Waziri Dkt. Mwigulu atoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu na kuleta mkanganyiko kwa wananchi

Wameacha kukwapua pesa Kutoka kwa akaunti zetu, sasa wanazichukua kwa kisheria zaidi. Kodi ya majengo kupitia Luku ni wizi wa wazi kabisa. Kama nyumba ina mita za Luku Zaidi ya moja ina maana kila mita Itakatwa Kodi ya jengo.
Unataka maendeleo hutaki changia
 
Naona Kuna watu wanataka kukwepa kulipa Kodi!!!as long as sipendi direct taxes na wewe unatumia indirect taxes,Dr Mwigulu ntakuunga mkono %!direct taxes zinaleta usumbufu Sana!Ila tunawataka hiyo pesa mtakayokusanya ikafanye shughuli zilizokusudiwa siyo tena muanze kuendekeza ulafi na ubinafsi!!
Lipa kodi tupate pesa za kuwalipa akina Halima Mdee miposho wawapo bungeni
 
Watanzania tunataka maendeleo ila hatutaki kulipa kodi.
Je una habari kuwa wanaotafuna mabilioni ya kodi zetu bila kulala kama nzige hawalipi kodi? Ni upumbavu kuwalipisha kodi wanaohangaika juani kwa nguvu zao wakitafuta pesa huku wanasiasa na wagonga meza bungeni, wanaokula jasho letu kivulini kwenye viyoyozi, hawalipi hata senti. Inashangaza, inaudhi na inasikitisha...!
 
Wengine hata vyama vya siasa hawana wanakula mpunga wanajua mandondocha yatalipa tu
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha bungeni wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kuleta mkanganyiko kwa wananchi ikiwemo makato ya miamala ya simu, kodi ya majengo kwa njia ya Luku na Makato yanayopendekezwa ya mafuta kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kodi hizo zimetafsiriwa kinyume na lengo la Serikali, ambapo kwenye kodi ya kuongeza salio mtu akiweka kuanzia Sh. 1000 hadi Sh. 2500, atatozwa shilingi 10, shilingi 2500 hadi 5000 atatozwa Sh. 21, shilingi 50,000 hadi 100,000 atatozwa shilingi 186 na shilingi 100,000 kwenda juu anatozwa shilingi 200 na sio kila siku ni pale anapoweka mudawa maongezi.

“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

Akielezea kuhusu kodi ya miamala ya simu Dkt. Nchemba alisema kuwa kila mwananchi atakaopofanya miamala kwenye simu chini ya shilingi 1000 kodi hiyo haiwahusu, kuanzia shilingi 1000 hadi 2000 atatozwa shilingi 10, shilingi 10,000 hadi 15,000 atatozwa shilingi 300, shilingi 30,000 na kuendelea atatozwa shilingi 1000 na shilingi milioni tatu na kuendelea watatozwa shilingi 10,000.

Kuhusu Kodi ya Majengo kwa kutumia LUKU alisema kuwa mfumo huo mpya unatumika katika nchi nyingi Duniani na unarahisisha ukusanyaji wa mapato kuliko mfumo uliokuwepo ambao unawafanya watu kutumia muda mwingi kwenye foleni.

Kwa upande wa kodi katika mafuta, alisemaongezeko la kodi hiyo itasaidia kukarabati, kujenga na kufufua barabara ambazo ni muhimu katika usafiri na usafirishaji.

Alisema kutumia barabara mbovu ni gharama kubwa kuliko ongezeko la kodi hiyo kwenye mafuta, akitolea mfano wa vifo vya wakinamama wajawazito wanopokwenda kujifungua kutokana na ubovu wa barabara hizo.

Kwa kuwafuata walipa kodi kwajia ya kawaida hatuzidi watu laki mbili, kwa kutumia Mita za umeme watu wamezidi milioni tatu kwa hiyo tukaona kwa nini tusitumie utaratibu huu wa digitali ili kuwaondolea watu usumbufu.

Waziri Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha zitakazopatikana katika kodi hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika kama mfuko wa Barabara na elimu hivyo kutumika kwa kusudi lililowekwa.

Kwa upande wao wahariri walioshiriki semina hiyo wamempongeza Waziri Dkt. Nchemba pamoja na uongozi wa Wizara kwa kutoa ufafanuzi huo na kuomba kuendelea na utaratibu huo ili kuondoa mikanganyiko kwa wananchi.

