Wazee wa CHADEMA wakutana na Dr. Slaa leo

Wazee wa CHADEMA wakutana na Dr. Slaa leo

Chadema si mali ya mtu,ni vyema dr.slaa afahamu kuwa chadema tunamhitaji na kuheshimu matakwa ya wengi ni hulka nzuri kwa kiongozi,karibu kazi kiongozi wetu
Mkuu hayo maneno tafadhali sana labda waambie Bavicha.

Chadema ni mali ya Mbowe na Mtei.
 
Hivi uwongo mbona umezidi? Wanakwenda kuongea nae nini? Muda mfupi mbowe kasema wameshaongea nae kawaruhsuu waendelee na vikao, mbona mnatuchanganya tu

Haha ndio nashangaa,naona kuna u Zombie ndani yake.
Mie mwenyewe ndio naangalia taarifa ya habari kwamba Dr.Slaa alitofautiana na Kamati kuu.Na wakaulizwa Wajumbe wakasema kwamba Apumzike.
Na kama uliangalia Clouds Tv,ni kwamba kuna wajumbe walienda kwake walinzi wakawageuzisha njia kama watu wengine na kuondoka zao.
 
Wacha Dr apumzike kwanza. Ikiwezekana akagombee ubunge. Baada ya uchaguzi mkuu tutampa uwaziri mkuu
 
Hivi ile Taasisi iliyopewa na UKAWA Tender ya kufanya utafiti ilishauri nini katika report yao ya Utafiti!!? Isije ikawa hii ni sehemu ya mbinu waliyoshauri itumike kuifuta CCM katika maongezi na vyombo vya habari!! Maana hali ilivyo sasa watu wamesahau kabisa kuwa CCM iliteka vyombo vya habari pale Dodoma, sasa hivi pamoja na mchakato unaoendele wa kura za maoni ndani ya CCM bado vyombo vya habari vimemulika habari toka ndani ya CHADEMA/UKAWA na Dr. Slaa.

Baada tu ya Magufuli kuteuliwa tuliona namna walivyoamua kuendelea kuwa hewani kwa kuteka vyombo vya habari kwa madai ya kwamba wanamtambulisha mgombea wao kwa wananchi, lakini tangu CHADEMA/UKAWA nao walipokamata lami jamaa wamepotea jumla. Nchi kwa sasa hatumsikii rais wala waziri mkuu wala nani, kiasi cha kuanza kupata hisia kuwa huenda hata rais na mawaziri wake nao wameamua kujitoa Chamani kimya kimya. Nafikiria mambo mengi ambayo yananiongoza kufikiri kuwa huu ni MKAKATI na kuishia kutamani iwe kweli ni MKAKATI na kama ni kweli basi MKAKATI huu itabidi uingie katika records za kidunia.
Katika hili sina dots za ku connect , kwakweli nimeachwa gizani na mbaya zaidi ni pale suala hili linapoonekana kukosa ushawishi wa marafiki, yaani hakuna rafiki wa karibu na Dr. Slaa au mkewe, anaye ripotiwa kuwa karibu na Dr. Slaa au familia hiyo anayeelekea kufahamu chochote kile anachowaza Dr. wetu. Imekuwa ni siri mbele ya dunia sawa kabisa na ile ya ndege ya Malaysia ambayo imekosa kabisa wataalam wa kuweza kuelezea japo fununu kuhusiana na where abouts zake. Hata serikali haikuwahi kuhifadhi siri kwa kiwango hiki, ukiwaza sana inasisimua sana na wakati fulani 'inaogopesha', sihitaji kuendelea kuotea au kukisia, nasubiri Tarehe nane au siku chache kabla ili sisikie taarifa rasmi, sihitaji tena kupapasa.
 
We unajua ni lini na wapi ilipigwa? Pili hawa wazee wako wapi sasa na umewasiliana nao? Hebu weka facts sio ya kweli.
Haya kamanda ngoja nikufurahishe ni kweli ni kweli hao wazee wa Chadema wamepiga picha nyumbani kwa Dr.Slaa, aliowapiga picha hiyo ni mzee Mtei, umefurahi sasa mgogoro umeisha.
 
