DOKEZO DAWASA Kibaha Wamesitisha Huduma ya Kuunganisha Maji kwa Wateja wapya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Satu

JF-Expert Member
Nov 22, 2013
259
472
Habari za leo ndugu zangu?

Kwa miezi kadhaa sasa, wananchi wengi wa Kibaha wanaoomba kuunganishiwa maji kwa mara ya kwanza (wateja wapya) hawajaweza kupata huduma hiyo.

DAWASA Kibaha wanapokea maombi mapya, lakini hawatoi bili za malipo (control namba), wanadai wameishiwa vifaa.

Wadau tusaidieni kupaza sauti, kuna watu wameomba maji toka mwezi wa pili hadi leo bado hawajahudumiwa.

Foleni ya kusubiri huduma imekuwa ndefu mno, hali inayotengeneza mazingira ya rushwa.

===
Soma Dawasa Kibaha yarejesha huduma ya kuunganisha maji kwa wateja wapya
 
Afafhali ya hiyo Kigamboni mtaa wa muungano walilitoa kabisa bomba lililochimbiwa na kudai eti hakuna wateja wakati maombi walishapelekewa.
 
Nilikwenda ofisini KIBAHA MAILI MOJA wakasema hawapokei maombi mapya,,

Nikauliza sababu za kufanya hivyo,
Wakasema kwamba Kuna uhaba wa maji na hawataki kupokea maombi mapya wakati maji hatoki..

Sasa kuwekewa huduma za maji na maji kutokutoka kwa wakati kunahusiana vipi?

INCHI NGUMU SANA HII
 
Hiyo hali ilinikuta mwaka 2020 walisema hivyo. Jiongeze utapata control number ndani ya dakika tano. Kuna wengine wanaunganishiwa maji ndani ya mwezi mmoja wakati wewe una subiri kwa mwezi hata kumi
 
Hata Mimi nimeambiwa hivyo hivyo kuwa vifaaa hamna na control number hawajatoa ,bongo ubabaishaji mwingi sanaa DAWASA badala ya kuunga watu wauze maji wao business as usual Kwa vile mshahara unaingia

Bandari wapewe tu DP world plus DAWASA,TANESCO ikiiwezekana hata jeshi la polisi wapewe wachina
 
Jamaa ni wahuni sana.Wanadai.vifaa hakuna hizo hela anazolipa mteja si ndio za kununulia vifaa sasa wanapeleka wapi
 
Tatizo la uhada wa vifaa litatatuliwa lini? Ni zaidi ya miaka miwili sasa wimbo ni ule ule uhaba wa vifaa... mara tusubiri mwaka wa bajeti... miaka ya bajeti imeshapita mingapi sasa?
 
Kwanini miradi mingi ya serikali huwa inaanza kwa kwa bashasha na kwa kadri muda unavyoendelea, ndivyo inavyozidi kudorora? Suala la kuunganishiwa maji limekuwa gumzo katika maeneo mengi. Wacha nitoe uzoefu wangu.

Mimi ni mkazi wa Mivumoni, Kata ya Wazo, Wilaya ya Kinindoni, nilijaza form ya kuunganishiwa maji, lakini ilibidi nifuatilie ndipo ilipopatikana!

Baada ya kupatikana kwa hiyo form nililipia kiasi kilichotakiwa. Nililipa tarehe 7. 7. 2023, nikaambiwa nisubiri siku 14 za kazi.

Nikasubiri kwa hamu kwelikweli. Baada ya siku 17 kupita nikaenda ofisini kuulizia (maana ndio utamaduni wetu, kufuatilia), nilipofuatilia niliambiwa Mita zimeisha. What? Mita zimeisha? Ina maana wakati mradi unaanza hamkuwa na vifaa vya kutosha?

Jibu: Mita zimeisha.
Swali: DAWASA mnafeli wapi?

Ina maana huu mradi haukuwa na bajeti? Mpaka hivi ninavyoandika, sijapata maji. Hiki kilio nikipeleke kwa nani?

0769080629
 
Duh ngoja nitulize kipago maana nilikuwa na plan za kwenda huko dawasco
 
Mita zimeisha na pesa mmelipia?
 
Back
Top Bottom