Chanzo: Mpekuzihuru
Yaani huyu mtu sijui kasoma uchumi upi! Yaani kila nikununua muda wa maongezi nakatwa halafu anasema siyo mzigo! Hii miradi si walisema wana hela! Mwendazake kaondoka nazo? Mbona kodi tunalipa nyingi tu! Kama vipi hiyo miradi waisitishe kama hawana hela. Mbona wao wabunge hawalipi kodi? Kwanini wao hawaonyeshi uzalendo? Uzalendo ni sisi tu wananchi?
 
Sijaona Shida hapo, pesa kidogo sana hiyo ndugu zangu tulipe Kodi nchi iende mbele
 
Mbona hajasema kuanzia elf 5 mpaka elf 50 tutalipa shs ngapi? pia hiyo miradi tuliulizwa wananchi au ni wao na dikteta walikaa wakaamua? sababu siyo lazima mambo yote yaishe kwa wakati mmoja tungeweza kumaliza reli au bwawa la umeme kwanza ndiyo kingine kikafuata. wapuuzi kabisa
Tena sana!!!!
 
Angetoa na pendekezo la kupunguza mishahara yao na kuweka kodi kwenye kiwango kitakacho salia na kupunguza kiwango cha pesa kwenye kiinua mgongo ,Ili kuonesha kwa vitendo kwamba wanataka kufanikisha hiyo miradi, sio kutufinya wananchi peke yetu
 
Nyumba nilopanga tuko wapangaji wawili na kila mmoja ana mita yake sasa tutalipaje hiyo kodi ya majengo.
Hafu mita yenyewe ina jina la mpangaji wa zamani
Hiyo ni advantage kwa serikali kama nyumba itakuwa na mita zaidi ya moja, pia inajazilizia nyumba zisizokuwa na Umeme, cha muhimu kuliko vyote wigo wa mapato umepanuka.
 
Inasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
 
Watanzania tunataka maendeleo ila hatutaki kulipa kodi. Tunawalaumu wafanyabiashara kwa ukwepaji kodi utafikiri wako mil 50. Kumbe labda hawafiki hata asilimia 2 ya population yetu.
Tukumbuke kuwa maendeleo ya kweli ni ya kujiletea wenyewe. Sio haya ya kuomba omba na kukopa bila mipangilio. Tukomae kodi zetu zitumike vizuri. Wana siasa wasiwe na kazi ya kuanzisha project kama IPTL na kuruhusu ufujaji ndani ya taasisi za umma.
Halafu ndio tutafurahia maendeleo
Inasikitisha sana MBUNGE anapata MSHAHARA wa Sh.Mil.11 na KIINUA MGONGO cha Sh.Mil.200 na Hakatwi KODI na huo Mshahara na Kiinua Mgongo ni KODI za WANANCHI leo Anasimama MBUNGE na Kudai Wananchi Wakatwe KODI ya UZALENDO .Kama ni UZALENDO anzeni nyinyi WABUNGE wenye MISHAHARA ya MAMILIONI Kukatwa Pesa na Ziende kwenye MIRADI ya MAENDELEO Majimboni Kwenu Huo Utakuwa UZALENDO.Wananchi Wanyonge na Masikini Mnawarundikia UTITIRI wa KODI nyinyi MNASTAREHE kwa MISHAHARA MINONO na MAGARI Mazuri Hebu Waoneeni Huruma Wapiga KURA
 
