Watu wanaamini kuna Mungu na shetani kwa sababu kuamini ni rahisi kuliko kufikiri

whiteskunk

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
3,758
8,900
Kuna tofauti kubwa kati ya uwezo wa kufikiri na uwezo wa kukariri.

Ubongo usiokuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri unapenda majibu mepesi.

Mfano unaweza kumwambia mtu mwenye akili ya kutosha kuwa, kuiba sio vizuri kwa sababu kuna matokeo mabaya kama kufungwa, kupigwa n.k na akakuelewa,

Ila mjinga ni lazima umuogopeshe kuwa kuiba ni dhambi, hivyo hataiba kwa kuhofia anatenda dhambi.

Hivyo ni rahisi sana kumuaminisha mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri kuwa kuna nguvu isiyoonekana na akaamini.

Sababu nyinginezo ni kama
  • Kurithishwa utamaduni, pale mtoto anapozaliwa analazimishwa aamini imani ya wazazi kwa kubatizwa n.k
  • Woga, watu wengi wanaogopa kutokana na vitisho mbalimbali mfano kutengwa kwenye jamii zao
  • Kifo, wengi hawakubaliani na ukweli kwamba ni lazima kiumbe hai afe, hivyo wanatamani wapate maisha mengine baada ya kifo.
  • Majibu ya kisayansi hayafariji kama ya kidini n.k.
 
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Faith is the practice of training the mind to ignore facts, evidences and logic.

Watu hawana uhakika wala uthibitisho wa uwepo wa Mungu na shetani zaidi ya mawazo yao ya kufikirika tu na hadithi za kusadikika, kusimuliwa na kurithishwa.

Watu wame aminishwa kwamba kuna invisible creature beyond the sky anaitwa Mungu.

Hadithi hizi ni sawa na Hekaya za Abunuwasi na riwaya za Alfu Lela ulela.
 
Mungu ana akili sana.

Ulimwengu wa Roho hauwezi kuuingia kwa kutumia mbinu za kimwili. Imani (ambayo huonekana ujinga kwa waliojaa 'hekima, uwezo wa kufikiri) ndio kianzio. Ukijishusha, ukasema 'Naamini', ndio unaanza kuona hadi maono wazi wazi.

Rejea andiko hili:

”bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;“
‭‭1 Kor‬ ‭1‬:‭27‬ ‭SUV‬‬
 
Pia kuna wale wapuuzi wanaosema kuwa dini zimeleta maadili mema, jambao ambalo si kweli, mtu mwenye akili timamu haitaji dini wala imani yoyote kufanya mambo mema bali kuheshimu haki za wengine na sheria za kiutu.

Hatumuhitaji Mungu ili tufanye mema, hatutakiwi kufanya mema kwa kumuogopa Mungu bali kwa kujari utu wa wenzetu
 
Mwanadamu vitu aviwazavyo akishakuwa na uhakika wa kula...
Vipi watoto wadogo wanaokufa kwa baa la njaa maeneo mbalimbali duniani lakini Mungu huyo hajawahi kuwapa msaada wowote ule?

Watoto wadogo tu hawana uhakika wa kula na huyo Mungu hana msaada wowote kwao, wengi wamekufa, wanakufa na wanaendelea kufa.

Fuatilia vifo vya watoto wadogo wanaokufa kwa njaa nchi za Ethiopia, Somalia, Afghanistan, Kaskazini kwa kenya n.k

Sasa kama Mungu huyo Kashindwa tu kuwapa uhakika wa kula watoto wadogo kama hawa, Sembuse mimi mtu mzima?

Mungu huyo hana msaada wowote ule kwenye uhakika wa kula kwa wanadamu.

Mungu huyo hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Pia kuna wale wapuuzi wanaosema kuwa dini zimeleta maadili mema, jambao ambalo si kweli, mtu mwenye akili timamu haitaji dini wala imani yoyote kufanya mambo mema bali kuheshimu haki za wengine na sheria za kiutu.

Hatumuhitaji Mungu ili tufanye mema, hatutakiwi kufanya mema kwa kumuogopa Mungu bali kwa kujari utu wa wenzetu
Kwahiyo mkuu hata hizi jela na adhabu mbalimbali katika nchi yetu ni kwa ajiri ya watu wasio na akili timamu?
 
Mungu ana akili sana.

Ulimwengu wa Roho hauwezi kuuingia kwa kutumia mbinu za kimwili. Imani (ambayo huonekana ujinga kwa waliojaa 'hekima, uwezo wa kufikiri) ndio kianzio. Ukijishusha, ukasema 'Naamini', ndio unaanza kuona hadi maono wazi wazi.
Mungu huyo kama alitaka aaminiwe na binadamu wote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mwamini na kumtii siku zote?

Mungu huyo akiaminiwa anapata faida gani?

Na asipo aminiwa anapata faida gani?

Kwa hiyo Mungu huyo aliumba binadamu waje wamwamini tu?

Kama Mungu huyo aliumba binadamu wote tuje tumwamini na wengine hatumwamini basi kazi yake ya uumbaji ina kasoro na dosari.

Maana Mungu huyo ameshindwa kufanya sisi Atheists tumwamini.

Na automatically Mungu huyo hawezi yote.
Rejea andiko hili:

”bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;“
‭‭1 Kor‬ ‭1‬:‭27‬ ‭SUV‬‬
 
Vipi watoto wadogo wanaokufa kwa baa la njaa maeneo mbalimbali duniani lakini Mungu huyo hajawahi kuwapa msaada wowote ule?

Watoto wadogo tu hawana uhakika wa kula na huyo Mungu hana msaada wowote kwao, wengi wamekufa, wanakufa na wanaendelea kufa.

Fuatilia vifo vya watoto wadogo wanaokufa kwa njaa nchi za Ethiopia, Somalia, Afghanistan, Kaskazini kwa kenya n.k

Sasa kama Mungu huyo Kashindwa tu kuwapa uhakika wa kula watoto wadogo kama hawa, Sembuse mimi mtu mzima?

Mungu huyo hana msaada wowote ule kwenye uhakika wa kula kwa wanadamu.

Mungu huyo hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Mipango ya Mungu ni bora kuliko fikra zako
 
Mkuu unapinga kuwepo kwa Mungu au unapinga mambo yenye kuhusishwa na Mungu? Sijaelewa.
 
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika.

Faith is the practice of training the mind to ignore facts, evidences and logic.

Watu hawana uhakika wala uthibitisho wa uwepo wa Mungu na shetani zaidi ya mawazo yao ya kufikirika tu na hadithi za kusadikika, kusimuliwa na kurithishwa.

Watu wame aminishwa kwamba kuna invisible creature beyond the sky anaitwa Mungu.

Hadithi hizi ni sawa na Hekaya za Abunuwasi na riwaya za Alfu Lela ulela.
Huwa naona kama kutokuamini Mungu kuna husishwa moja kwa moja na kuwa na akili sana, hivi kwa nini inakuwa hivyo japo kwenye maisha ya kawaida hakuna huo utofauti kuonyesha kuwa wasioamini Mungu ndio wenye akili kuliko wenye kuamini Mungu?
 
Back
Top Bottom