Mazungumzo yameisha salama mungu mkubwa na dr slaa atarejea kazini muda si mrefu kuendelea na majukumu yake ya kichama.

Nitawawekea picha baadae kidogo.

Wito kwa wana chadema tujifunze uvumilivu wa kisiasa tuache siasa za kufata mkumbo na tuwe na heshima kwa wazee wa chama.
attachment.php

Hogera wazee kwani kumkosa Dr Slaa Ukawa ni pigo kubwa sana na tuombe Mungu Habari hizi ziwe za kweli
 
Namheshimu sana Dr Slaa lakini kwa kitendo cha usaliti bora aondoke kwa sasa sisi wananchi ni kuindoa ccm mtu anakuja na hoja za ajabu mzee wangu slaa umejiangusha sana. Mimi na familia yangu tumeishaamua kupigia kura mabadiliko na kura ni kwa Edo basi
 
Ccm kuchafu chadema na UKAWA ni sehem ya toba ya kweli
 
Binafsi nimependa sana msimamo wa Dr. Slaa. Iwapo hakutakuwa na watu wa kusimamia msimamo basi nchi hii itaendelea kuwa na viongozi wenye mawaa kwenye jamii na hawatojali kwani watajua hata iweje kutakuwa na viongozi wa aina ya kina Mbowe ambao hawana misimamo. Madhara ya hiki alichokifanya Mbowe tutaona madhara yake tukiwa tumeshachelewa. Huyo EL haaminiki na funzo alilotupa Shibuda naona kama tumeamua kurudia kosa. Yangu macho japo hata kama sijaridhika na kile kinachoendelea cdm kura yangu ni kwa ukawa tu.
 
Binafsi nimependa sana msimamo wa Dr. Slaa. Iwapo hakutakuwa na watu wa kusimamia msimamo basi nchi hii itaendelea kuwa na viongozi wenye mawaa kwenye jamii na hawatojali kwani watajua hata iweje kutakuwa na viongozi wa aina ya kina Mbowe ambao hawana misimamo. Madhara ya hiki alichokifanya Mbowe tutaona madhara yake tukiwa tumeshachelewa. Huyo EL haaminiki na funzo alilotupa Shibuda naona kama tumeamua kurudia kosa. Yangu macho japo hata kama sijaridhika na kile kinachoendelea cdm kura yangu ni kwa ukawa tu.


naungana na ww. dr nampenda lkn vyovyote vile kura yangu inabaki ukawa.
 
Apumzishwe t fomu ya urais hachukui akija wakuchukua anasusa
 
Mazungumzo yameisha salama mungu mkubwa na dr slaa atarejea kazini muda si mrefu kuendelea na majukumu yake ya kichama.

Nitawawekea picha baadae kidogo.

Wito kwa wana chadema tujifunze uvumilivu wa kisiasa tuache siasa za kufata mkumbo na tuwe na heshima kwa wazee wa chama.
attachment.php
Je ni baada ya hapo ndiyo Kamati Kuu/Baraza Kuu (?) Wakaridhia kumpumzisha? Source ITV
 
Mkuu PISTO LERO naomba kukuhakikishia kuwa hakuna mwana cdm wa kweli,hakuna aliye kuwa against na Dr slaa,hao wote unao waona wanatukana au kushinikiza mambo ya kijinga ni ingizo la Lumumba kutaka kuchafua hali ya hewa ndani ya cdm kwa makusudi hata hivyo makamanda tupo macho na ikibidi kukesha kuhakikisha tuna zuia upotoshaji huo kwa kueleza ukweli kwa watanzania wapenda mageuzi ya kweli

Kula like umenena vyema mkuu.
 
Ntaamini nitapomwona kwenye kikao cha kamati kuu.
 
Back
Top Bottom