Watoto wanaopata ufaulu wa juu na kupata nafasi ya kusoma shule binafsi wanakuwa wahanga katika ufadhili wa elimu ya juu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,275
Sophia binti wa miaka 16 alipata ufaulu wa daraja la kwanza kwa point 17 katika ufaulu wake wa shule ya upili. Baba yake Sophia ni dereva serikalini na mama anafanya biashara ya chakula. Nyumbani wamezaliwa watoto watano na Sophia ni watatu kuzaliwa.

Nyumbani waliishi maisha ya kawaida, wazazi walifanikiwa kujenga nyumba yenye maji na umeme. Baba Sophia alifahamu umuhimu wa elimu hivyo Jumamosi alimlipa mwalimu wa kuwafundisha watoto wake nyumbani hesabu, Kiingereza na Sayansi hasa wakiwa wanajiandaa na mitihani ya kidato cha nne. Baba Sophia ajima kunywa bia na wenzake alihakikisha hili linafanyika. Meza ya kulia Jumamosi inakua darasa.

Majibu ya Sophia yalileta furaha kubwa nyumbani. Furaha ya familia iliongezeka pale Waziri wa Elimu wa nchi ya Umofia alipoandaa tafrija ya kuwapongeza vijana waliofaulu vizuri wakiambatana na wazazi wao.

Mama Sophia alisimamia shughuli ya kununua mavazi ya sherehe. Familia ilipata nguo kutoka Uturuki katika maduka ya mji mkuu wa Umofia. Baba alipata suti, mama gauni na kofia kama Malkia na watoto wote walipendeza.

Katika tafrija kulikua na walimu wakuu wa shule mbalimbali za serikali na za binafsi. Mwalimu Mkuu wa shule ya Kimataifa alitoa zawadi ya ufadhili kwa Sophia kusoma katika shule yake kidato cha tano na sita.

===

Sophia alianza masomo ya kidato cha tano katika shule ya kimataifa. Wanafunzi wengi katika shule hii wazazi wao walikuwepo nchini kwa mikataba ya kimataifa, wengine walikuwa watoto wa wafanya biashara wakubwa. Sophia alifika shuleni kwa miguu akitembea kutoka kituo cha basi. Wenzake walishushwa na magari yenye namba za Ubalozi na LX, Range Rovers mambo kama hayo.

Licha ya masomo ya taaluma, kulikuwa na walimu wa michezo mingi kama tennis, kuogelea, hockey, cricket, football, drama nk. Sophia alikua na kipaji cha tennis na alichaguliwa kushiriki shindano Afrika Kusini lakini wazazi wake hawakumudu gharama za safari hii. Safari nyingine alipata ufadhili. Wazazi wake walimkumbusha kuwa yuko pale kutafuta elimu.

Wakati wa kuomba vyuo, ni wazi kuwa Sophia hakukidhi vigezo vya kupata mkopo katika bodi ya mikopo Umofia. Wanafunzi karibu wote waliomba vyuo Ulaya na Marekani.

Sophia alipata chuo Ujerumani kwa masharti ya kujitegemea kwa malazi na chakula lakini Chuo kitalipa ada ya masomo.

Hii offer haikuwa nzuri sana kwani wazazi wa Sophia hawakumudu. Sophia alipata msongo wa mawazo. Kuna mwalimu mzungu alipenda maombi ya Sophia. Alipiga simu kuulizia Sophia anatoka lini lakini Sophia hakuweza kumudu gharama zile.

Sehemu ya Pili
 
Sophia alianza masomo ya kidato cha tano katika shule ya kimataifa. Wanafunzi wengi katika shule hii wazazi wao walikuwepo nchini kwa mikataba ya kimataifa, wengine walikua watoto wa wafanya biashara wakubwa. Sophia alifika shuleni kwa miguu akitembea kutoka kituo cha basi. Wenzake walishushwa na magari yenye namba za Ubalozi na LX, Range Rovers mambo kama hayo.

Licha ya masomo ya taaluma, kulikua na walimu wa michezo mingi kama tennis, kuogelea, hockey, cricket, football, drama nk. Sophia alikua na kipaji cha tennis na alichaguliwa kushiriki shindano Afrika Kusini lakini wazazi wake hawakumudu gharama za safari hii. Safari nyingine alipata ufadhili. Wazazi wake walimkumbusha kuwa yuko pale kutafuta elimu.

Wakati wa kuomba vyuo, ni wazi kuwa Sophia hakukidhi vigezo vya kupata mkopo katika bodi ya mikopo Umofia. Wanafunzi karibu wote waliomba vyuo Ulaya na Marekani.

Sophia alipata chuo Ujerumani kwa masharti ya jujitegemea kwa malazi na chakula lakini Chuo kitalipa ada ya masomo.

Hii offer haikua nzuri sana kwani wazazi wa Sophia hawakumudu. Sophia alipata msongo wa mawazo. Kuna mwalimu mzungu alipenda maombi ya Sophia. Alipiga simu kuulizia Sophia anatoka lini lakini Sophia hakuweza kumudu gharama zile.

Inaendelea
 
Bora kuunga kuunga ukawa huru kuliko kuja kupambana na riba.Sitochukua mkopo Ili kuja kutesa wanangu na riba.mikopo ni ghali kuliko kuunga unga
Ungau unga wake wajihusishe na vitendo hatarishi vitakavyowaharibu kuliko hata huo mkopo..
Ushoga
Usagaji
Madawa ya kulevya
Umalaya.
Huna uwezo kopa... Mkuu ... Mtashirikiana kulipa Deni ..Kama unaona unampenda Sana...
Mbona Kuna waliomaliza madeni Helsb wamewezaje...
 
Back
Top Bottom