Mama na Baba kuishi Pamoja ni rahisi kuwasaidia na kuwahudumia kuliko Wakitengana.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,893
MAMA NA BABA KUISHI PAMOJA NI RAHISI KUWASAIDIA NA KUWAHUDUMIA KULIKO WAKITENGANA.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli

Fainali ya uzeeni naiona kwa wengi ikiwapiga Knockout Matata. Kuna kilio cha mbuzi Mee naliona kinakuja kwa waliowengi.
Nilisema, wewe kama kipato chako upo chini ya milioni tano kwa mwezi bado upo kundi la watu Maskini. Ni lazima kwenye uzee wako uhitaji usaidizi wa watoto wako.
Ukibisha waweza bisha. Lakini utashuhudia kwa macho yako kile nikisemacho miaka isiyozidi 40 ijayo.

Kuishi Mume na mke sio tuu inawarahisishia maisha ya utafutaji nyakati mkiwa na nguvu bali pia inawarahisishia watoto mtakaowazaa kuwasaidia na kuwahudumia.

Wazazi wanaoishi pamoja ni rahisi kuratibu shughuli ya Kuwasaidia na kuwahudumia tofauti na wazazi waliopeana talaka au kutengana.

Elewa, kama ilivyo ngumu na changamoto kulea mtoto mkiwa mmetengana ndivyo hivyohivyo itakavyokuwa ngumu kwa watoto kuwatunza na kuwasaidia mkiwa mmetengana.
Waliosema Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu walikuwa sahihi.

Fikiria kijana mwenye umri wa miaka 20 mpaka 40 unayejitafuta utawezaje kuwasaidia wazazi waliotengana kila mmoja na mahitaji yake ilhali wangekuwa pamoja mahitaji yao yangekuwa sawasawa tuu..

Fikiria mkeo wazazi wake wametengana na wewe Wazazi wako Wametengana. Huoni hapo mpo kwenye Balaa kubwa.

Baba akaoa mwingine (familia ingine)
Mama akaolewa na mwingine (Familia ingine)
Na mkeo naye Babaake akaoa mwingine (familia ingine) na Mamake akaolewa na mwingine ( familia ingine)
Jumla Familia NNE.
Jumlisha familia yenu inakuwa Familia tano. Kudadadeki!
Najua wenye akili ndogo hawawezi kuona hilo hao. Hawawezi kuona kuwa hilo ni tatizo.

Kiafrika Afrika kutohudumia wazazi ni Laana. Sasa unajikuta unahitajika kuhudumia familia tano. Dadeki! Na kama utashindwa automatically upo kwenye mkondo wa Laana.

Vijana, wakati huu ndio wakati sahihi wa kuweza kuona mbele.
Chagueni wenza ambao mtafika mwisho wa maisha pamoja. Chagueni wenza ambao watarahisisha maisha yenu na maisha ya watoto wenu huko mbeleni.

Hakuna kitu kibaya kwa mtoto kama kujiona anashindwa kusaidia wazazi. Anajilaumu na wakati mwingine hujiona hana thamani na sababu ya kuendelea kuishi kama anashindwa kutoa hata kidogo kwa wazazi wake. Alafu mbaya zaidi ninyi mmeamua kwa ubinafsi wenu kuparangana na kuparanganyika.

Kijana anafikisha umri wa kuoa au kuolewa inakuwa ni rahisi kwake kuratibu mambo ya ndoa. Sasa ninyi mmeparanganyika. Mtoto mnampa kazi ya kuanza kuzurura mara upande huu mara upande ule. Mara kwa mke upande huu mara upande ule.
Bado muanze kumtia shinikizo kwamba nani anastahili kuwa wakwanza kati ya Baba na Mama. Acheni upuuzi wenu.
Mngeishi pamoja mngerahisisha mambo.

Mtoto anataka ajenge nyumba aanze kufikiria aanze kumjengea nani. Alafu kipato chake ndio hicho cha kujikuna vipele. Wakati mngekuwa mnaishi pamoja ilikuwa ni ishu rahisi tuu.
Matokeo yake watoto wanakosa uchaguzi hata kujengwa hawajengi. Hawana kwao. Kwao wapi sasa kwa mama au kwa Baba waliotengana wanaoishi na wenza wengine.

