Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Nisome tena:

quote_icon.png
By FaizaFoxy

Sijui kuhusu Julius Kambarage maana na yeyey ni JK pia. Lakini kama unamaanisha Jakaya Kikwete, hapana dini yake ni Uislam na Uislam unaujuwa japo kwa kuusikia tu, sina haja ya kuelezea hilo.

Naam, Jakaya Kikwete katika mambo makuu aliyosimamia ni ufisadi na wizi na hilo ni ukweli kabisa na nafurahi kuwa umeliona. Leo tunaona ufosadi wa toka enzi za Mkapa akiuibuwa, laeo y=tanoana mawaziri na mabalozi wakifikishwa mahakamani kwa wizi na ufisadi.

Leo tunaona TAKUKURU ipo kila wilaya kusimamia wizi, rushwa na ufisadi na inazidi kuongezewa nguvu mara kwa mara, Hiyo ni kwa jitihada za Kikwete kusimamia hayo.

Hapa Nyerere anakujaje sasa.
We Ajuza utakuwa mchawi wewe sio bure
 
Ondoa mambo ya ISIS hapa, inawazuia nini kuenedelea na hizo mahakama huko misikitini. Kutumia kodi za wakristo kwa mahakama za kiislam ni dhulma.

Jee, wewe utachaguwa kiongozi au chama?
 
Hujuwi kuwa JK ni Julius Kambarage pia? au unajitia umajununi usiokuwa nao?

Mimi nimesema JK from.2005 Mpaka sasa,sasa hapa JK Nyerere anaingiaje.
Hizi Ashk Majnun za jumamosi mbaya sana...
 
Nisome tena:

quote_icon.png
By FaizaFoxy

Sijui kuhusu Julius Kambarage maana na yeyey ni JK pia. Lakini kama unamaanisha Jakaya Kikwete, hapana dini yake ni Uislam na Uislam unaujuwa japo kwa kuusikia tu, sina haja ya kuelezea hilo.

Naam, Jakaya Kikwete katika mambo makuu aliyosimamia ni ufisadi na wizi na hilo ni ukweli kabisa na nafurahi kuwa umeliona. Leo tunaona ufosadi wa toka enzi za Mkapa akiuibuwa, laeo y=tanoana mawaziri na mabalozi wakifikishwa mahakamani kwa wizi na ufisadi.

Leo tunaona TAKUKURU ipo kila wilaya kusimamia wizi, rushwa na ufisadi na inazidi kuongezewa nguvu mara kwa mara, Hiyo ni kwa jitihada za Kikwete kusimamia hayo.
hapo kwenye RED unaweza simamia wizi na ufisadi?????ha ha haha haaaaaaa
tafadhari muombe radhi!!!!!!
 
Hiyo ni mifano miwili tu niliyokuwekea ili kudhihirisha hoja yangu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Tanzania hakichaguliwi chama anachaguliwa kiongozi. Hata huko UKAWA mtachaguwa chama? au kiongozi? UKAWA si chama. Fikiri.

Imekuwaje Leo,unatuasa kuchagua kiongozi na si chama ilihali huko nyuma(hata kwenye chaguzi za mitaa) mlipaza sauti zenu, tena kwa mbwembwe nyingi kuwa "tuchague chama" mtu baadae.... kulikoni Leo!

Ni wazi kuwa mmegundua kuwa kwa sasa chama chenu hakina mvuto tena, na kimechokwa,ila mnahisi kuna baadhi yenu walau wanakubalika na ndio maana mmekuja na sarakasi hii.

Binafsi hujanidanganya hata kidogo,na ninawaasa Wadanganyika wenzangu kuwapuuza kabisa.
 
msimamo wako kwenye katiba mpya ni upi maana ccm wanaunga mkono kwa sababu tu ya wazo laccm
 
FF sasa umeanza kujitambua, ya kwamba zama za kuchagua chama zimekwisha! Hapo ni sawa, ila kuna swala la kujiuliza ambalo kabla ya kuchagua, je huyo mgombea anatoka kwenye mfumo wa namna gani?! Mada yako inaonyesha kwamba kwenye chama fulan kuna shida, so tunatakiwa tumchague mtu personally and not the party!!!
Iko hivi, kwa Tanzania, kuna haja ya kuangalia yote mawili, i.e chama na mtu mwenyewe! Kwa mfano mgombea anaweza kuwa ni msafi na mwadilifu sana ila kutokana na chama alichopo, uadilifu wake hauonekani wala hawezi kusema lolote! Haya tumeyashuhudia hapa TZ, CCM kuna waadilifu ila wahalifu ni wengi kuliko waadilifu! Kama wahalifu ni wengi kuliko waadilifu unategemea nini?!
Kwenye scandal ya ESCROW, waadilifu ndani ya CCM tuliona walivyojipambanua, lakin kutokana na uchache wao haikusaidia lolote na wameonekana wasaliti! Maswala ya chama na mgombea hayana issue kama unavyowaza wewe! Mimi nashauri tutafute viongozi wazalendo, sio hao Mbwa mwitu walioko huko CCM.....! Hata kama anatoka chama cha kanisa/msikiti, kama sio mzalendo akafie mbali. Nashangaa kuna watu wamepandishwa mahakamani jana eti walipokea rushwa, mbona huyo mtoa rushwa hakupanda mahakamani!

