Waziri Jafo atamani Halmashauri zijitegemee baada kutembelea mradi wa Government City Complex wa jijini Dodoma

Mnaua uwekezaji, mnaua biashara, mnategemea hizo halmashauri zenu zitapata wapi mapato?
Licha ya kuua biashara hata mapato ya vilabu vya pombe yanaenda benki kuu unategemea hayo mapato halmashauri zitayapata wapi. Antenna ya serikali kuu ipo busy kutafuta mapato ikigundua mwanya mpya inatolewa control namba tu. kwishney!
 
hujaelewa points zangu au hutaki kuzielewa ,sehemu nyingi nchini haya ma frames na ma ofisi ni mapambo tu kwa sasa mazingira ya hizo biashara ni HOVYOOOO kabisa serikali iliyotakiwa kuweka mazingira mazuri ya bishara ndo kwanza inayavuruga inatamani kufanya biashara ,usishangae hata wakafungua na baa zao sasa
Soko kuu mbeya limedorora vibaya mno.
 
Huyo anayejiita mwendawazimu alilazimisha mapato ya halmashauri ya majiji, miji na wilaya zote Nchini zipeleke mapato yote Serikali Kuu kisha Serikali Kuu itaamua ni kiasi gani wanahitaji kwenye budget yao na kuwapelekea matokeo yake Nchi nzima halmashauri zote ziko hoi bin taabani kifedha.
Ile miradi ya Dar es Salaam Development Cooperation (DDC) iliishia wapi? Walikua na majengo, band ya mziki, kikundi cha ngoma.

Hakuna serikali nyingine iliyowahi kutawala zaidi ya CCM.
 
kwa mfano wapi dar,arusha na shinyanga hata chato maeneo yliyotengwa..wapi?

Kwa jiji la Dar, fursa kubwa ni uwekezaji shughuli za utalii maeneo mbalimbali na Urejelezaji wa Taka Ngumu.

Kwa mfano Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliwatangazia wananchi wotewa kawaida kutumia kituo kipya cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kwa huduma za usafiri, usafirishaji,shughuli za biashara, uwekezaji na uchumi katika Kituo kipya cha mabasi cha Mbezi Luis kuanzia badala ya kutumia kituo cha mabasi cha Ubungo kinachotumika hivi sasa.

Faida ya uwekezaji huo kituo kipya cha mabasi cha Mbezi Luis ni kwa mwananchi waliomba kufanya shughuli mbalimbali zinazojumuisha :-

Maeneo ya Ofisi za kukatia Tiketi.

Maeneo ya kutolea huduma za benki, kampuni za simu, uwakala na wakala wa Fedha.

Maduka ya jumla, Supermarket na Mini Supermarket.

Zahanati, Maabara na Famasi.

Cafe & Fast Food, Migahawa, Vinywaji na baa.

Maeneo ya Wafanyabiashara wadogo na wa Kati.

Sehemu ya kuhifadhia mizigo.

Sehemu ya kuweka Ofisi.

Sehemu ya mazoezi (Gym)

Vending Mashine / ATM.

Maeneo ya Maduka ya bidhaa kama vile Vipuri, vifaa vya kieletroniki, vifaa vya Michezo, vitambaa, Nguo, Magodoro, Vito, Vipodozi, Mapambo, Saloon, Urembo, viatu, nguo za watoto/wanawake na wanaume, pembejeo za Kilimo na Mifugo, Samani (Furniture), Stationary, kioski, Carpets/pillow/curtains
 
kwa mfano wapi dar,arusha na shinyanga hata chato maeneo yliyotengwa..wapi?
Kwa mkoa wa Arusha unawakaribisha wadau wote kuwekeza katika maeneo haya na mengine mengi kwa mfano:
1. fursa mbalimbali za uwekezaji katika nyanja za Utalii,Viwanda,Mifugo na Kilimo.

2. Sekta ya ufugaji ni Ujenzi wa Majoshi yakuogeshea mifugo; Upatikanaji wa Soko maalumu la kuuzia mifugo; Upatikanaji wa Soko la bidhaa zinazotokana na Ng'ombe kama vile; Ngozi Maziwa na Nyama; Uwazishwaji wa Viwanda vya kusindika Nyama na Ngozi; na Uwazishwaji wa Viwanda vya kutengeza bidhaa zinazotokana na Maziwa ya Ng'ombe.

3.Katika Sekta ya Viwanda fursa za Uwekezaji zipo katika viwanda vya kusindika bidhaa zitokanazo na Wanyama kama Ng'ombe na Mbuzi na viwanda vya kutengeneza Mazao yatokanayo na Kilimo.

4. Fursa katika sekta ya utalii ni Uboreshaji na ujenzi wa Hotel za kitalii zenye Campsites na kumbi za mikutano; Kuanzisha maeneo ya historia ya Makabila kama moja ya kivutio cha utalii; Kutangaza vivutio vya utalii wetu ndani ya Mkoa,nchi na nje ya nchi; na Kuboresha huduma ya usafiri kwa watalii wanaoingia Mkoani.
 
