Watanzania, huu ni wakati wa kufunga na kuliombea Taifa. Mkataba wa Bandari zetu ni mlango usiopendeza kwa haya yanayoendelea

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,755
Amani iwe kwenu Watanzania

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeainisha wazi kwamba serikali haina dini na imeenda mbali zaidi kwa kutoa hakikisho lenye ulinzi wa Kikatiba wa Uhuru wa Kuabudu. Ingawa kiutekelezaji wake unahitaji ithibati ya serikali isiyojiingiza kwenye masuala ya kiimani directly.

Baada ya dibaji hii, wacha tuingie kwenye hoja yangu niliyodhamiria kuwaomba.

Hivi sasa nchi yetu inapitia kipindi kigumu sana kutokana na mienendo ya wanasiasa na makundi mengine ya kijamii. ugumu huo umetokana na sababu kadha wa kadha zikiongozwa na sakata la Inter-Governmental Agreement (IGA) kama lilivyopelekwa Bungeni na serikali ili kupata ridhio. Ingawa inaonesha kupelekwa kwa mkataba huo kuridhiwa na Bunge kumefanyika huku ikiwa tayari Mkataba huo kupewa nguvu za kisheria kwa viongozi wa serikali kuusaini kabla ya kuridhiwa na Bunge.

Mambo mengine, ni ongezeko la ufa wa Muungano baada ya wanasiana na makundi ndani ya jamii kuamua kubeba agenda ya Uzanzibari na Utanganyika katika kupeleka hoja zao kwa wananchi. Haya yote yanafanyika kwa upotofu na usahihi katika wakati mmoja. Viongozi wa nchi wamekosa kauli thabiti kiasi kwamba inawatumia watu wanaoonekana kutokuwa na taaluma ya kuzungumzia uzuri na manufaa ya IGA ambao ni wale ambao hawana upeo maridhawa ya kujadili ama kuchambua mikataba hususani inayohusisha taaluma stahiki ya Sheria za Mikataba ya nchi na nchi.

Leo tunamuona mtu kama Maulidi Kitenge, Mwijaku, Baba Levo. Steve Nyerere, Mhe. Msukuma na Watanzania wachache ambao elimu zao siyo jambo la kujifcha wakitumika kujibu hoja za wanazuoni kama vile Maaskofu, Masheikh, Wanasheria ikiwemo TLS, Maprofesa (Shivji and Co) na wananchi waliojitokeza kuchambua clauses za Mkataba huu....

Hii ni wazi kama Taifa tumeamua to embrace anguko la elimu kwa hizi makusudi zinazoendelea. Hata humu Mitandaoni tunaona hata wale wenye kuonesha kuwa uelewa fulani wakija na hoja nyepesi zinazosukuma ulazima wa wananchi kukubaliana na move ya serikali ambayo awali imeshaonesha wazi kutosikiliza kilio cha wengi ambao wanatamani serikali ikubali kuupitia upya Mkataba kabla haujaanza kutekelezwa. Tumeona baadhi wakizawadiwa vyeo baada ya kutoa kauli zinazoonekana ni nyepesi zinazohusu huu mkataba

Nimeongea haya kwa lengo kwamba tuangalie kama Taifa tunachukua msimamo upi? Swali hili si jepesi kwa divided state. nasema Divided State kwa sababu hata ndani ya serikali wameshaanza kujitokeza sauti zinazoashiria kutokuwa na kauli ya pamoja kuhusu huu mkataba. Kwa wenye macho na wasioyatumia kuona wanaweza kushangilia hii hali. lakini kwa wenye hekima na upeo wa kiroho wataona dalili ama kiashiria kibaya tena kitisho kwa nchi kama taifa ambalo limedumu katika umoja, mshikamano na kuvumiliana.

Dalili zote zinaashiria, kipimo cha uvumilivu na mshikamano wa Wananchi vipo shakani kutokana na kauli zinazotokana na wanasiasa wa pande zote. hata ukimya wa wanaoelewa haya mambo ni dalili mbaya sana. Kujitokeza kwa wastaafu na wazee kuelezea mashaka yao juu ya IGA kati ta Tanzania na Dubai, ni hatua inayoashiria kukosekana kwa ushwari ndani ya mamlaka zetu za nchi.

