ACT Wazalendo: Kutofanyiwa kazi matatizo ya upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam; Tunamtaka Waziri wa Maji kuiwajibisha DAWASA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Kutofanyiwa kazi matatizo ya upatikanaji wa maji safi Dar es Salaam; Tunamtaka Waziri wa Maji kuiwajibisha DAWASA.

Utangulizi
Kwa muda wa miezi miwili Chama cha ACT Wazalendo kupitia Waziri Kivuli wa Maji imekuwa ikipokea changamoto juu ya hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa Mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya Kibaha, Bagamoyo ambayo yanahudumiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA). Changamoto zinazoelezwa ni za muda mrefu lakini Serikali kupitia DAWASA haijachukua hatua kushughulikia, hali inayopelekea kuwepo kwa wananchi wanaokosa huduma wanapohitaji, kuongezewa kwa gharama za kulipia huduma ya maji, kutotaribika kwa gharama na ukatikaji wa mara kwa mara. Changamoto hizo ni kama zifuatazo;

  • Kucheleweshwa kuunganishwa na huduma za maji;
  • mamlaka ya imekua ikichelewesha kuwaunganisha wateja na huduma ya maji hata baada ya kumaliza taratibu zote za malipo, Maeneo ya Kigamboni, kibaha, Pugu, Chanika, Gongo la mboto, Mlandizi na Bagamoyo wamekua wakicheleweshewa sana kuunganishwa na huduma za maji, malalamiko mengi yanaonesha kwamba inapita zaidi ya Miezi mitatu (3).

  • Kubambikiwa bili za maji;
  • Wateja wengi wamekuwa na malalamiko ya kuongezewa bili tofauti na matumizi yao au kupewa bili ambazo si za kwao tatizo hili limekuwa sugu na wananchi wanalazimika kulipa fedha hizo kutokana na kutokuwa na uwazi katika usomaji mita, na kusoma mita kwa makadirio. Malalamiko haya yanadhibitishwa pia na ripoti ya CAG kwa mwaka 2021/22 iliyoonyesha kwamba DAWASA wanatoa bili za makaridio badala ya kusoma mita za wateja hasa hasa kwa Wilaya za Kinondoni, Mlandizi na Kigamboni.

  • Kukatika kwa maji mara kwa mara bila taarifa. Tatizo jingine linalolamikiwa sana ni suala la upatikanaji wa maji usio kuwa wa uhakika au kutolewa kwa mgawo. Yapo maeneo maeneo maji upatikana usiku na alfajiri. Changamoto hii inaleta mateso makubwa hasa kwa Wanawake hasa hasa maeneo ya Mkuranga, Kisarawe na baadhi ya Wilaya za Dar es Salaam (Ubungo, Kigamboni na Kinondoni). Kuwepo kwa mgawo au kutokuwa na uhakika wa huduma za maji kunaongeza gharama mathalani wapo wananchi katika miji hii wananunua maji ndoo kubwa shilingi 1000 hadi 1500.

  • Kupata huduma maji yasiyo safi. Malalamiko mengine ni kuwa maji yanayotoka kwenye mabomba ni machafu mno na mengine yanatoa harufu kwa baadhi ya maeneo. Zipo taarifa za baadhi ya wananchi kupatwa na magonjwa ya ngozi kutokana na kile wanachoeleza kutumia maji hayo. Tatizo hili lipo hadi sasa kwa maeneo ya Kigamboni, Pugu, Kawe, Kisarawe, Baganoyo na Mkuranga.
Malalamiko mengine ni pamoja na ukataji maji bila taarifa, kuchelewa kurudisha maji, malalmiko kuhusu huduma za maji taka, kuchelewa kukarabati mita, gharama kubwa zisizotabirika za kuunganishwa na maji na kuchelewa kurekebisha Dira.

Ni wazi kuwa changamoto hizi zinaonyesha kwa kiasi gani watendaji na mamlaka imeshindwa kutekeleza kwa ufanisi majukumu iliyokabidhiwa. Aidha, kuna uzembe wa kiuongozi katika kuisimamia DAWASA, jambo linalopelekea inaenda kinyume kabisa na Mkataba wa huduma kwa wateja unaotoa Mwongozo juu wa muda wa kuunganisha wateja, suala la ukarabati wa Miundombinu, kushughulikia malalamiko ya Ankara na bili kwa muda usiozidi siku 5 na gharama za kuunganisha wateja.

Sisi, ACT Wazalendo kutokana na kuendelea kuwepo kwa changamoto hizi katika Mkoa wa Dar es Salaam na maeneo yanayoizunguka tunaitaka Serikali kuchukua hatua zifuatazo;

  • Tunamtaka Waziri wa Maji Ndg. Juma Aweso kuwachukulia hatua watendaji wote wanaohusika na uzembe huu kama alivyofanya kwa Mamlaka ya Maji ya Mwanza (MWAUWASA).

  • Tunatoa wito kwa Serikali kupitia wizara ifanyie kazi kwa haraka ununuzi wa vifaa vya kutosha vya kuunganisha maji kwa kuziwesha Mamlaka za maji kuagiza kwa mujibu wa kanuni za manunuzi.

  • Vilevile, ili kudhibiti Usalama na usafi wa maji tunaitaka Serikali kufanya ukarabati wa miundombinu ya kusafirisha maji (mabomba) na kuweka vifaa vya kuzuia kutu.

  • Tunaitaka DAWASA kuangalia taarifa zake na kulipa fidia wateja wote kwa kushindwa kutekeleza malengo ndani ya muda wa Makubaliano ya Shilingi 5,000 kwa kila siku kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa wateja kwa kuendelea kuchelewa;

  • Serikali kupitia DAWASA ifute bili ya Maji ya kipindi chote cha mwezi huu agosti 2023 kwa kutoa maji yasiyosafi kwa wakazi wa Wilaya ya Kigamboni, Mbezi na Kisarawe itumie muda huu kutibu maji kwa viwango stahiki na kusambaza maji safi na salama
Mwisho, Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA) kusimamia kikamilifu na kuwajibika kwa matatizo haya, Maji ni huduma msingi sana kwa uhai na ustawi wa jamii hivyo, huduma hii inapaswa kutazamwa na kutolewa kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia uhutaji na sheria, ACT Wazendo tutachukua hatua zaidi endapo tutajiridhisha hakuna hatua stahiki zinazochukuliwa katika kukabiliana na adha tuliyoeleza hapo juu.

Imetolewa na;

Mwanaisha Zuberi Mndeme

Twitter(X); @Mwanaishamndeme

Waziri kivuli wa Maji

ACT Wazalendo.

25 Agosti, 2023.
 
Kati ya vyama ambavyo sielewi ILANI yao au sera ni hiki, ni kama mzee kikwete alivyokuwa anamzungumzia ndege mbaiwai alikuwa anakiongelea hiki chama!

Mara wahamie kuwa wanahakati wa raia wa Ethiopia, mara dawasco! Sijawah kuwasikia wakitoa ushauri kwa serikali kwenye sakata la bandari, Chama cha mchongo hichi
 
Wacheni uhuni tuko busy na Bandari . Hayo maji tangu enzi za mwalimu ni shida tushazoea kunywa maji ya mtoni.

Jikiteni kwenye hoja pana zenye maslahi mapana kwa Taifa BANDARI BANDARI na umoja wa kitaifa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom