Waziri Dkt. Mwigulu atoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu na kuleta mkanganyiko kwa wananchi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha bungeni wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kuleta mkanganyiko kwa wananchi ikiwemo makato ya miamala ya simu, kodi ya majengo kwa njia ya Luku na Makato yanayopendekezwa ya mafuta kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kodi hizo zimetafsiriwa kinyume na lengo la Serikali, ambapo kwenye kodi ya kuongeza salio mtu akiweka kuanzia Sh. 1000 hadi Sh. 2500, atatozwa shilingi 10, shilingi 2500 hadi 5000 atatozwa Sh. 21, shilingi 50,000 hadi 100,000 atatozwa shilingi 186 na shilingi 100,000 kwenda juu anatozwa shilingi 200 na sio kila siku ni pale anapoweka mudawa maongezi.

“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

Akielezea kuhusu kodi ya miamala ya simu Dkt. Nchemba alisema kuwa kila mwananchi atakaopofanya miamala kwenye simu chini ya shilingi 1000 kodi hiyo haiwahusu, kuanzia shilingi 1000 hadi 2000 atatozwa shilingi 10, shilingi 10,000 hadi 15,000 atatozwa shilingi 300, shilingi 30,000 na kuendelea atatozwa shilingi 1000 na shilingi milioni tatu na kuendelea watatozwa shilingi 10,000.

Kuhusu Kodi ya Majengo kwa kutumia LUKU alisema kuwa mfumo huo mpya unatumika katika nchi nyingi Duniani na unarahisisha ukusanyaji wa mapato kuliko mfumo uliokuwepo ambao unawafanya watu kutumia muda mwingi kwenye foleni.

Kwa upande wa kodi katika mafuta, alisemaongezeko la kodi hiyo itasaidia kukarabati, kujenga na kufufua barabara ambazo ni muhimu katika usafiri na usafirishaji.

Alisema kutumia barabara mbovu ni gharama kubwa kuliko ongezeko la kodi hiyo kwenye mafuta, akitolea mfano wa vifo vya wakinamama wajawazito wanopokwenda kujifungua kutokana na ubovu wa barabara hizo.

Kwa kuwafuata walipa kodi kwajia ya kawaida hatuzidi watu laki mbili, kwa kutumia Mita za umeme watu wamezidi milioni tatu kwa hiyo tukaona kwa nini tusitumie utaratibu huu wa digitali ili kuwaondolea watu usumbufu.

Waziri Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha zitakazopatikana katika kodi hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika kama mfuko wa Barabara na elimu hivyo kutumika kwa kusudi lililowekwa.

Kwa upande wao wahariri walioshiriki semina hiyo wamempongeza Waziri Dkt. Nchemba pamoja na uongozi wa Wizara kwa kutoa ufafanuzi huo na kuomba kuendelea na utaratibu huo ili kuondoa mikanganyiko kwa wananchi.

Chanzo: Mpekuzihuru
 
Mbona hajasema kuanzia elf 5 mpaka elf 50 tutalipa shs ngapi? pia hiyo miradi tuliulizwa wananchi au ni wao na dikteta walikaa wakaamua? sababu siyo lazima mambo yote yaishe kwa wakati mmoja tungeweza kumaliza reli au bwawa la umeme kwanza ndiyo kingine kikafuata. wapuuzi kabisa
 
Ufafanuzi wa kodi ya majengo kupitia LUKU haueleweki, ni mfupi mno. Wazee wenye umri wa miaka 60 wataondolewa vipi kwani hawatakiwi kulipa kodi hiyo, Wenye majengo yasiyo na umeme watalipia vipi. Kodi ya jengo ni ya mpangaji au mmiliki, kama ni ya mmiliki hawa wapangaji ambao ndiyo hulipa LUKU si watalipa kodi isiyo yao?

Hao wastaafu ambao serikali ilikopa fedha zao na kuziingiza kwenye miradi iliyokwama kama ule wa mbigiri, watalipaje kodi ya majengo wakati fedha zao umesema unaziingiza kwenye hati fungani (aina nyingine ya deni kwa serikali) - eti hiyo inakwenda kumaliza tatizo lao!! Shame kabisa. Kwani hati fungani zikiiva lazima serikali ilipe? si inaweza kuzibadilisha zikawa za muda mrefu zaidi? Hayo wadanganye wasiojua

Suala la kodi kwenye laini kuwa kwa siku alilisema mwenyewe, au ameona mbwembwe zake pale bungeni zinaanza kumletea shida. Aseme tu kuwa aliteleza. Wenye uwezo wataweka Clip hapa
 
Kodi ni kodi, haijawahi kutokea binadamu akapenda sana kulipa kodi. Tujitahidi kulipa kwa maendeleo ya Taifa letu na "Viongozi wetu".
 
Naona Kuna watu wanataka kukwepa kulipa Kodi!!!as long as sipendi direct taxes na wewe unatumia indirect taxes,Dr Mwigulu ntakuunga mkono 💯%!direct taxes zinaleta usumbufu Sana!Ila tunawataka hiyo pesa mtakayokusanya ikafanye shughuli zilizokusudiwa siyo tena muanze kuendekeza ulafi na ubinafsi!!
 
