Waziri Aweso: DAWASA wakopesheni wanaotaka kuunganishiwa maji watalipa kidogokidogo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi Mkandarasi Mradi wa Maji Bangulo, Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso amemwambia Mkandarasi kuwa Wananchi wa Kusini mwa Dar wameteseka kwa muda mrefu, hivyo hana kisingizio kutekeleza mradi huo kwa kuwa fedha zipo.

Waziri Aweso amewaambia DAWASA kuzingatia vijana waliopo karibu na maeneo ya Mradi ili ikiwezekana wale wenye vigezo wapewe ajira, ambapo pia amewataka watakaopata nafasi wawe waaminifu na kuachana na tabia ya udokozi.

“Kuna eneo ambalo naomba DAWASA mliwekee nguvu, Mwananchi anayeomba kuunganishiwe maji isizidi wiki mbili aunganishiwe maji.

“Hata ikitokea kuna Mwananchi ambaye anataka kuunganishiwa maji na mnajua hana hela mkopesheni mumuunganishiee, maji hayana mbadala.

“Wapo watu ambao wanaweza kuhitaji maji na wakalipa, lakini ikitokea mtu hana uwezo mumkopeshe na mtamlipa kidogokidogo kupitia kwenye bili yake.”

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi kwa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Bangulo katika maeneo ya Pugu Mnadani Jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Kiula Makalla KinguAmesema eneo hilo lipo katika muinuko wa juu kuliko maeneo mengine yote ya Mji.

Eneo hilo litaweza kusambaza maji katika sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam hasa upande wa Kusini mwa Mji.

Amesema “Jimbo la Kibamba ni sehemu ambayo kuna miinuko mingi, DAWASA tumejipanga kufikisha maji maeneo yote, tumetenga Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya eneo hilo ambapo linatarajiwa kupeleka maji kwa Wananchi zaidi ya 12,200.

“Jimbo la Ukonga tumetenga Shilingi Milioni 722 ambapo kuna miradi midogomidogo tunayoendelea nayo, tunatarajiwa kuhudumia Wananchi 19,444 katika maeneo ya Majohe, Viwengwe, Kichangani, Bombambili, Rada, Pugu Station, Kivule, Mji Mpya hadi Dampo.

“Jimbo la Segerea, DAWASA imepanga kutumia Shilingi Milioni 334 kwa Mwaka huu wa Fedha, kuna miradi midogomidogo inayoendelea maeneo kadhaa, fedha hizo tunatarajia zitahudumia Kaya 1,050.”

Mradi wa maji Bangulo
Akizungumza zaidi Mradi wa Tenki la Bangulo amesema utatekelezwa katika Awamu Kubwa 2 kila moja ikihusisha miezi 12 kuanzia siku ya kusaini mkataba

Amesema mradi huu unaotekelezwa na DAWASA na ufadhili wa Benki ya Dunia kwa gharama ya Tsh Bilioni 42, utahudumia Wananchi Takribani 450,000 katika Majimbo ya Kibamba, Segerea, Ukonga, Ubungo, Temeke na Ilala.

Mradi wa maji Bangulo utanufaisha wakazi wa mitaa ya Ulongoni B, Mwembe Supu, kwa Pepepeteka, Bangulo Mwembe Kiboko, Bangulo shule ya Msingi na Kifuru kwa Asha Madenge.

Wakazi wa Kata za Gongo la mboto, Mwanagati, Pugu station na Kinyerezi na maeneo jirani ya Bangulo katika kata ya Pugu Wilayani Ilala wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji kupitia umradi wa maji Bangulo

Mkandarasi wa mradi huu anaitwa M/S SINOHYDRO kutoka China na Utasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S SCET TUNISE ya Tunisia akishirikiana na SMARCON ya Tanzania kwa Ushirikiano wa DAWASA.

Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji Maji Kusini mwa Dar unahusisha vitu Vifuatavyo.

*Ulazaji bomba la Chuma la kusafirisha maji kutoka Kibamba hadi Tenki la Bangulo (km 11).

*Ulazaji wa bomba kuu za usambaxaji maji za chuma km 17.39 kutoka Tenki la Bangulo mpaka bomba za Usambazaji.

*Ulazaji wa bomba kuu za usambazaji maji za plastic umbali wa km 91.297

*Ujenzi wa Tenki la kuhifadhi na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita 9,000,000 litakalojengwa Bangulo.

*Ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Kibamba ambapo unategemewa kuzalisha mita za ujazo 23,333 kwa siku.

Chanzo cha maji katika mradi huu ni mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu.

Mradi wa maji Bangulo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na DAWASA inayolenga kufikisha asilimia 95 ya upatikanaji wa huduma ifikapo 2025.
 
Biashara haina mkopo, kwa mtindo huo muda sio mrefu watashindwa kujiendesha. Sawa nafahamu kuna watakaosema hii ni huduma sio kweli hii ni biashara ambayo inatoa huduma ya maji.

Baada ya muda mamlaka ikishindwa kujiendesha sababu utasikia ni fedha ya uendeshaji, kisa kukopesha jiji zima linakosa maji.
 
Muelewe alichosema Waziri.
Amesema wapewe huduma watalipa kidogo kidogo kupitia bill zao.
Waziri pia amesema maji hayana mbadala.
Maana yake kila mmoja ayapate.
Sidhani kama kuna tatizo.
 
Yah hii inawezekana. Unakopa. Then unalipa ndani ya labda tuseme 2 years (miezi 24).

