maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,144
- 15,144
Wanabodi (Kwa sauti ya Paskali Mayalla),
Nasikitika sana kuleta kero yangu kwa hawa DAWASA ambao wameamua kutufanyia uhuni sisi wateja wao wapya.
Binafsi nililipia kuunganishiwa maji tangu October 2023 ila tukaambiwa kuna upungufu wa vifaa tusubiri. Tukasubiri hadi mwaka ukaisha tunaambiwa bado vifaa havijafika.
January ikapita, February ikapita, na sasa ni March bado sijafungiwa maji (Tegeta A). Baada ya kuanza kufuatilia muungwana mmoja wa DAWASA akashangaa how comes muda wote sijafungiwa maji muda wote huo wakati vifaa vilishafika na kuna watu wamelipia mwezi February wamefungiwa.
Baadaye ikabidi afunguke kuwa wanafungiwa wateja wanaojiongeza kwa kutoa rushwa, na akanitajia baadhi ya waliolipia mwaka huu wamefungiwa tena ndani ya siku mbili tu wakati wengine tumesubirishwa miezi mitano.
Huu si uungwana kabisa kumbe mmeamua kutengeneza tatizo makusudi ili kutengeneza mianya ya rushwa.
Na mkibisha nitaweka ushahidi wote hapa, acheni ujinga fanyeni kazi kwa weredi kama wenzenu wa TANESCO hawakawii kukuletea huduma ya umeme ukilipia, njooni mtufungie maji wateja tuliotangulia kulipia. Miezi mitano mnatusubirisha na kumbe mna agenda yenu? Naomba waziri husika afuatilie hii hujuma.
Na ninaomba TAKUKURU mchunguze hata kwenye system mtagundua kuna wateja tuliolipia tangu October na November hatujafungiwa maji wakati kuna waliolipa mwaka huu na wamefungiwa, DAWASA wawaambie ni kwa nini.