Dawasa Kibaha yarejesha huduma ya kuunganisha maji kwa wateja wapya

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Meneja wa DAWASA Kibaha, Alfa Ambokile amesema “Kila ofisi au taasisi inaweza kupitia kipindi fulani kigumu lakini huduma ya kuunganisha maji tayari imerejeshwa na hata leo hii (Agosti 28, 2023) tumehudumia wateja wapya wa kuunganishiwa maji.

Tulisitisha kipindi cha ukame Mwaka jana (2022), wapo waliochukua control number wakakaa nazo nyumbani muda mrefu bila kulipia, wengine tunawapigia simu hawaji, wengine walikosea namba za simu.

Pia Machi 2023 tulisimamisha huduma lakini kuanzia wateja walioomba Aprili 2023 tunawahudumia.

Huduma imenza kwa walioanza kutangulia kuomba awali, kama kuna mtu aliomba huduma ya kuunganishiwa maji zamani na hajapata huduma aje atapata huduma.

Kila siku watu wanawasilisha maombi ya kuunganishiwa maji, vifaa vipo.


Pia soma DAWASA Kibaha Wamesitisha Huduma ya Kuunganisha Maji kwa Wateja wapya
 
Back
Top Bottom