#COVID19 Waziri Gwajima akamilisha barua ya kukamatwa kwa askofu Gwajima

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Nipashe inaripoti kuwa waziri wa afya Dorothy Gwajima amesema amewaandikia polisi barua ya kukamatwa kwa mchungaji josephat Gwajima.

Hii ni baada ya IGP kusema kuwa afuate hatua za kisheria

Soon mtasikia Gwajiboy ametiwa ndani

USSR

---
Amesema amekamilisha taratibu zote za kisheria ikiwamo kuandika barua rasmi kwa vyombo vya usalama ili vianze kumhoji Askofu Gwajima.

Juzi Dk. Dorothy aliomba vyombo vya usalama kumhoji Askofu Gwajima, lakini Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro, alisema jeshi hilo haliwezi kufanya kazi hiyo bila kupata barua rasmi kutoka katika mamlaka husika.

Akizungumzia kauli hiyo ya IGP Sirro, Dk. Dorothy alisema kiongozi huyo wa Jeshi la Polisi yupo sahihi kwa kuwa vyombo vya usalama haviwezi kuanza kumhoji mtu bila kupata malalamiko rasmi kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni yeye.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kuzungumza na watumishi wa Sekta ya Afya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali jijini Mwanza, waziri huyo alisema hakuagiza Askofu Gwajima akamatwe bali alitaka aitwe na kuhojiwa.

"Juzi nikiwa Butiama niliagiza vyombo vya usalama kumhoji Askofu Gwajima ili athibitishe madai yake kwamba viongozi wa serikali wamehongwa ili kuruhusu kuingiza chanjo ya UVIKO-19,'' alisema.

Alisema anataka Askofu Gwajima aitwe na kuhojiwa ili aeleze nani kahongwa, lini alihongwa, wapi alipewa fedha hizo na zilikuwa kiasi gani.

Kuhusu upotoshaji wa chanjo ya UVIKO-19, waziri huyo alisema kuna watu wengi wanapotosha suala hilo na kwamba kila mtu mwenye simu, atafute habari zake na kuzisoma ili afanye uamuzi badala ya kusikiliza mambo ya watu.

Dk. Dorothy alisema mtu akichanjwa ni rahisi mwili wake kupambana na ugonjwa wa corona kama ukimpata kuliko yule ambaye hajachanja.

“Wengi hawakusikiliza kipindi cha awamu ya tano, ndiyo maana wanauliza mbona mlisema hivi, Hayati Rais John Magufuli katika hotuba yake alisema msiwe mnakimbilia chanjo hadi mjiridhishe, hakusema msichanje," alisema.

Waziri huyo alisema kuna watu wanatembea na kivuli cha Hayati Rais Magufuli kwa kuwa na ajenda zao zinazopotosha.

Akizungumzia tiba asili, alisema chanjo haifuti tiba hizo na kuwapiga marufuku watu wanaogeuza Wizara ya Afya kuwa ajenda ya kisiasa.

Kuhusu takwimu za vifo vilivyotokana na ugonjwa wa corona, Dk. Dorothy alisema bado zinaandaliwa na muda siyo mrefu zitatolewa kwa nchi nzima.

"Hizi takwimu tunazo, zikiwa tayari zitatolewa kwa nchi nzima kwa sababu zipo wazi na kila mtu ataziona na kuzisoma,'' alisema.

Katika hatua nyingine, waziri huyo alizungumzia ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Mwanza (Sekou Toure), akisema serikali imepitisha bajeti ya Sh. bilioni sita kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa ajili ya kumalizia jengo hilo.

Aliagiza kufikia Desemba mwaka huu jengo hilo liwe limekamilika na kuanza kutoa huduma kwa mama wajawazito.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel akizungumza hospitalini hapo, alisema jengo hilo lipo katika hatua nzuri na kumwomba Dk. Gwajima kuwaongezea fedha kwa ajili ya kukamilisha ili kufikia Desemba lianze kutoa huduma.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Bahati Peter, alisema ujenzi huo ulianza Oktoba 2017 chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na gharama za mradi ni Sh. bilioni 10.1 na kwamba fedha zilizopokewa hadi sasa ni Sh. bilioni 9.8.

Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Mwanza, Bernad Mayemba, alisema ujenzi huo umefanyika kwa mfumo wa ujenzi na usimamizi kwa kufuata mchoro na kuzingatia ubora wa vifaa vilivyotumika.

Chanzo: Nipashe
 
Nahisi kwamba huyu waziri na shemeji yake wana matatizo ya shemeji-shemeji ambayo wanayaleta kwenye uwanja wa siasa na dini. Inawezekana kuna chuki hapa, labda Gwajima mwanaume anaona Gwajima waziri anamnyanyasa na kumfunika sana mdogo wake, na hasira zake kwa waziri shemeji anazileta kwenye chanjo.

Na pia inawezekana labda waziri kabla maisha hayajawaendea vema na mumewe Gwajima mbunge alikuwa akikataa kuwasaidia, na ndio maana anamfanyia hizi mbofumbofu.

