha madini, gesi na mafuta) maliasili zilizobaki ziko chini ya wizara hii ya Dr Kigwangala zikijumlisha wanyamapori, misitu, ndege wa angani/ porini na viumbe mbali mbali hususani vyura wa kihansi, panya buku na mijusi.

Sheria hii mpya ya maliasili inataka pamoja na mambo mengine, biashara zote zinazohusu maliasili ya nchi serikali iwe na carry free shares za 16%, faida itokanayo na biashara hizi baada ya kutoa kodi zote za serikali igawanye 50 kwa 50 kati ya serikali na huyo mfanyabiashara/ muwekezaji, manunuzi na mauzo yawe wazi kwa pande zote mbili, hakuna kudanganyana nk.

Kwa kuwa maliasili nyingi ziko kwenye wizara hii inategemewa kuwa Mh. Kigwangala atatekeleza sheria hii. Tunategemea kwa mfano kuona kuwa hiyo biashara ya uwindaji/ uvunaji wa wanyamapori wetu kwenye hivyo vitalu vitafanyika kwa kufuata sheria hii ya 16% hisa + 50/50 profit + kodi zote. Kinyume cha hapo hatutamwelewa na panaweza pakachimbika! Zipande ndege au zisipande ndege haina shida ili mradi serikali ipate pesa zake stahiki kwa maendeleo ya wananchi wote. Kwani hayo ndiyo matumizi bora ya wanyama hao. Tukiwa na budget deficit tunauza ziada ya simba au twiga walioko kwenye vitalu hivyo dead or alive! Kuna mbaya gani kuuza ziada ya wanyamapori wetu na kupata mabilioni ya dollar?

We wish all the best Dr Kigwangala.
 
Majitu ya aina yako ni ya kupiga risasi hadharani. Wewe unajua uharamia wanaofanya hao mabedui wenzako? Ndugu zangu Wamasai wanapoteza maisha kila kukicha katika ardhi yetu ya Asili.
Pathetic swine!

..naunga mkono uamuzi wa kuwaondoa Waarabu Loliondo.

..ila napendekeza wafugaji wasiruhusiwe kuingiza mifugo ktk eneo lililoachiwa na Muarabu pamoja na eneo lote la Pori tengefu la Loliondo.

..kuna tuhuma za wafugaji kulazimisha kuchunga maelfu ya mifugo ktk eneo la pori tengefu na vitendo hivyo ni kinyume na malengo ya uhifadhi wa mazingira ya mbuga zetu za wanyama.
 
JPM hawajui waliokula hizo pesa. Labda makada wa zamani. Yeye ananyoosha tu. Waarabu washavuna imetosha
Tafuta muda usome historia ya hao waarabu wa loliondo mpaka kuuziwa hilo eneo ktk kipindi ambacho Mzee Ruksa alikua madarakani.
 
Nakumbuka wakati niko mdogo ingawa nilikuwa najua kusoma na kuandika wakati huo,kulikuwa na kashfa moja kubwa sana iliyoitingisha nchi,kashfa ya loliondo,kipindi hicho kuna mwandishi mmoja alikuwa anaitwa Stan Katabalo,nadhani alikuwa anaandikia gazeti la Mfanyakazi au.., huyu jamaa mwandishi alikuwa anapambana na system na mbaya zaidi alikuwa peke yake katika kutetea masilahi ya nchi yetu, nakumbuka watu kama Ndolanga na wenzake.
Pamoja na Rais wa kipindi kile walikuwa wanahusika sana kwenye ile kashfa ya Loliondo, huyu jamaa mwandishi shujaa huyu alikuja kufa katika mazingira ya ajabu sana na mpaka leo sijasikia hata akienziwa,inauma sana...
Huyu jamaa alikuwa si tu shujaa bali alifungua njia kwenye tasnia nzima ya investigative journalism hapa nchini,hivi kwanini isianzishwe hata tuzo kwa jina lake?
Huyu mtu anadeserve heshima ya pekee sana katika suala hili,kwa sababu hizi kashfa zote mnazoziona leo zikiwemo Richmond, IPTL, ESCROW sio kwamba zimeanza jana au juzi katika nchi hii.
Ni tangu kipindi hichoo cha Mwinyi sema tu watu hawakuwa makini kama ilivyo sasa na matokeo yake kwa wale waliokuwa conscious kama Stan Katabalo waliishia kupotezwa kusikojulikana, REST IN PEACE STAN KATABALO, HAKIKA WEWE ULIKUWA JABALI NA MZALENDO HALISI WA NCHI HII.
 
Back
Top Bottom