#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Gwajima alikuwa anatumia chanjo kutaka kutrend/kiki ili aendelee kuzungumzwa maana tangu ile movie watanzania walianza kumsahau.
 
Gwajima hana maadili na huo uasikofu wake ni utapeli tu,nashangaa Sana Kuna watu Bado wanamuamini Askofu tapeli.Yeye taaluma ya udaktari wa binadamu hana eti ndo anapinga chanjo ya korona kwa fake facts .Ina maana Gwajima ndo ana akili kuliko wanasayansi wote duniani aache uhuni wake.
Wewe unanjua sifa za kuwa Askofu, au unabwabwaja tu?
 
Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa naagiza akamatwe popote na akahojiwe juu ya haya madai - Dk. Gwajima
--
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
acha wafu wazikane
 
Gwajima ni mhuni tu Hana maadili kwa nchi ambazo Zina sheria za maadili huyu jamaa hakifaa kuwa mbunge,na pia ni tapeli na mlaghai ashandanganya anafufua watu ,rejea kisa cha Amina chifupa.Inaskitsha sn Kuna watu Bado wanamuamini.
Hata Mimi bado najiuliza hivi anapowadanganya waumini wake na wanapiga vigelegele akiri wanakua wamepeleka wapi jamani hivi kwenye jukwaa hill hakuna muumini wa gwajima aje atuambie wakati bwana gwajima anapojimwambafai kanisani.akiri zake yeye binafsi anakua amepeleka wapi?
 
Maneno ya Yesu Kristo Math. 10: 34 - 39 yanatimia kwa mshindo mkuu

"....sikuleta amani duniani Bali mafarakano kati ya mtu na ndugu yake...............

SOMA MISTARI YOTE
 
Leseni hiyo hiyo aliyotumia kutoa expert opinion ya kuwa dawa ni maji, sijui zimewekewa nini aruhusiwe kuendelea nayo kwenye kuthibitisha.

Aende kuchezea centrifuge huko maabara na test tube kuthibitisha madai yake. Yeye si anajua sana nini kimo ndani ya hizo vaccine kushinda wataalamu wa afya.

Serikali itajibu vipi madai yake bila ya yeye kuthibitisha kwanza uhalali wenyewe.

Gwajima asipotokea itatufanya tumuone muongo kweli kweli.
Nimecheka kwa sauti,nimefanya imagination Gwajima kamwagina makemiko kibao pamoja na vifaa kibao anabaki anatetemeka hajui achukue kemiko ipi aache ipi.Hajui achanganye nini.Kabaki katumbua macho tu.Anaongea Story zake atueleze kama anaweza kuthibitisha
 
Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa naagiza akamatwe popote na akahojiwe juu ya haya madai - Dk. Gwajima
--
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
Jibuni hoja kwa hoja na si kuweweseka kumkamata Josepht.
Wakati wa Magufuli ni nyie hao hao mlokuwa mstari wa mbele kuungana naye kupinga chanjo.Wewe waziri wa afya ulionyesha mifano mingi na kusisitiza matumizi malimao,vitunguu,pilipili na takata nyingine nyingi,pamoja na kupiga nyungu kuwa ndo dawa za korona.Mlikwenda hata kuchukua uchafu mwingine kule Madagascar kwa ndege ya serikali.Sasa toeni proof za kisayansi kudhibitisha kwamba chanjo ni salama na si kusumbua wale wanaosema si salama kwa maana ninyi tangu mwanzo mlituaminisha hivyo.
Acheni kuwa na double standard.
 
Huko mbele watu wanakosoa kuhusu chanjo, na wanamuweka mtu kati gavana wa jimbo kwenye mitahalo ya ana kwa ana, wala hakuna mtu anayekamatwa na FBI, PD etc na kwenda kuhojiwa...

Kwenye hili nimetumia mfano wa US kwa sababu kuna mambo mfano maisha baada ya uchaguzi, viongozi wetu wamekuwa wakitolea mfano wa namna viongozi mathalani wa US wanavyokuwa wamoja pimdi chaguzi zinapoisha...
 
Back
Top Bottom