#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Shughuli Za mwenge zilipoanza nilijua kabisa wataalam wa zindiko wameamka.

Kuna mambo ndani ya Taifa letu yanafanyika mpaka unajiuliza wananchi kweli Tunaakili?

Hii inshu ya gwajima ni usanii Mtupu,Gwajima si mwanasiasa na wala hana ubavu wa kusimamia anachokisema.

Wanatengeneza huu usani kuwasahaulisha Watanzania matukio muhimu yanayolikabili Taifa Kwa sasa.

Yaani juzi tu katibu mkuu wa CCM ametoa onyo halafu Jumapili gwajima anainua Pembe,anaachwa mpaka jumanne waziri anaagiza atafutwe ahojiwe. Jiulize Kwa nini iwe Leo? na waziri alikuwa anasubiri maagizo Kwa Nani ili atoe amri Leo.
 
Bro unasema waziri kote huko.. mteule wa raisi ka mkuu wa wilaya anampa order police ..

Reference maneno ya mwendazakei.. " ....sheria inawaruhusu kumweka mtu ndani 48hours..."
RC na DC ni wenyeji wa kamati za ulinzi na usalama ktk maeneo yao
 
Nashindwa kuelewa kwanini Mwenge unahusishwa na ushirikina.
Kwa hivyo unataka kutuaminisha kuwa Uchawi utatumika kuhamasisha Sayansi ya Chanjo au?
Ni mambo gani ambayo tunasahaulishwa nayo ambayo ni muhimu kwa maisha ya kila siku ,labda tunaweza kukuelewa!!!
 
Hao wote wawili ni wa kupuuzwa kama sio kukamatwa, huyo wa Kike alituaminisha kwamba corona itaisha kwa kujifukiza na matangawizi haina haja ya chanjo,wa Kiume alituambia maombi yataifuta Corona hivyo tusihofu chochote

Matokea yake;Kwa misomamo ya wote hao tukapoteza maisha ya watu wengi mno wengine viongozi wakubwa,Leo wakike anageuka anasema chanjo ni muhimu wakati wa kiume anashikilia msimamo wake huku watu wakiendelea kufa na waliokufa akishindwa kuwafufua.
 
Wameshatoa enough data

Ni wakati sasa gwajiboy athibitishe tuhuma dhidi ya chanjo feki, content ya chanjo na madhara ya chanjo
Wao ndio wathibitishe chanjo ni salama
Kwa kutoa data za majaribio za muda mfupi, wa kati, na muda mrefu (10yrs +)
 
Kamata mzee wa nanomilimita, na amfifiro.
Dahhhh Gwajima muongo kinoma yaani.
Hata sijui hao waumini wake ni viumbe kutoka mapango gani.
 
RC ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
Chief kaa chini tena ikiwezekana ingia darasani ukasome. We umeona wapi mtu aliyeko kwenye Local government (Serikali za mitaa) ana mamlaka kuliko aliyeko kwenye Central govenment? (Serikali kuu)
Hao wakuu wa mikoa wote wako chini ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa tofauti na mawaziri wote wengine.
Ciao!
 
Wao ndio wathibitishe chanjo ni salama
Kwa kutoa data za majaribio za muda mfupi, wa kati, na muda mrefu (10yrs +)
All the science za safety, efficacy na effectiveness zimeshatolewa… unfortunately you don’t listen because you have already fixed your mind towards a certain direction

on the safety ya long term … unataka virtual or actual, because actual data pick as the timelines elapse
 
Huyo mama anaweza kutafuta pa kulala maana moto wa mawifi huwaga si wa kitoto.....
 
Muda ni mwalimu mzuri sana. Ipo haja ya waziri mwenye dhamana na wizara ya afya kujitathmini. Narudia, Muda utasema! Waziri jjitazame na ikikupendeza kaa pembeni.
 
Shughuli Za mwenge zilipoanza nilijua kabisa wataalam wa zindiko wameamka.
Kuna mambo ndani ya Taifa letu yanafanyika mpaka unajiuliza wananchi kweli Tunaakili?
Hii inshu ya gwajima ni usanii Mtupu,Gwajima si mwanasiasa na wala hana ubavu wa kusimamia anachokisema.
Wanatengeneza huu usani kuwasahaulisha Watanzania matukio muhimu yanayolikabili Taifa Kwa sasa. Yaani juzi tu katibu mkuu wa CCM ametoa onyo halafu Jumapili gwajima anainua Pembe,anaachwa mpaka jumanne waziri anaagiza atafutwe ahojiwe. Jiulize Kwa nini iwe Leo? na waziri alikuwa anasubiri maagizo Kwa Nani ili atoe amri Leo.