Niwaangukie wenye nia njema na nchi yetu kupaza sauti zao kumlilia Mungu (kila mtu kwa imani yake) atuvushe salama kwenye kipindi hiki kigumu sana. Kama kosa limefanyika ama halijafanyika hayo yatajulikana huko mbele. cha muhimu ni kufunga na kuomba ili kuiombea nchi na viongozi wake. Viongozi tunaowaombea ni wote yaani wanashika hatamu za nchi sambamba na wapinzani maana kila mmoja ana umuhimu kwenye siasa za nchi yetu.

Bandari Salama ibaki katika dhima ya jina lake. Tanzania ibaki salama, Amani yetu isalie kama tunu zetu, Tusiruhusu mazingira ya majeshi ya kulinda amani kupiga kambi ndani ya Tanzania yetu.

Tuwaombee ulinzi wa Mungu wale wote wanaopokea vitisho dhidi ya misimamo yao juu ya huu Mkataba. Mungu awalinde, awaepushe na mdomo wa mauti ama madhara yeyote yatokanayo na makusudio ya wanadabu na ibilisi.

Tuwaombee wenetu na watoto ambao bado hawajazaliwa ili wao nao wafaidi uhuru, haki na keki ya Taifa letu.

Tuwaombee wale wote wanaounga mkono Mkataba huu kama una tija kwa Taifa basi misimamo yao iweze kueleweka kwa Watanzania, kama ni mkataba unaoliingiza Taifa katika sintofahamu basi shauri lao likageuzwe ili kuutupilia mbali huu mkataba.

Naandika haya nikiwa na wivu mkubwa na mahaba tele kwa Taifa letu sote la Tanzania.

Msanii wa JF
 
Ndio tuombe, tutaomba kwa mukhtadha upi, kupinga au kukubali mkataba au neutral? Kama kuna wanadini wanaopinga na wanaounga mkono mkataba Mungu awe upande gani? Any way wananchi wote wasikilizwe hoja zao na pawepo na muafaka katika kuweka mustakabali wa taifa
 
Mpaka sasa, wanaopinga ni 1% tu ya watanzania, sema wengi wao ni wale 'wajanja' wa mitandaoni na ni watu wa kukamatia fursa km hao kina lissu and co. 99% huku mtaani tunataka huu uwekezaji.......tumevurugwa miaka mingi kiasi kwamba tunatamani mabadiliko. Tuko pamoja saaaaaaaana na mama!!
 
Kinacho udhi ni viongozi kulazimisha wananchi kuukubali huo mkataba,

ilihali wanaelewa DP world imeshaleta mtafaruko huko Kenya Kwa kuwapiga na kitu kizito
 
Huu mkataba wewe binafsi unaupendea kipengele kipi.?
 
Mimi ninachoona ni hatari iliyopo mbele yetu kama Taifa.

Tunajiundia timu kila upande. Mimi sipo neutral ninajua ninachokitaka. Lakini muhimu na kubwa kuliko vyote ni Tanzania na Watanzania kwanza.

Tumuombe Mungu atuvushe
 
Ndio tuombe, tutaomba kwa mukhtadha upi, kupinga au kukubali mkataba au neutral? Kama kuna wanadini wanaopinga na wanaounga mkono mkataba Mungu awe upande gani? Any way wananchi wote wasikilizwe hoja zao na pawepo na muafaka katika kuweka mustakabali wa taifa
Ukinisoma vizuri utaelewa muktadha wa kuombea.

Kama ni mkataba mzuri basi tuukubalu na iwapo ni wa magumashi basi ukataliwe mbali.

Kikubwa Mungu atusaidie maana wanadamu hatuaminiani
 
Kinacho udhi ni viongozi kulazimisha wananchi kuukubali huo mkataba,

ilihali wanaelewa DP world imeshaleta mtafaruko huko Kenya Kwa kuwapiga na kitu kizito
Mimi nimeukubali huo mkataba, wananchi gani waliolazimishwa?
 
Bila shaka unamaanisha vipengele kwa tafsiri za lissu, slaa na tibaijuka and Co., Sio? Sidhani kama umewahi kumsikiliza mwingine yeyote!
Jibu swali ndugu yangu.
Mkataba huu umeupenda kwa kipengele kipi kilicho kugusa.
Kama huna copy sema nikutumie.
Ungeniuliza Mimi kwanini nauchukia ningeweka bayana.
 