Najua kuna Watu hawatanielewa, na sio kosa lao kwa sababu Watu wengi huishi kama wanaota ndoto. Ilhali mimi naandika mambo kwa uhalisia wake.

Watoto hawawezi kuwa na umoja kama Baba na Mama hamkuwa na umoja. never Ever! Watoto hawawezi kuwa na upendo na kupendana kama ninyi wazazi hamkuonyesha huo upendo ninyi kwa ninyi. Haya maadili kumomonyoka chanzo kikuu ni wazazi.

Sisi kama Wazazi tunaowajibu wa kuhakikisha tunarahisisha maisha ya watoto wetu. Na njia ya kwanza ya kurahisisha maisha yao ni sisi kuwa pamoja.

Hata watoto kugombea Mali na kuua kisa urithi chanzo kikuu ni Wazazi kushindwa kuwa pamoja.
Familia zote zinazogombea Mali na kuuana chanzo kikuu ni utengano baina ya Mume na Mke tangu wakiwa Hai.
Watu wanaishi pamoja lakini wametengana. Alafu kuna waliotengana kabisa yaani hawaishi pamoja. Ni vita na machafuko.

Wewe kama kweli ni Baba au Mama Unaowajibu wa kulinda familia yako kwa kuwa pamoja. ubaba au Umama wako utaonekana kupitia familia na sio Kuzaa.

Wapo watakaosema kuwa pesa ndio kila kitu lakini ukifuatilia utagundua vijana fulani ambao labda wameajiriwa na wanavimishahara visivyozidi milioni tatu, sasa ule umaskini waliotoka kwao wanaona hizo ni pesa nyingi ilhali sio pesa nyingi. Kadiri wanavyokua na maisha yanavyosonga wanakuja kugundua ile pesa ni ndogo.
Hapo wanastaafu wanapewa marupurupu yao. Kisha taabu inaanza.

Zipo familia ambazo zinakipato kidogo lakini wazee wao wanaishi kwa furaha kutokana na muunganiko wa familia.
Hakuna jambo zuri kwa Baba kama kuona Watoto wake wako pamoja na wanapendana.

Katika umri wa miaka 50 ndio miaka ambayo Wanaume wengi hutafuta watoto wao waliowazaa mahali mahali na hutamani kuwakusanya wawe sehemu moja na kuwatunza lakini kwa bahati mbaya jambo hilo kwa wengi hufeli.
Ukiwa na mali watoto watakuja wakitaka urithi wao. Ukiwa huna mali watoto watakudharau kisa tuu hukuwalea au ulikuwalea lakini kwa Nyodo na Kiburi kisa tabia yako ya kuoa Oa hovyohovyo.
Ingawaje kiafrika na kimila sio jambo la busara kwa mtoto kumzuia mzazi asioe au kuolewa hovyohovyo lakini matokeo yake huonekana mbeleni.

Ongezeko la idadi ya Single Mothers hainipi picha nzuri kwa maisha ya mbeleni. Itakuwa hatari tupu. Kitakuwa ni kilio sio tuu kwa Wababa bali pia hao single Mothers ambao wamehangaika kwa kila namna.

Suluhisho ni vijana kutokupaparika na kukurupuka kuoa au kuolewa bila tahadhari na umakini.

Acha Nipumzike sasa

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unang'ang'ania mtoto kama huna mbegu bhana! Wewe ni Mwanaume. Sawa kijana Mwanamke akikuringia mtoto muachie. Toto likijifanya halikutaki lifukuze na Achana nalo. Simple tuu!

Alafu uone kama hautaishi Kwa Amani.
Mwanaume hang'ang'anii mtoto

Kwangu kuna Bajeti ya familia tuu.
Hakuna Pesa ya mwanaume au Mwanamke.😊😊
Kukishakuwa na pocket money ya Mwanamke sijui Mwanaume hiyo nyumba tayari inaufa.

MKE wangu haombi Pesa Bali anatumia Pesa zangu kama ambavyo angetumia Wakati akiwa Single.

Mwanamke yeyote akiishi vigezo nilivyoviweka anaweza kuwa mke wangu bila kujali wengine watasema nini

Nina familia ya watu saba, watoto watano na mimi na mke wangu

Na kama utashindwa automatically upo kwenye mkondo wa Laana.
 
Back
Top Bottom