Naona tunarejea makosa Yale Yale ya miaka ya mwanzoni baada ya Uhuru, ya kutaka serikali kuhodhi shughuli zote za kiuchumi.
Tunakwenda kufeli tena Kama Taifa
 
1609383657253.png

DAR ES SALAAM KUSUKWA NA MAENDELEO HAYANA CHAMA 🇹🇿​
 
Halmashauri ya chato,chemba iliyo Dodoma, siha, mwanga, iramba, urambo, kakonko, Hadi yesu arudi hazitakaa zijitegemee. Jaffo unakuwa Kama mahoka kumdanganya mkuu wa nchi. Uliosoma Home economics SUA hukua muongo ,umeharibika lini?
Miaka ile ikiitwa BSc Home economics and human nutrition.
 
hujaelewa points zangu au hutaki kuzielewa ,sehemu nyingi nchini haya ma frames na ma ofisi ni mapambo tu kwa sasa mazingira ya hizo biashara ni HOVYOOOO kabisa serikali iliyotakiwa kuweka mazingira mazuri ya bishara ndo kwanza inayavuruga inatamani kufanya biashara ,usishangae hata wakafungua na baa zao sasa
Mkuu nadhani kinachofanya watu wakimbie hizo frem na vibanda ni kodi kubwa kutoka kwa wamiliki wake. Wamiliki wanaishi kwa kukariri unakuta frame moja mmiliki anataka laki, laki tatu, tano wengine mpka mill. kwa mwezi bila kujali hali halisi ya uchumi.

Watu kukimbia vibanda au frem sio kipimo cha hali mbaya ya biashara, biashara bado zinafanya vizuri tu na inaonesha hali ya uchumi ni nzuri tu, haiwezekani mtu una frem zako halafu ukubali mtu akimbie na usimshushie kodi ili angalau upate hata fedha kidogo kama hali yako ya uchumi ni mbaya.
 
Asante, hiyo course watu walikuwa wanaidharau Sana hata ajira zake hazikuwepo .
Ndiyo wameisoma akina Esther Matiko (aliyekuwa mbunge wa Tarime) na wengine kibao nawaona kwenye mashirika ya UN wanakula bata. Zamani ilikuwa inachukuliwa kama kozi ya wanawake.
 
Kwa mkoa wa Arusha unawakaribisha wadau wote kuwekeza katika maeneo haya na mengine mengi kwa mfano:
1. fursa mbalimbali za uwekezaji katika nyanja za Utalii,Viwanda,Mifugo na Kilimo.

2. Sekta ya ufugaji ni Ujenzi wa Majoshi yakuogeshea mifugo; Upatikanaji wa Soko maalumu la kuuzia mifugo; Upatikanaji wa Soko la bidhaa zinazotokana na Ng'ombe kama vile; Ngozi Maziwa na Nyama; Uwazishwaji wa Viwanda vya kusindika Nyama na Ngozi; na Uwazishwaji wa Viwanda vya kutengeza bidhaa zinazotokana na Maziwa ya Ng'ombe.

3.Katika Sekta ya Viwanda fursa za Uwekezaji zipo katika viwanda vya kusindika bidhaa zitokanazo na Wanyama kama Ng'ombe na Mbuzi na viwanda vya kutengeneza Mazao yatokanayo na Kilimo.

4. Fursa katika sekta ya utalii ni Uboreshaji na ujenzi wa Hotel za kitalii zenye Campsites na kumbi za mikutano; Kuanzisha maeneo ya historia ya Makabila kama moja ya kivutio cha utalii; Kutangaza vivutio vya utalii wetu ndani ya Mkoa,nchi na nje ya nchi; na Kuboresha huduma ya usafiri kwa watalii wanaoingia Mkoani.
Wewe unawekeza kwenye nini hapo?
 
Ile miradi ya Dar es Salaam Development Cooperation (DDC) iliishia wapi? Walikua na majengo, band ya mziki, kikundi cha ngoma.

Hakuna serikali nyingine iliyowahi kutawala zaidi ya CCM.
Hahahahahahah kweli kabisa
 
Hii miradi ya Dodoma imeegamia upande mmoja, sioni diversification. Nilifikiri wangekumbuka winery industry ili kutoa ajira na kukuza soko na uwezo wa wateja kwenye hizo malls na supermarkets wanazojenga.
 
Meya wa halmashauri ya jiji la Dodoma ametoa maelezo kuhusu miradi mikubwa waliokweza kuongeza mapato ya ndani y jiji kupitia link
 
Mirad imeegemea upande mmoja wa mji kwanini uwanja ulikuwa ujengwe nala wakahamisha wakapeleka nane nane,

Nane nane kujengwe stand soko ,na bado uwanja tena.. Mbona hii kama hii haiji.
 
Mirad imeegemea upande mmoja wa mji kwanini uwanja ulikuwa ujengwe nala wakahamisha wakapeleka nane nane,

Nane nane kujengwe stand soko ,na bado uwanja tena.. Mbona hii kama hii haiji.
"Rais Magufuli aliagiza litafutwe eneo karibu na Dodoma mjini kujenga uwanja huo na kuhakikisha linapatikana eneo zuri kuelekea njis ya Dar es Salaam. Karibu ekari 300 zipo tayari kwa ajili ya hoteli na hosteli kwa vijana na majumba makubwa ya michezo." Kule Nara eneo ekari 150 lakini lilikuwa na chagamoto zake nyingi na kupelekea hata CDA kuvunjwa milele.
1612609002564.png
 
View attachment 1695921
Huku kutajazana kila kitu !! ,kwanini kusiwe na mgawanyiko wa vitega uchuki kwenye mji !!, huoni ukuaji wa mji kuelekea singida unakuwa mgumu tofauti na njia ya DSM.
 
Back
Top Bottom