Dawa za Kulevya: Serikali yawatia Mbaroni Mapapa 7 wa Unga

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,744
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamisha jenereli wa Kudhibiti na kupambana na madawa ya Kulevya bwana Kyimo imesema Wafanyabiashara hao wakubwa wa Kimataifa wametiwa mbaroni Mkoani Dar na Iringa.

Wamekutwa na dawa za Kulevya kilo zaidi ya 3182 ambazo kama zisingekamatwa zingeathiri watu mil.76.

========

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), imekamata kilo 3,182 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya oparesheni maalum iliyofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Iringa kati ya Desemba 5 hadi Desemba 23, mwaka huu.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo, Desemba 27, 2023 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo alipozungumza na waandishi wa habari.

"Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180.29 za dawa aina ya methamphetamine ambayo ni mpya katika soko," amesema.

Kulingana na Lyimo, watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na wawili kati yao wana asili ya Asia na kwamba huo ndiyo mtandao mkubwa zaidi wa dawa za kulevya nchini.

Alipoulizwa kuhusu majina yao, amesema ni vigumu kuwataja kwa sababu za kiuchunguzi.

Chanzo: Mwananchi

-----

My Take:
Hongera sana Kamishna Kwa kazi nzuri.

Vijana wa Mama wako kazini kuwalinda Watanzania na maharamia.

View: https://twitter.com/PMadeleka/status/1740766418717565040?t=YO9glMG-CPB27Egy_ixg9w&s=19
 
Back
Top Bottom