Watanzania Wengi Wana Chuki, Wivu na Husda

Watanzania Wengi Wana Chuki, Wivu na Husda

Watu hawana kazi unawaringishia Bentley na Rolls Royce unategemea nini?

Tena ashukuru wanamsema tu hawajataka kumuua na kumuibia.

Tunkjoelekea huko kwa tofauti hii ya kipato, kutatokea magenge ya utekaji watu ya kuwaachia kwa kulipwa (kidnap for ransom gangs).

Sitetei mambo hayo, naelezea tu uhakisia.

Katika maisha kuna kanuni moja inaitwa "Dark Forest Hypothesis" kwamba maisha ni kama msitu mnene wenye wanyama wakali usiku wa kiza. Ukiwa katika msitu huo hutakiwi kujionesha sana, unavyozidi kujionesha sana , kuna wanyama wakali wanaweza kukudhuru.

Wasanii wana changamoto kwa sababu kazi zao zinakuwa promkted kwa wao kujionesha.

Ila pia, hata kujionesha kunaweza kufanywa kwa akili kimkakati.

Kuna nyumba za yatima msanii anaweza kuonesha uwezo wake, kujitangaza, na kusaidia yatima kwa namna ambayo hata majambazi yenye akili yanaweza kumuheshimu.
 
Umasikini wa kipato ni kitu kibaya sana.
Wengi wanaotoa povu kwa mali za watu ndiyo hao wanaohangaika na maendeleo ya wengine kwenye mitaa tunayoishi
 
Nakumbuka miaka michache nyuma kuna msanii maarufu alinunua Rolls Royce. Kwa kweli mitandao ilichafuka kwa kebehi,kashfa na maneno mengi yenye mlengo hasi. Mara used, mara bei kaongeza sifurimara sio lake,mara matairi vipara basi tu ili mradi watu waliojaa sumu mwilini wazitoe na wamshushe.

Sasa hivi karibuni mke wa huyu msanii kanunua Bentley, yaani maneno yale yale yamerudi. Mara used, bei yake sio ile ni hii yaani ni tafrani ili mradi tu kumshusha. Wengine wanaenda mbali zaidi kuingia mitandaoni kutafuta gari kama hio iliogongwa au kuwa scrapped huko ughaibuni na kusema ndio bei za haya magari.

Kwanini watu wanakuwa na roho za namna hii? Hata humu JF mtu akipost kitu chake gari au nyumba watakuja watu na kuanza kumkashifu kwa maneno ya kejeli na dhihaka. kwanini lakini? Yaani watu wako busy na mitandao mwezi mzima kujadili gari ya mtu kuwa bei ni ndogo sana,mara used sasa hata ikiwa used wewe unapungukiwa nini? Au kama inauzwa 10m yeye kasema 100m wewe unapungukiwa nini?
Umaskini umaskini umaskini.
 
Back
Top Bottom