Kodi Kwenye luku tangu awamu ya JPM ilikuepo.

Sema waliificha kimya KIMYA kwa mfumo wa unaponunua luku kupitia simu, salio liliobaki hawakuletei Kama ilivyo miamala mingine.

Na ndo Mana ukiwa na Ela kamili mf: 10,000 HUWEZ kununua umeme wa 10,000.

Lazima uwe na Ela ya ziada ili wakate Kodi yao.

Sema Kama wanaongeza Kodi nyingine,
Ni kuzidi kutuumiza Sana watanzania.
 
Hongera Sana Waziri wa Fedha, nchi yetu bado ni changa, wananchi shine tulipe Kodi...!
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha bungeni wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kuleta mkanganyiko kwa wananchi ikiwemo makato ya miamala ya simu, kodi ya majengo kwa njia ya Luku na Makato yanayopendekezwa ya mafuta kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kodi hizo zimetafsiriwa kinyume na lengo la Serikali, ambapo kwenye kodi ya kuongeza salio mtu akiweka kuanzia Sh. 1000 hadi Sh. 2500, atatozwa shilingi 10, shilingi 2500 hadi 5000 atatozwa Sh. 21, shilingi 50,000 hadi 100,000 atatozwa shilingi 186 na shilingi 100,000 kwenda juu anatozwa shilingi 200 na sio kila siku ni pale anapoweka mudawa maongezi.

“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

Akielezea kuhusu kodi ya miamala ya simu Dkt. Nchemba alisema kuwa kila mwananchi atakaopofanya miamala kwenye simu chini ya shilingi 1000 kodi hiyo haiwahusu, kuanzia shilingi 1000 hadi 2000 atatozwa shilingi 10, shilingi 10,000 hadi 15,000 atatozwa shilingi 300, shilingi 30,000 na kuendelea atatozwa shilingi 1000 na shilingi milioni tatu na kuendelea watatozwa shilingi 10,000.

Kuhusu Kodi ya Majengo kwa kutumia LUKU alisema kuwa mfumo huo mpya unatumika katika nchi nyingi Duniani na unarahisisha ukusanyaji wa mapato kuliko mfumo uliokuwepo ambao unawafanya watu kutumia muda mwingi kwenye foleni.

Kwa upande wa kodi katika mafuta, alisemaongezeko la kodi hiyo itasaidia kukarabati, kujenga na kufufua barabara ambazo ni muhimu katika usafiri na usafirishaji.

Alisema kutumia barabara mbovu ni gharama kubwa kuliko ongezeko la kodi hiyo kwenye mafuta, akitolea mfano wa vifo vya wakinamama wajawazito wanopokwenda kujifungua kutokana na ubovu wa barabara hizo.

Kwa kuwafuata walipa kodi kwajia ya kawaida hatuzidi watu laki mbili, kwa kutumia Mita za umeme watu wamezidi milioni tatu kwa hiyo tukaona kwa nini tusitumie utaratibu huu wa digitali ili kuwaondolea watu usumbufu.

Waziri Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha zitakazopatikana katika kodi hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika kama mfuko wa Barabara na elimu hivyo kutumika kwa kusudi lililowekwa.

Kwa upande wao wahariri walioshiriki semina hiyo wamempongeza Waziri Dkt. Nchemba pamoja na uongozi wa Wizara kwa kutoa ufafanuzi huo na kuomba kuendelea na utaratibu huo ili kuondoa mikanganyiko kwa wananchi.

Chanzo: Mpekuzihuru
Hili ndo linahitaji na ufafanuzi sio hoja hata ulaya wanatumia, nani mlipaji kama nyumba moja na mita zaidi ya moja

Kafafanua vizuri,
Tutalipa Kodi kwa maendeleo ya nchi yetu, madhali yule dhalimu kwasasa ayupo, Tutaipenda zaidi nchi yetu
 
Kodi Kwenye luku tangu awamu ya JPM ilikuepo.

Sema waliificha kimya KIMYA kwa mfumo wa unaponunua luku kupitia simu, salio liliobaki hawakuletei Kama ilivyo miamala mingine.

Na ndo Mana ukiwa na Ela kamili mf: 10,000 HUWEZ kununua umeme wa 10,000.

Lazima uwe na Ela ya ziada ili wakate Kodi yao.

Sema Kama wanaongeza Kodi nyingine,
Ni kuzidi kutuumiza Sana watanzania.
Ambacho hujaelewa ni nini? Hakuna anayesema kodi haikuwepo. Wanachoongeza hapo ni kodi ya majengo.
 
Watanzania tunataka maendeleo ila hatutaki kulipa kodi. Tunawalaumu wafanyabiashara kwa ukwepaji kodi utafikiri wako mil 50. Kumbe labda hawafiki hata asilimia 2 ya population yetu.
Tukumbuke kuwa maendeleo ya kweli ni ya kujiletea wenyewe. Sio haya ya kuomba omba na kukopa bila mipangilio. Tukomae kodi zetu zitumike vizuri. Wana siasa wasiwe na kazi ya kuanzisha project kama IPTL na kuruhusu ufujaji ndani ya taasisi za umma.
Halafu ndio tutafurahia maendeleo
 
Back
Top Bottom