Sasa ushauri wetu kwao ni kwamba wakamalize matatizo yao kifamilia, sio kunufaisha majukwaa, sijui mkono wa bouncer. Habari ya kujua ulikuwa mkono wa Gwajima, wa bouncer au wa mtoto sijui msituletee hadharani, mnajuana wenyewe mtu na shemeji yake.
 
Tuhuma lazima zithibitishwe, na wakiamua kuacha hili lipite kimya kimya kwa tabia ya CCM kubebana tutaamini kweli Rais alihongwa.
 
Kamwe usijaribu kujibizana na mwanamke...kama ni mkeo,atakaa dirishani aseme,apayuke ili majirani na wapita njia wasikie siri zako!

Pole mchungaji...Sasa hivi unapambana na shemejio! Tutasikia mengi. Na 'wataibuka washindi'
 
Nipashe inaripoti kuwa waziri wa afya Dorothy Gwajima amesema amewaandikia polisi barua ya kukamatwa kwa mchungaji josephat Gwajima.

Hii ni baada ya IGP kusema kuwa afuate hatua za kisheria

Soon mtasikia Gwajiboy ametiwa ndani

USSRView attachment 1898106
Nae anatutia aibu kwa kusema lugha za aibu kwenye vyombo vya habari hadi tunaona aibu kukaa na watoto setu sebuleni,lugha za kutest mitambo ni lugha za kihuni kunenwa na kiongozi
 
Nae anatutia aibu kwa kusema lugha za aibu kwenye vyombo vya habari hadi tunaona aibu kukaa na watoto setu sebuleni,lugha za kutest mitambo ni lugha za kihuni kunenwa na kiongozi
Ila unasikiliza miziki yenye matusi na madansa wako uchi na wanao

USSR
 
Umeandika kishabiki zaidi Bila uhalisia

IGP alitamka wazi kuwa si tu kuandika barua kutamkamatisha Gwajima Bali polisi wataangalia kama kuna jinai yeyote ya ku warrant kukamtwa kwake

Wewe umeshatoa conclusion very sad weledi umepotelea kwenye ushabiki
 
Nahisi kwamba huyu waziri na shemeji yake wana matatizo ya shemeji-shemeji ambayo wanayaleta kwenye uwanja wa siasa na dini. Inawezekana kuna chuki hapa, labda Gwajima mwanaume anaona Gwajima waziri anamnyanyasa na kumfunika sana mdogo wake, na hasira zake kwa waziri shemeji anazileta kwenye chanjo.

Na pia inawezekana labda waziri kabla maisha hayajawaendea vema na mumewe Gwajima mbunge alikuwa akikataa kuwasaidia, na ndio maana anamfanyia hizi mbofumbofu.

Sasa ushauri wetu kwao ni kwamba wakamalize matatizo yao kifamilia, sio kunufaisha majukwaa, sijui mkono wa bouncer. Habari ya kujua ulikuwa mkono wa Gwajima, wa bouncer au wa mtoto sijui msituletee hadharani, mnajuana wenyewe mtu na shemeji yake.
Kwa wenye akili na uelewa wa mambo ya siasa wala hatushangazwi na haya. Kwa sasa hakuna anaemuongelea Mbowe wala kufikiria kuandamana kwa ajili yake. I mean akili na masikio yote ya bavicha yamehamia kwenye ugomvi wa kina Gwajima, huku likitengenezwa tukio lingine kupitia Sabaya au someone else.
 
Nahisi kwamba huyu waziri na shemeji yake wana matatizo ya shemeji-shemeji ambayo wanayaleta kwenye uwanja wa siasa na dini. Inawezekana kuna chuki hapa, labda Gwajima mwanaume anaona Gwajima waziri anamnyanyasa na kumfunika sana mdogo wake, na hasira zake kwa waziri shemeji anazileta kwenye chanjo.

Na pia inawezekana labda waziri kabla maisha hayajawaendea vema na mumewe Gwajima mbunge alikuwa akikataa kuwasaidia, na ndio maana anamfanyia hizi mbofumbofu.

Sasa ushauri wetu kwao ni kwamba wakamalize matatizo yao kifamilia, sio kunufaisha majukwaa, sijui mkono wa bouncer. Habari ya kujua ulikuwa mkono wa Gwajima, wa bouncer au wa mtoto sijui msituletee hadharani, mnajuana wenyewe mtu na shemeji yake.
By the way,huwa ni vita ngumu sana kupambana na mwanamke.hasa mwenye kariba(sema tena kariba) ya mwambao wa pwani siyo kabira .Ndiyo naona type ya Dr.Doroth Gwajima,yaani mwanamke wa wa type hiyo huwa anapenda zogo,hasa "kujaza watu kwenye zogo lake,furaha yake ni pale watu wanaoshangaa wanapokuwa wengi" Kama unabisha nenda ukaangalie show za Geah tv . Askofu atakuwa provoked soon,kiasi akapoteza credibility hiyo ndogo iliyobaki.
 
I say, huyu mama anaupepeta sishangai hawaelewani na shemeji yake. Namuonea huruma huyo Gwajima junior. Hivi anaweza hata kumwambia niletee chakula kweli? Pepepepepepepepepeepepepepeeeeeee!!! Kapakue mwenyewe jikoni.
 
Back
Top Bottom