Haya ndiyo maazimio ya cc - ccm Zanzibar. Baada ya ccm kujua wamechafuka na chama chao hakikubaliki tena, waliazamia kupiga kampeni za kuchagua mtu ili watu wasiangalie maovu ya ccm!. Ff hii inajulikana.
a
Mara zote Kikwete amekuwa msaliti wa umma kwa kufuata maazimio ya chama chake. Mfano sahihi ni BMK. Amebariki mchakato na amepokea draft ya Warioba, ameikubali na akaenda mbele zaidi na ku isaini. Ccm walipoikataa kwamba haina maslahi kwao, wakapanga na namna ya kuivuruga, na bahati nzuri kwake wakamtask kuvuruga, AKAVURUGA KWA UTASHI WA CHAMA.
Amekaa na watetezi wa katiba ya wananchi, wamepatana mchakto wa katiba usitishwe, lakini ccm wakamgomea, wakaendeleza hadi hapo wlaipo sasa. Na yeye kama mwanaccm mwaminifu, ameshindwa kusimamia maazimio yale aas if hayakuwepo, na sasa anatekeleza matwaka ya ccm.
Hatutachagua mtu bila kuangalia chama chake kwa sababu chama ndicho kitakachomwongoza na kumpa dira katika uongozi wake wote!.
Acheni kudanganya watu Faizafoxy. Huyu mtu hataunda serikali nje ya chama chake, hatekelezi sera zake nje ya chama chake, hatengenezi mfumo nje ya misingi ya chama chake, hatekelezi ilani nje ya zile za chama chake. Iweje leo mseme tuchague mtu bila kuangalia chama? Hii ni nini?
Vinginevyo atangaze yeye ni mgombea binafsi hana chama, tutamwangalia kwa namna ile lakini tutahitaji kujua anaunda serikali kwa utaratibu upi iwapo anashinda.
Hii kampeni ninaona ni kutaka kuficha makovu ya ccm kwa sababu haitakiwi, halfu tujikute tumewapa uongozi waendelee kutunyonyoa wakavu wakavu!.
Aidha mtu ana chama tutamwangalia na chama chake, ama awe binafsi bila chama tutamtathimni muundo wake pendekezwa wa serikali yake ukoja.
Kuchanganyachanganya mambo hapa ni hila na hatukubali
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.
Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.
Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.
Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.
Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.
Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.
Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.
Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.
Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.