#COVID19 Waziri Gwajima aagiza Askofu Gwajima kukamatwa ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya UVIKO-19

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,079
8,219
Askofu Gwajima ni shemeji yangu, lakini mimi waziri wa wananchi nimekula kiapo mbele ya Rais cha kutumiakia nchi, sio kumtumikia shemeji. Mimi ndiye msemaji wa masuala ya afya nchini, nimechoka kuvurugwa naagiza akamatwe popote na akahojiwe juu ya haya madai - Dk. Gwajima
--
Butiama.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Doroth Gwajima ameliagiza Jeshi la Polisi pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ( Takukuru) kumkamata na kumhoji mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima ili athibitishe kauli anazozitoa dhidi ya Serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko 19.

Dk Gwajima ametoa agizo hilo leo Jumanne Agosti 17, 2021 katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama akibainisha kuwa Askofu Gwajima amekuwa akitoa taarifa za kupotosha kwa makusudi jambo linaloivuruga wizara yake na Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

Credits: Mwananchi

Pia soma
- #COVID19 - Dkt. Mollel: Askofu Gwajima ataitwa athibitishe kauli zake, akishindwa tutamshughulikia
 
Wanataka kukata tawi lote, kisha kulichoma. Walikate tu wasilichome kwa sababu matunda yaliyo kwenye tawi hilo yameishakomaa na mbegu zake zaweza kusaidia kuotesha miche mingine ya mti huo.

Chonde chonde msikate na kuchoma tawi hilo! Mkitumia jicho la tatu mwaweza kung'amua kuwa hakuna haja ya kukata tawi hilo achilia mbali kuwaza kulichoma.
 
Askofu Gwajima hajaanza leo kuzungumzia masuala ya Chanjo, na mara ya mwisho alisema libaki suala la hiari ila yeye msimamo wake na wanaomfuata ni kuwa hawatochanja mpaka wathibitishiwe kilichopo kwenye chanjo. Akawa amemaliza na mjadaka ukaisha kila mtu ametua akili zake kuamua

Kitendo cha Waziri leo kutoa amri ya kukamatwa Gwajima ni dalili moja wapo za hujuma anazofanya kuzorotesha utoaji huduma za chanjo kwa kuendeleza mjadala, ubishani na sintofagamu, watu walishasikiliza wakang'amua waliomua kuchanja wakachanja waliokataa wamekataa anachofanya sasa ni kama kuirudisha tena sinema ile na kuendeleza sintofahamu hiyo makusudi

Leo hii Mama hayupo, anatoa amri shemeji yake ( kaka wa mume wake) akamatwe wakati hakuna kiongozi wa mkubwa yeyote wala wa vyombo vya dola aliyewahi kuagiza akamatwe kwa sababu ni suala la hoja. Tuko tunajadili mengine tunarudishwa nyuma tena mjadala wa Askofu Gwajima na chanjo

Kama unaona misimamo yako ya sasa inakinzana na uliyokuwa nayo utawala uliopita kaa pembeni, jiuzulu au nenda kamwambie Mama unaomba upumzike.
 
Kujiita askofu ni kuchafua hadhi ya uaskofu, kuwa askofu kuna kanuni zake sio kujitangazia kiholela. Kamati iliyokaa na kumpa Gwagima uaskofu waliangalia sifa za uaskofu? Bila shaka hawakuangalia ndio maana anapayuka ovyo. Chungu ulimi wako mbele ya serikali.
 
Back
Top Bottom