Je una habari kuwa wanaotafuna mabilioni ya kodi zetu bila kulala kama nzige hawalipi kodi? Ni upumbavu kuwalipisha kodi wanaohangaika juani kwa nguvu zao wakitafuta pesa huku wanasiasa na wagonga meza bungeni, wanaokula jasho letu kivulini kwenye viyoyozi, hawalipi hata senti. Inashangaza, inaudhi na inasikitisha...!
Nafikiri sasa wawe wanawajibishwa. Shida yetu tumeruhusu wawe untouchables. Suala la kulipa kodi sio suala la bargaining. Ni la lazima.
Kuhusu matumizi ya kodi, wananchi tuwabane wakusanya kodi watumie kwa weledi. Wafujaji wawajibishwe na sio wanalindwa.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ametoa ufafanuzi wa baadhi ya tozo alizowasilisha bungeni wakati wa Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kuleta mkanganyiko kwa wananchi ikiwemo makato ya miamala ya simu, kodi ya majengo kwa njia ya Luku na Makato yanayopendekezwa ya mafuta kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Dkt. Nchemba alisema kuwa kodi hizo zimetafsiriwa kinyume na lengo la Serikali, ambapo kwenye kodi ya kuongeza salio mtu akiweka kuanzia Sh. 1000 hadi Sh. 2500, atatozwa shilingi 10, shilingi 2500 hadi 5000 atatozwa Sh. 21, shilingi 50,000 hadi 100,000 atatozwa shilingi 186 na shilingi 100,000 kwenda juu anatozwa shilingi 200 na sio kila siku ni pale anapoweka mudawa maongezi.

“Hatujaweka kodi kwenye laini za simu kama ambavyo baadhi ya wananchi wamekuwa wakichanganya, hata kule Bungeni wanachanganya wanasema sasa kila siku itakuwa inakatwa shilingi 10 mpaka 200 kwa hiyo kama ni 200 kwa siku 30 ni shilingi 6000, halafu hata kama hukuweka fedha, siku ukiweka inakatwa kama nipige tafu, hatukuweka hivyo”, alieleza Dkt. Nchemba.

Alibainisha kuwa haimaanishi kwamba shilingi 10 sio mzigo lakini Serikali iliangalia matatizo yaliyopo na kugundua kuwa yanagharimu zaidi, kuliko thamani ya shilingi 10 itakayotozwa kama kodi.

Alifafanua kuwa miradi mikubwa inayotekelezwa nchi ukiwemo wa mradi wa Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere ambao unahitaji zaidi ya shilingi trililioni nne na ujenzi wa Reli ya Kisasa unaohitaji zaidi ya shilingi trilioni 20 ili kukamilika, iwapo fedha zote zitategemea mikopo nchi itapitiliza uwezo wa kukopa na kutokukopesheka hivyo ushiriki wa wananchi ni muhimu.

Akielezea kuhusu kodi ya miamala ya simu Dkt. Nchemba alisema kuwa kila mwananchi atakaopofanya miamala kwenye simu chini ya shilingi 1000 kodi hiyo haiwahusu, kuanzia shilingi 1000 hadi 2000 atatozwa shilingi 10, shilingi 10,000 hadi 15,000 atatozwa shilingi 300, shilingi 30,000 na kuendelea atatozwa shilingi 1000 na shilingi milioni tatu na kuendelea watatozwa shilingi 10,000.

Kuhusu Kodi ya Majengo kwa kutumia LUKU alisema kuwa mfumo huo mpya unatumika katika nchi nyingi Duniani na unarahisisha ukusanyaji wa mapato kuliko mfumo uliokuwepo ambao unawafanya watu kutumia muda mwingi kwenye foleni.

Kwa upande wa kodi katika mafuta, alisemaongezeko la kodi hiyo itasaidia kukarabati, kujenga na kufufua barabara ambazo ni muhimu katika usafiri na usafirishaji.

Alisema kutumia barabara mbovu ni gharama kubwa kuliko ongezeko la kodi hiyo kwenye mafuta, akitolea mfano wa vifo vya wakinamama wajawazito wanopokwenda kujifungua kutokana na ubovu wa barabara hizo.

Kwa kuwafuata walipa kodi kwajia ya kawaida hatuzidi watu laki mbili, kwa kutumia Mita za umeme watu wamezidi milioni tatu kwa hiyo tukaona kwa nini tusitumie utaratibu huu wa digitali ili kuwaondolea watu usumbufu.

Waziri Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha zitakazopatikana katika kodi hizo zitawekwa moja kwa moja kwenye mifuko husika kama mfuko wa Barabara na elimu hivyo kutumika kwa kusudi lililowekwa.

Kwa upande wao wahariri walioshiriki semina hiyo wamempongeza Waziri Dkt. Nchemba pamoja na uongozi wa Wizara kwa kutoa ufafanuzi huo na kuomba kuendelea na utaratibu huo ili kuondoa mikanganyiko kwa wananchi.

Chanzo: Mpekuzihuru
This is rubbish
 
Back
Top Bottom