KERO Wauza Chipsi wa Stendi ya Mabasi Babati zingatieni usafi wa huduma yenu ya chakula. Mnaweka hatarini afya za wateja wenu (abiria)

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nilifika Babati kusubiri basi kwa ajili ya kuelekea mkoa fulani, wakati nipo pale nilihisi njaa, niliamua kutafuta sehemu mojawapo wanaopika pale hususan wanaokaanga chipsi ili nile.

Nilipokelewa vizuri na kuoneshwa sehemu ya kukaa, niliagiza chipsi, nikaletewa lakini zilikuwa za baridi sana. Nikamuambia aliyeniletea kuwa siwezi kula zikiwa zabaridi ilibidi achukue na kuniambia nisubiri ambazo zipo jikoni.

WhatsApp Image 2025-06-14 at 13.19.04_98f49d7d.jpg

WhatsApp Image 2025-06-14 at 13.19.04_a6f6735f.jpg

Wakati nasubiri nikiwa kwenye meza Wanawake wawili walikuja kwenye banda lile la chipsi miongoni mwao alikuwa ndiye mmiliki, Wanawake hao walitoka kuuza Chipsi kwa abiria walio kuwa kwenye mabasi hapo stendi.

Kilichonishangaza ni kwamba hawakuwa wanazingatia usafi wakati wa uuzaji wao na hata mazingira yao.

Katika meza niliyo kaa kulikuwa na bakuli la chumvi ambalo limechanganyika na stick, kila mmoja alipokuja kuchukua chipsi kwa ajili ya kupelekea abiria walikuwa wakichukua chumvi na zile stick kwa mikono yao na hakukuwa na kitu maalum cha kuchukulia chumvi.

WhatsApp Image 2025-06-14 at 13.19.03_65033d2a.jpg
 
usipende sana kula njiani ndugu

njaa ya siku moja haiondoi uhai wako,nunu maji kama kuna ulazima inatosha
 
Usafi wanaojua watanzania ni wa kuoga, kufua, kupiga deki na kufagia uwanja kuzunguka nyumba zao ila hawana kinyaa kabisa.
 
Kweli mkuu Watanzania wachafu sana tena awa wafanyabiashara wa vyakula, Utakuta Muuza chapati na Mandazi na vitumbua anashika pesa kwa mikono na hapo ana shika vyakula na mikono.
 
Tatizo wateja na ni wachafu wanaona sawa na wala hawahoji. Watanzania ni wachafu sana.
 
Nilifika Babati kusubiri basi kwa ajili ya kuelekea mkoa fulani, wakati nipo pale nilihisi njaa, niliamua kutafuta sehemu mojawapo wanaopika pale hususan wanaokaanga chipsi ili nile.

Nilipokelewa vizuri na kuoneshwa sehemu ya kukaa, niliagiza chipsi, nikaletewa lakini zilikuwa za baridi sana. Nikamuambia aliyeniletea kuwa siwezi kula zikiwa zabaridi ilibidi achukue na kuniambia nisubiri ambazo zipo jikoni.

Wakati nasubiri nikiwa kwenye meza Wanawake wawili walikuja kwenye banda lile la chipsi miongoni mwao alikuwa ndiye mmiliki, Wanawake hao walitoka kuuza Chipsi kwa abiria walio kuwa kwenye mabasi hapo stendi.

Kilichonishangaza ni kwamba hawakuwa wanazingatia usafi wakati wa uuzaji wao na hata mazingira yao.

Katika meza niliyo kaa kulikuwa na bakuli la chumvi ambalo limechanganyika na stick, kila mmoja alipokuja kuchukua chipsi kwa ajili ya kupelekea abiria walikuwa wakichukua chumvi na zile stick kwa mikono yao na hakukuwa na kitu maalum cha kuchukulia chumvi.

unakulaje chips za stend na ww msukuma nini.... ndo nyie huwa mnatusumbua njian kuharisha mwazo mwsho
 
Back
Top Bottom