Serikali haina dhamira ya dhati kupambana na ugonjwa huu ambao death toll yake hakuna asiyeiona:

1. Waliopotosha ugonjwa awamu ile ndiyo wale wale ambao leo eti ni vinara wa kupambana nao.
2. Mikusanyiko ya watu ikiwamo mbio za mwenge, makanisani, misikitini, kwenye mabasi, masokoni, magulioni nk iko pale pale na bila tahadhari zozote kuchukuliwa.
3. Hakuna takwimu zinazotolewa kuhusiana na ugonjwa huu kiasi haieleweki tuko wapi na tunakwenda wapi.
4. Haupo mkakati wowote ulio wazi wa kupambana na ugonjwa huu.
5. Kupimwa Corona inaendelea kuwa ni kwa pesa na si kidogo.
6. Waathirika wa ugonjwa huu wanajigharimia wenyewe matibabu.
7. Serikali haitambui kuathirika kwa watu na ugonjwa huu ndiyo maana ya kuwaongezea tozo na kodi zaidi ndani ya janga hili.
8. Serikali inatoa chanjo bila kuzingatia masharti wala vigezo vyovyote kinyume na maelekezo ya mtengeneza chanjo.

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

Badala ya kuwahami watu chanjo na Corona kwa serikali amekuwa ni mwendelezo wa siasa.
 
RC na DC ni wenyeji wa kamati za ulinzi na usalama ktk maeneo yao

Wizara hazina kamati za ulinzi? Mbona hata chikeni pati zinazo. Serikali iipe kibali wizara ya Afya angalau iwe na kamati ya ulinzi ya maslahi ya chanjo.
 
All the science za safety, efficacy na effectiveness zimeshatolewa… unfortunately you don’t listen because you have already fixed your mind towards a certain direction

on the safety ya long term … unataka virtual or actual, because actual data pick as the timelines elapse
Nitake Virtual data kwani tupo kwenye video game? Kwahiyo sisi mnataka kutufanya ‘actual’ rats wa kupata ‘actual’ data sivyo baada ya miaka 10 sivyo? No thanks.
 
All the science za safety, efficacy na effectiveness zimeshatolewa… unfortunately you don’t listen because you have already fixed your mind towards a certain direction

on the safety ya long term … unataka virtual or actual, because actual data pick as the timelines elapse
Nani katoa? Bongo bwana utakuta bwana shamba anaongelea issue za electronics...ajabau ajabu!
 
Tatizo Gwajima wa kiume anafurahia hii ligi. Anajua yeye huwa anaongea na watu ambao wameshakubaliana naye kwa kila kitu kabla hata hajaongea.
Angekuwa ananisikia, ningemkumbusha tu kuhusu jambo ambalo analijua; Kuwa siku zote Utukufu ni kwa Mungu na sio sisi binadamu.
 
Serikali haina dhamira ya dhati kupambana na ugonjwa huu ambao death toll yake hakuna asiyeiona:

1. Waliopotosha ugonjwa awamu ile ndiyo wale wale ambao leo eti ni vinara wa kupambana nao.
2. Mikusanyiko ya watu ikiwamo mbio za mwenge, makanisani, misikitini, kwenye mabasi, masokoni, magulioni nk iko pale pale na bila tahadhari zozote kuchukuliwa.
3. Hakuna takwimu zinazotolewa kuhusiana na ugonjwa huu kiasi haieleweki tuko wapi na tunakwenda wapi.
4. Haupo mkakati wowote ulio wazi wa kupambana na ugonjwa huu.
5. Kupimwa Corona inaendelea kuwa ni kwa pesa na si kidogo.
6. Waathirika wa ugonjwa huu wanajigharimia wenyewe matibabu.
7. Serikali haitambui kuathirika kwa watu na ugonjwa huu ndiyo maana ya kuwaongezea tozo na kodi zaidi ndani ya janga hili.
8. Serikali inatoa chanjo bila kuzingatia masharti wala vigezo vyovyote kinyume na maelekezo ya mtengeneza chanjo.

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

Badala ya kuwahami watu chanjo na Corona kwa serikali amekuwa ni mwendelezo wa siasa.
Wamwachie mwenyekiti MBOWE hatutaki hayo mazingaombwe yao. Waondoe tozo onevu na za kinyonyaji.,Watupatie Katiba mpya... Tunachoshwa na maigizo yao yasiyo na kichwa wala mkia!!!
 
Back
Top Bottom