Kwahiyo kama gharama za kuunganisha zilikua 300k inamaana ukiigawa ktk miezi 24 ni kama 12,500 kila mwezi.

Kwahiyo kwenye control number unakua unaongezea iyo gharama.

Sema ina changamoto ila ni afadhali.

Ila mi mawazo yangu:
Watu wa Dar kupata maji tatizo sio gharama za kuunganisha tatizo no DAWASA wazembe sana yaani unaweza apply leo ukaja fungiwa after miezi 10.
 
Akizungumza katika hafla ya kumkabidhi Mkandarasi Mradi wa Maji Bangulo, Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso amemwambia Mkandarasi kuwa Wananchi wa Kusini mwa Dar wameteseka kwa muda mrefu, hivyo hana kisingizio kutekeleza mradi huo kwa kuwa fedha zipo.

Waziri Aweso amewaambia DAWASA kuzingatia vijana waliopo karibu na maeneo ya Mradi ili ikiwezekana wale wenye vigezo wapewe ajira, ambapo pia amewataka watakaopata nafasi wawe waaminifu na kuachana na tabia ya udokozi.

“Kuna eneo ambalo naomba DAWASA mliwekee nguvu, Mwananchi anayeomba kuunganishiwe maji isizidi wiki mbili aunganishiwe maji.

“Hata ikitokea kuna Mwananchi ambaye anataka kuunganishiwa maji na mnajua hana hela mkopesheni mumuunganishiee, maji hayana mbadala.

“Wapo watu ambao wanaweza kuhitaji maji na wakalipa, lakini ikitokea mtu hana uwezo mumkopeshe na mtamlipa kidogokidogo kupitia kwenye bili yake.”

Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi kwa Mkandarasi wa Mradi wa Maji Bangulo katika maeneo ya Pugu Mnadani Jijini Dar es Salaam, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Kiula Makalla KinguAmesema eneo hilo lipo katika muinuko wa juu kuliko maeneo mengine yote ya Mji.

Eneo hilo litaweza kusambaza maji katika sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam hasa upande wa Kusini mwa Mji.

Amesema “Jimbo la Kibamba ni sehemu ambayo kuna miinuko mingi, DAWASA tumejipanga kufikisha maji maeneo yote, tumetenga Shilingi Milioni 500 kwa ajili ya eneo hilo ambapo linatarajiwa kupeleka maji kwa Wananchi zaidi ya 12,200.

“Jimbo la Ukonga tumetenga Shilingi Milioni 722 ambapo kuna miradi midogomidogo tunayoendelea nayo, tunatarajiwa kuhudumia Wananchi 19,444 katika maeneo ya Majohe, Viwengwe, Kichangani, Bombambili, Rada, Pugu Station, Kivule, Mji Mpya hadi Dampo.

“Jimbo la Segerea, DAWASA imepanga kutumia Shilingi Milioni 334 kwa Mwaka huu wa Fedha, kuna miradi midogomidogo inayoendelea maeneo kadhaa, fedha hizo tunatarajia zitahudumia Kaya 1,050.”

Mradi wa maji Bangulo
Akizungumza zaidi Mradi wa Tenki la Bangulo amesema utatekelezwa katika Awamu Kubwa 2 kila moja ikihusisha miezi 12 kuanzia siku ya kusaini mkataba

Amesema mradi huu unaotekelezwa na DAWASA na ufadhili wa Benki ya Dunia kwa gharama ya Tsh Bilioni 42, utahudumia Wananchi Takribani 450,000 katika Majimbo ya Kibamba, Segerea, Ukonga, Ubungo, Temeke na Ilala.

Mradi wa maji Bangulo utanufaisha wakazi wa mitaa ya Ulongoni B, Mwembe Supu, kwa Pepepeteka, Bangulo Mwembe Kiboko, Bangulo shule ya Msingi na Kifuru kwa Asha Madenge.

Wakazi wa Kata za Gongo la mboto, Mwanagati, Pugu station na Kinyerezi na maeneo jirani ya Bangulo katika kata ya Pugu Wilayani Ilala wanatarajiwa kunufaika na huduma ya maji kupitia umradi wa maji Bangulo

Mkandarasi wa mradi huu anaitwa M/S SINOHYDRO kutoka China na Utasimamiwa na Mhandisi Mshauri M/S SCET TUNISE ya Tunisia akishirikiana na SMARCON ya Tanzania kwa Ushirikiano wa DAWASA.

Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji Maji Kusini mwa Dar unahusisha vitu Vifuatavyo.

*Ulazaji bomba la Chuma la kusafirisha maji kutoka Kibamba hadi Tenki la Bangulo (km 11).

*Ulazaji wa bomba kuu za usambaxaji maji za chuma km 17.39 kutoka Tenki la Bangulo mpaka bomba za Usambazaji.

*Ulazaji wa bomba kuu za usambazaji maji za plastic umbali wa km 91.297

*Ujenzi wa Tenki la kuhifadhi na kusambaza maji lenye ukubwa wa Lita 9,000,000 litakalojengwa Bangulo.

*Ujenzi wa kituo cha kusukuma maji Kibamba ambapo unategemewa kuzalisha mita za ujazo 23,333 kwa siku.

Chanzo cha maji katika mradi huu ni mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu.

Mradi wa maji Bangulo ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa na DAWASA inayolenga kufikisha asilimia 95 ya upatikanaji wa huduma ifikapo 2025.
maji yenyewe hayatoki
 
Back
Top Bottom