Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Sikutegemea Mradi wa kubeba abiria Dar es Salaam akabidhiwe kampuni ya kigeni. Usafirishaji ni sekta ambayo Watanzania wanafanya vizuri sana. Nchi nzima mabasi yanamilikiwa watanzania wenzetu. Wanasafirisha abiria bila kelele wala malalamiko tena kwa mabasi mazuri yenye huduma zote.
Kafulila na wenzake walipoambiwa kubinafsisha wakakimbilia kwenda kutafuta wageni kwa kigezo kwamba Watanzania hawana uwezo wa kufanya hizi kazi. Naomba kuuliza kuna mgeni anamiliki dala dala au zinimilikiwa na Watanzania? Kuna kampuni ya mabasi ya wageni au makampuni haya ni ya watanzania?
Watumishi wa umma kama ninyi biashara imewashinda mnaamini kila Mtanzania biashara imemshinda? Leo hii wapo watanzania wanaweza kukopesheka magari huko China wakalipa taratibu sawa na ambavyo huyu Mwarabu anakwenda kufanya.
Kwanini tufikie kukabidhi kila kitu kwa wageni? Tuambieni kuna ugumu gani wa kusimamia mradi wa Mwendokasi hadi tukamtafute RAIA wa kigeni aje kutuongoza? Tuliomba kura za kubinafsisha kwa wageni kila kitu?