Watoto wanne wa familia moja wafariki kwa ajali ya moto

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Watoto wanne wa familia moja, wamefariki dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 6:30 usiku wa kuamkia leo Jumamosi Septemba 24,2022 katika makazi ya watu yaliyopo ndani ya eneo la mgodi wa Mwadui, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.

Watoto waliopoteza maisha kutokana na tukio hilo, ni Cecilia Richard mwenye umri wa miaka 14, aliyekuwa akisoma darasa la saba katika shule ya msingi Mwadui (C), Clarence Richard mwenye umri wa miaka 6, aliyekuwa akisoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwadui (A), Thadeo Richard mwenye umri wa miaka 3 na Aisha Ashraf mwenye umri wa miaka 6 aliyekuwa akisoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwadui (C).

Chanzo cha moto huo kinataiwa kuwa ni dawa ya mbu waliyokuwa wamewasha watoto hao, muda mfupi kabla ya kulala.

Chanzo: Nipashe
 
Inna lillah wa inna ilaih rajun.

Mungu atutie nguvu wakati huu wa magumu.
 
Back
Top Bottom