FF nakushauri muwe mnamshauri JK manake anachofanya hata watoto wanamshangaa tena mno!!!! Tibaijuka kaadhibiwa kwa ukosefu wa maadili, wakati huo huo pesa alopokea ambayo ndo iliyomtoa kazin tunaambiwa sio ya umma, sasa ina maana ukipewa hela na mtu ukapokea ndo huna maadili...!? This is nonsense Faiza!!!!
Mwambie JK na genge lake hapo Ikulu, kiama chake hata kaburin kitamfuata.... They can't make us fool as such...!

Na wewe ipo siku hii ID yako itapotea humu. Huezi kutetea uovu namna hii ukategemea kuwa salam! One thing for sure, hata dola ya Rumi ilianguka. Tutafanya kila kitu kwa imani hoping that ipo siku tutaiangusha CCM. Na usidhan kwamba tunaichukia CCM, wengi wetu tunaipenda maana ni chama kilichotutoa mbali, tatizo letu ni hao Mbwa mwitu mliofuga. Kuanzia JK na cabinet yake nzima! Mbwa mwitu hawa wameamua hata kuua wale kondoo waliopo ndani ya zizi kama akina dr. Mvungi na wengine wengi tu wamepotea kisa Mbwa mwitu mnaowafuga hapo ikulu!!! Hivi kweli JK anampa mtu madaraka and then anashindwa kumwajibisha!? Huyu ni raisi goigoi kabisa tena hajui lolote.

Samahan kama utakwazika na lugha yangu..! It's that I'm fed up of you guys...!

Nisome tena post namba moja.

Watanzania hawajaanza leo kuwachaguwa viongozi na si chama, na mifano nimeiweka, rudia post namba moja tafadhali.

Hapa nnawakumbusha tu, usifikiri kuwa Watanzania hawajielewi, isipokuwa ningependa ukumbuke kuwa, leo hii kuna Watanzania ambao mwaka 2005 hawakuwa kwenye umri wa kupiga kura na pengine hata hawajuwi ilikuwaje, hapa nnawakumbusha kuwa Watanzania wakati huo hatukutazama chama tulitazama uwezo wa mgombea, na hilo ndilo la muhimu, Watanzania tunapoelekea kwenye kupiga kura tuwe makini na tusitazame vyama kwani Tanzania tunachaguwa kiongozi na si chama na kiongozi wa kwanza ni wewe mwenyewe, si mwingine. Kumbuka hilo.
 
Safari hii tutazamie tufani ndani ya ccm, hizi kwenye JF ni rasharasha tu. Hapo ni kwamba bado UKAWA hawajaanza kuwavuruga.
Hapana mkuu!
Huyu ni mnafiki hana mapenzi na chama,kachungulia maazimio ya CC kaona wa dini yake kuteuliwa CCM ni vigumu ndo maana anakuja hapa na ngonjera za kuchagua mtu wala sio chama!
kwake yeye uislamu kwanza mengine badae....UKAWA wakimsimamisha muislamu anawaunga mkono!
yaani huyu twaweza kumuita CONDOMU au TOILET PAPER
 
Mfano hai ni mwaka 1995 wakati Kikwete alipowania kuwa Rais kwa mara ya kwanza, hakuna asiyejuwa kuwa alishinda ndani ya chama lakini wenye chama hawakutaka, matokeo unayajuwa.
kwani wenye chama si ni wanachama ama? Sijakuelewa hapo mkuu.
 
nitamchagua mla KITIMOTO wewe je?????

Ngoja nikupe darsa dogo la Kiislam:

Kumbuka ni rahisi sana mimi kumchaguwa kiongozi wa Kikristo anaefata dini yake na ambae hadhalilishi Muislam na asiye Muislam kuliko Muislam asiyefata dini yake na anaedhalilisha Waislam na wasiyo Waislam, kwa sababu Qur'an inasema hivi:

Qur'an 5:82
You will surely find the most intense of the people in animosity toward the believers [to be] the Jews and those who associate others with Allah ; and you will find the nearest of them in affection to the believers those who say, "We are Christians." That is because among them are priests and monks and because they are not arrogant.

Isitoshe, ukisoma historia ya Mtume Muhammad Salla Llahu Alayhi Wasalaam alipopata Utume huko Makkah na alipoanza kufanikiwa kuwabadilisha wengi kutoka katika upagani, kulitokea Waislam wa mwanzo kunyanyaswa na kupingwa na hata kufikia kuuliwa. Mtume Muhammad Salla Llahu Alayhi Wasalaam akawaamrisha waondoke Makkah na wahamie Habash (Ethiopia) na huko Mfalme alikuwa ni Mkristo maarufu kwa jina la Nagash. Nagash akawasikiliza na akawapokea na hakuwadhuru wala kuwafanyia vitimbi.

Na hiyo hiyo Habash (Ethiopia) ndiyo ilikuwa mpaka huku kwetu kwa enzi hizo na ndipo Uislam ulioenea huku kwetu ni kutokana na hao walio "immigrate" mwanzo na kupokelewa vyema na Nagash.

Nadhani kwa darsa hili dogo, utauelewa msimamo wa Kiislam kuhusu kiongozi.
 
kwani wenye chama si ni wanachama ama? Sijakuelewa hapo mkuu.

Nnamaanisha wapo kwenye vyama wanaoamini kuwa wao ndiyo wenye vyama na maamuzi yao ni ya mwisho. Na wapo wanachama wanaoamini kuwa hivi vyama vina wenyewe. Hilo linatokea sana kwenye vyama vyetu. Mfano mzuri ni kura za maoni na nimeelezea juu huko, kaisome vizuri post namba moja.
 
Back
Top Bottom