Nimeshtushwa na idadi ya watoto wanaosoma shule binafsi kurudishwa shule za Serikali

mr pipa

JF-Expert Member
Jul 26, 2021
2,330
4,854
Nimeenda shule moja ya msingi ya Serikali na kukuta Wazazi kama 48 wakiomba kuwahamishia watoto wao katika shule hiyo ya msingi. Hiyo inaweza kuwa ina maana gani?

Kwamba hali ni ngumu ya kimaisha kwahiyo kipato hakikidhi mahitaji au wameona huko private hakuna la maana zaidi ya kujua Kiingereza? Najua wazazi mliofanya hivyo mpo humu mngetupa majibu tupate mwanga.
 
Ukisomesha mtoto private school, basi isiwe mtaala wa Tanzania.

Kumsomesha mtoto private ya mtaala wa Tanzania ni kupoteza pesa bure.

Kwa sababu hakuna value addition, hakuna kitu extra mtoto anakuja nacho kuliko mtoto aliesoma shule za serikali.

Ukisema kingereza, hii ni hoja ya kipumbavu kwa sababu kwa ulimwengu wa sasa kutokujua kingereza hakujawahi kua kikwazo cha watu kufanya shughuli zao. Mfano, Tanzania tuko 61+M, watumiaji wa simu wako 34m, asume 30% ni double line, watumiaji wanabaki 24m, toa watoto ambao ni 31m, watu wasio na simu hawazidi 10m

Sasa je, Tanzania kila mtu mwenye simu anatumia simu vizuri kuwasiliana na simu zote 99% zinatumia kingereza, je watu wameshindwa kuwasiliana kisa kingereza?
 
nimeenda shule moja ya msingi ya serikali na kukuta wazazi kama 48 wakiomba kuwahamishia watoto wao katika shule hiyo ya msingi hiyi inaweza kuwa inamaana gani ?? Kwamba hali ni ngumu ya kimaisha kwahiyo kipato hakikizi mahitaji au wameona huko privet hakuna la maana zaidi ya kujua kiingeleza najua wazazi mliofanya hivyo mpo humu mngetupa majibu tupate mwanga
Ukimsomesha mwanao private,kupata ajira ni fasta,
 
nimeenda shule moja ya msingi ya serikali na kukuta wazazi kama 48 wakiomba kuwahamishia watoto wao katika shule hiyo ya msingi hiyi inaweza kuwa inamaana gani ?? Kwamba hali ni ngumu ya kimaisha kwahiyo kipato hakikizi mahitaji au wameona huko privet hakuna la maana zaidi ya kujua kiingeleza najua wazazi mliofanya hivyo mpo humu mngetupa majibu tupate mwanga
Mnapoambiwa nchi imejaa umasikini muwe mnaelewa
 
Huu uzi ZITAJAA OPINIONS TUUU kuliko FACTS.
Na makasiriko ya watu baada ya mdororo wa kiuchumi una nafas yake katika opinion hizo 😂😂.

NB
maisha sio mashindano.
Ishi uwezavyo na vile upendavyo.
No body cares..no nody thinks of your moves. Was was wako tu
 
Watu wanajifariji wakati pvt schools zina wanafunzi kibao, and truth be told 98% ya wabongo wangependa watoto wao wasome shule za pvt quality kama Feza, St Francis na nyinginezo, kikwazo uchumi na uwezo wa watoto tu,

Kama hauna hela usikatishe tamaa wenzako
 
nimeenda shule moja ya msingi ya serikali na kukuta wazazi kama 48 wakiomba kuwahamishia watoto wao katika shule hiyo ya msingi hiyi inaweza kuwa inamaana gani ?? Kwamba hali ni ngumu ya kimaisha kwahiyo kipato hakikizi mahitaji au wameona huko privet hakuna la maana zaidi ya kujua kiingeleza najua wazazi mliofanya hivyo mpo humu mngetupa majibu tupate mwanga
Uongo weka majina Yao hao watoto na shule wanazotoka na wanazohamia za serikali
 
Private saa hivi ghali sana, wa kwangu yupo nursery bado lakini ada ya mwaka ni ada ya mara mbili niliyokua nalipa chuo.... Usafiri tu nalipa 1.1M kwa mwaka, hapo bado ada, stationary,hela ya mitihani, uniform na takataka kibao...

Huyu mwingine bado hajaanza shule, sasa kama una watoto wanne aisee hapo Kuna kutoboa kweli

Private nyingi ukiweka na usafiri ada ni kama 2M kwa mwaka
 
Watu wanajifariji wakati pvt schools zina wanafunzi kibao, and truth be told 98% ya wabongo wangependa watoto wao wasome shule za pvt quality kama Feza, St Francis na nyinginezo, kikwazo uchumi na uwezo wa watoto tu,

Kama hauna hela usikatishe tamaa wenzako

St francis sio shule ya msingi english medium.

St francis ni sekondari ambayo inaaanzia form one.
 
Private saa hivi ghali sana, wa kwangu yupo nursery bado lakini ada ya mwaka ni ada ya mara mbili niliyokua nalipa chuo.... Usafiri tu nalipa 1.1M kwa mwaka, hapo bado ada, stationary,hela ya mitihani, uniform na takataka kibao...

Huyu mwingine bado hajaanza shule, sasa kama una watoto wanne aisee hapo Kuna kutoboa kweli

Private nyingi ukiweka na usafiri ada ni kama 2M kwa mwaka
Usike ukaongea mwenyewe mkuu. Chukulia maisha kwa urahisi mkuu
 
Back
Top Bottom