Waziri January Makamba akishiriki katika Uzinduzi wa Taarifa ya TANESCO kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linazindua taarifa ya mwaka 2023/2024 na Mpango Mkakati wa miaka 10 utakaoanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.



Omary Issa aeleza sababu kuwajengea uwezo watumishi Tanesco
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Omary Issa amesema 2021/22 ulikuwa wa kihistoria katika kuleta mabadiliko ndani ya shirika hilo, ikiwemo kuwajengea uwezo watumishi ili kuleta ufanisi.

Septemba 2021, Samia Suluhu Hassan alimteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco sambamba na Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo.

Uteuzi huo pia uliendana na uteuzi wa bodi ya shirika hailo ukiwa na lengo la kuliboresha.

"Sasa hivi kuna kikundi kipo nje ya nje kwa ajili ya kupata mafunzo ya kujiandaa kuliongoza shirika hili kikirudi watakwenda wengine.

“Najua kuna watu watauliza kwa nini tunatumia fedha nyingi kuwasomesha lakini, bodi inaona kipaumbele nii kuwaandaa wafanyakazi watakaoweza kuliendesha shirika hili kwa siku za usoni,” amesema.

Amesema kwa nyakati tofauti walikuwa wakikutana kwa ajili ya kuandaa mipango ya muda na mrefu, akisema bodi pia ilichukua jukumu la kusimamia miradi mikubwa ikiwemo Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere.

"Nikuhakikishie mikakati ya miaka 10 iliyoandaliwa tutahakikisha inatekelezwa," amesema Issa.

Kongamano hilo lilikwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa safari ya mabadiliko ya katika kuliangaza Taifa na ripoti ya mpango mkakati wa miaka 10.
F2WogP9WUAA5Ero.jpg

Maharage Chande aeleza mkakati wa kuisuka upya Tanesco
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Maharage Chande amesema safari ya mabadiliko ndani ya shirika hilo ilianza kwa kujipanga ikiwemo kwenda kila mkoa ili kujua changamoto za wananchi.

Chande amesema hayo leo Jumatatu Julai 31, 2023 katika kongamano la Mwananchi Jukwaa la Fikra (MTLF) kwa ushirikiano na Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco).

Kongamano lilikwenda sambamba na uzinduzi rasmi wa safari ya mabadiliko ya kuliangaza Taifa na ripoti ya mpango mkakati wa miaka 10 ya Tanesco.

"Kujipanga ni kwenda kila wilaya, mkoa na kitongoji kujua matatizo ya wananchi na kuanisha mipango ya kuyatatua. Sasa hivi tunafahamu matatizo yote na majawabu yake.

"Kazi hii tulianza na kuimaliza sasa hivi tupo awamu ya pili ya kutekeleza yale yaliobainika, tunaamini 2026/27 tutakuwa tupo vizuri kwa sababu matatizo mengi yatakuwa yamekwisha na tutakwenda vizuri," amesema Chande.

Mbali na hilo, Chande amesema faida ya Tanesco imeongezeka kutoka Sh77bilioni kwenda 109.4 bilioni.

Hata hivyo, amesema faida hizo zitaelekezwa zaidi katika biashara ili kuboresha huduma za shirika.

"Tanesco imeweza kupunguza upotevu wa umeme kutoka asilimia 15 iliyokuwapo hadi kufikia asilimia 14.5," amesema Chande.

Makamba.JPG


F2WODJPXIAAWXAZ.jpg
 
Nimefurahishwa na chalamila ameongea vizuri mno,point kwa point!,nimechukizwa na tanesco wakati nawatazama wakakata umeme tena du!!how funny is it 😁😁😁
 
Financial statement inapatikana wapi watu wasome wenyewe.

Unaita watu kwenye kuzindua Financial statement nakala kwa umma amna.

Masaa zaidi ya mawili hakuna Financial ratio’s, unaongelea vipi financial statement bila ya ratio.

Hizo ndio porojo wanazompa ‘Bi Tozo’ hakuna lolote la maana hapo.
The agenda of (O.P) is Negativity negativity negativity! NO BETTERMENT NOR GOODNESS BEING DONE BY GOVT.
NOTE THIS!
IGNORE QUICKLY!
 
The agenda of (O.P) is Negativity negativity negativity! NO BETTERMENT NOR GOODNESS BEING DONE BY GOVT.
NOTE THIS!
IGNORE QUICKLY!
Nilitegemea utakuja na maelezo hiyo QR code inapatikana wapi ili mtu aweze scan kupata hizo info nilizouliza unakuja na porojo zisizo na kichwa wala miguu.

Umeona wapi mtu anaongelea annual statements bila ya kuonyesha metric measures za finance (ratios) kwa masaa zaidi ya mawili.

Unaweza kuongelea Financial statement bila ya kuwapa copy wadau kwanza; ushaona taasisi yoyote duniani inafanya annual meeting au kuongelea financial results bila ya kutoa copy kwenye public kwanza.

Kwa sababu wewe zwazwa ambae upo tayari kulishwa ujinga usidhani kila mtu humu ana akili zako.

44F81CE7-8D32-4160-BD2E-F5FF55034C5B.jpeg


Kutopenda kuuliza matokeo yake unapewa upuuzi kama huo. Toka lini separate financial position ikawa kubwa kushinda consolidated.

Iko wapi share of subsidiary revenue, iko wapi revenue from associate kwenye equity statement; does that even follow IFRS kama wanavyodai statement imetengenezwa kwa misingi wakati info muhimu hamna. Trust me ukiisoma yote ya mwaka uliopita ujinga mtupu ambao hakuna bank itakopesha kwa statement hiyo.

Kwanini mwaka huu iwe tofauti in terms of adhering to account principles kama ya mwaka jana ilikuwa ovyo; unaweza sifia kitu ambacho ujaona.

Keep your nonsense to yourself
 
Back
Top Bottom