Waziri Aweso hivi unafahamu kwamba ni mwezi mzima sasa DAWASA hawajaunganisha maji kwa Wateja wapya?

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Habarini za Majukumu wadau,

Kama kichwa cha habari kisemavyo, mamlaka ya maji Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani (DAWASA) wameshindwa kuwaunganishia wateja wapya huduma ya maji kwa sababu wanadai vifaa hamna.

Specifically, binafsi nimefanya malipo ya kuunganishiwa huduma ya maji katka ofisi ya DAWASA KIBAHA TC takriban mwezi mmoja na wiki zimepita mpaka sasa huduma iyo haijafika ktk eneo langu bali na kulipia gharama za huduma iyo

Katika kufuatilia KERO hii nikafika pale maili moja DAWASA karani mmoja akasema vifaa bado havija fika mpaka leo.

Waziri Aweso na Naibu Waziri Marryprisca tutatulieni kero hii kwani hivyo vifaa vinatoka mbinguni Mpaka vichukue majuma yote hayo?
 
Mkuu mwez wa sita kuingia wa saba mara nyingi hua wanafunga mwaka, Hakuna kinachotoka hata tanesco kipind kama hiki kupata meter ni ngumu.

Kama mwez utaisha hivi hivi bas kutakua na matatzo mengne
 
Mkuu mwez wa sita kuingia wa saba mara nyingi hua wanafunga mwaka, Hakuna kinachotoka hata tanesco kipind kama hiki kupata meter ni ngumu..
Kama mwez utaisha hivi hivi bas kutakua na matatzo mengne
Kwa hiyo unataka kusema hata MSD hawa supply dawa ma hospitalin mwez huu kamaa wagonjwa kufa na wafe tuu

Iyo ni kitu mbaya sanaaa
 
Sambamba na hilo, Morogoro vifaa vipo ila vinauzwa na Mamlaka ya maji kwa bei mara mbili ya kawaida, vifaa ni vilevile, mtengenezaji ni yuleyule, ukiomboleza wanakwenda kuchukua kwenye maduka yao binafsi au ya mtu kati ambaye anagawana cha juu na watumishi wa Mamlaka
 
Kwa hiyo unataka kusema hata MSD hawa supply dawa ma hospitalin mwez huu kamaa wagonjwa kufa na wafe tuu

Iyo ni kitu mbaya sanaaa
Hahahaha mkuu nahis wanafanya assumption ukikosa umeme na maji kwa mwez t huwez kufa. Na wakianza kufunga foleni inakua nzito sana, lazma upitie shortcut ya kwa mpalange ili mambo yaende fasta..😁
 
Sambamba na hilo, Morogoro vifaa vipo ila vinauzwa na Mamlaka ya maji kwa bei mara mbili ya kawaida, vifaa ni vilevile, mtengenezaji ni yuleyule, ukiomboleza wanakwenda kuchukua kwenye maduka yao binafsi au ya mtu kati ambaye anagawana cha juu na watumishi wa Mamlaka
Yaani MORUWASA hio idara imeoza Sana aisee

Kama Kuna idara ya serikali imeoza kwa pale Moro Basi Ni idara ya maji Morogoro.

Yaani badala ya kufungulia Mabomba yatoe maji wanauza maji kwenye ma Bowser Yao binafsi mitaani wapige hela .

Ile idara Ni kuisafisha yote .

Kule kihonda kwenye Mabomba mapya maji yanatoka kwa wiki Mara moja tu .duuh aisee

Acheni tu kila waziri wa maji anakuja na kusepa hao watu wako

MORUWASA imeooza
 
Yaani MORUWASA hio idara imeoza Sana aisee

Kama Kuna idara ya serikali imeoza kwa pale Moro Basi Ni idara ya maji Morogoro..
Wanastawisha biashara zao kupitia ofisi ya umma, fikiria hata hayo maji hayatoki siku nzima, wanafungulia kwa masaa mawili au less, wazoefu huwa wanatoa tip kwa mfunguliaji anaongeza muda. Ni kama ile Mamlaka haina msimamizi, na Wizara haina Waziri
 
Acha tu hawajui Kama Kuna idara ya maji mbovu nchini Ni hio ya MORUWASA
 
Lakini Waziri wao anawalea, alishasikika akiwaomba fedha kipindi cha kampeni, kwa mwendo huo atawawajibisha?
Kama ndio hivyo wakazi wa Moro hasa kihonda yote Hadi makunganya kule ,nane nane tubuyu Hadi kingolwira watakoma

Ukiisha hayo maeneo unaweza utukana ule mji kila siku .

Unaweza pitisha siku hujaoga kisa maji hamna idara imeoza .

Yaani ningekuwa waziri wale watu ningewasafisha wote pumbavu zao
 
Jambo la kustaajabisha ukienda maeneo ya Kigurunyembe unakuta mabomba yamepasuka yanamwaga maji mitaani nobody cares
 
Mamlaka ya maji mbeya ni moja kati ya idara bora kabisa kwa nchi hii maana wako active muda wote,pongezi ziwafikie
 
Nakushauri pata kishoka akuunganishe na wale wafanyakazi wanaounganisha maji utaunganishiwa fasta... Vifaa vipo ila shida ni ukiritimba na pengine mlungula. Meneja aliyeondoka alikuwa the best ila hawa waliopo sasa... Mmh
 
Mfano hao DAWASA Kibaha TC,.wana namba zao za huduma kwa wateja izo namba kila ukipiga kuna mawili

Mosi, wapokee kisha wana kwambia njoo ofisi ukienda huko ofisi kwao hamna la maana wanacho kujibu ni porojo tupu.

..sasa mm huwa najiuliza ni nini maana ya kuweka namba za simu kitengo huduma kwa wateja ?

lakini mbili unaweza piga iyo namba then isipokelewe mpaka inakatika kisha haipatikani tenaaa

kiukweli Waziri aweso, na GM wa DAWASA Mr Cyprian Lubemeja do something kwa hawa watu wa Kibaha Tc ofisi ya Dawasa
 
Nakushauri pata kishoka akuunganishe na wale wafanyakazi wanaounganisha maji utaunganishiwa fasta... Vifaa vipo ila shida ni ukiritimba na pengine mlungula... Meneja aliyeondoka alikuwa the best ila hawa waliopo sasa... Mmh
Meneja yupi aliye ondoka ? Dawasa GM ni yule yule Cyprian
 
Mkuu mwez wa sita kuingia wa saba mara nyingi hua wanafunga mwaka, Hakuna kinachotoka hata tanesco kipind kama hiki kupata meter ni ngumu..
Kama mwez utaisha hivi hivi bas kutakua na matatzo mengne

Kwan walikua hawajui kama mwezi wa saba wanafunga dirisha ili wawe na stoku ya kutosha?
 
Back
Top Bottom