Amani iwe kwenu Watanzania

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeainisha wazi kwamba serikali haina dini na imeenda mbali zaidi kwa kutoa hakikisho lenye ulinzi wa Kikatiba wa Uhuru wa Kuabudu. Ingawa kiutekelezaji wake unahitaji ithibati ya serikali isiyojiingiza kwenye masuala ya kiimani directly.

Baada ya dibaji hii, wacha tuingie kwenye hoja yangu niliyodhamiria kuwaomba.

Hivi sasa nchi yetu inapitia kipindi kigumu sana kutokana na mienendo ya wanasiasa na makundi mengine ya kijamii. ugumu huo umetokana na sababu kadha wa kadha zikiongozwa na sakata la Inter-Governmental Agreement (IGA) kama lilivyopelekwa Bungeni na serikali ili kupata ridhio. Ingawa inaonesha kupelekwa kwa mkataba huo kuridhiwa na Bunge kumefanyika huku ikiwa tayari Mkataba huo kupewa nguvu za kisheria kwa viongozi wa serikali kuusaini kabla ya kuridhiwa na Bunge.

Mambo mengine, ni ongezeko la ufa wa Muungano baada ya wanasiana na makundi ndani ya jamii kuamua kubeba agenda ya Uzanzibari na Utanganyika katika kupeleka hoja zao kwa wananchi. Haya yote yanafanyika kwa upotofu na usahihi katika wakati mmoja. Viongozi wa nchi wamekosa kauli thabiti kiasi kwamba inawatumia watu wanaoonekana kutokuwa na taaluma ya kuzungumzia uzuri na manufaa ya IGA ambao ni wale ambao hawana upeo maridhawa ya kujadili ama kuchambua mikataba hususani inayohusisha taaluma stahiki ya Sheria za Mikataba ya nchi na nchi.

Leo tunamuona mtu kama Maulidi Kitenge, Mwijaku, Baba Levo. Steve Nyerere, Mhe. Msukuma na Watanzania wachache ambao elimu zao siyo jambo la kujifcha wakitumika kujibu hoja za wanazuoni kama vile Maaskofu, Masheikh, Wanasheria ikiwemo TLS, Maprofesa (Shivji and Co) na wananchi waliojitokeza kuchambua clauses za Mkataba huu....

Hii ni wazi kama Taifa tumeamua to embrace anguko la elimu kwa hizi makusudi zinazoendelea. Hata humu Mitandaoni tunaona hata wale wenye kuonesha kuwa uelewa fulani wakija na hoja nyepesi zinazosukuma ulazima wa wananchi kukubaliana na move ya serikali ambayo awali imeshaonesha wazi kutosikiliza kilio cha wengi ambao wanatamani serikali ikubali kuupitia upya Mkataba kabla haujaanza kutekelezwa. Tumeona baadhi wakizawadiwa vyeo baada ya kutoa kauli zinazoonekana ni nyepesi zinazohusu huu mkataba

Nimeongea haya kwa lengo kwamba tuangalie kama Taifa tunachukua msimamo upi? Swali hili si jepesi kwa divided state. nasema Divided State kwa sababu hata ndani ya serikali wameshaanza kujitokeza sauti zinazoashiria kutokuwa na kauli ya pamoja kuhusu huu mkataba. Kwa wenye macho na wasioyatumia kuona wanaweza kushangilia hii hali. lakini kwa wenye hekima na upeo wa kiroho wataona dalili ama kiashiria kibaya tena kitisho kwa nchi kama taifa ambalo limedumu katika umoja, mshikamano na kuvumiliana.

Dalili zote zinaashiria, kipimo cha uvumilivu na mshikamano wa Wananchi vipo shakani kutokana na kauli zinazotokana na wanasiasa wa pande zote. hata ukimya wa wanaoelewa haya mambo ni dalili mbaya sana. Kujitokeza kwa wastaafu na wazee kuelezea mashaka yao juu ya IGA kati ta Tanzania na Dubai, ni hatua inayoashiria kukosekana kwa ushwari ndani ya mamlaka zetu za nchi.

Niwaangukie wenye nia njema na nchi yetu kupaza sauti zao kumlilia Mungu (kila mtu kwa imani yake) atuvushe salama kwenye kipindi hiki kigumu sana. Kama kosa limefanyika ama halijafanyika hayo yatajulikana huko mbele. cha muhimu ni kufunga na kuomba ili kuiombea nchi na viongozi wake. Viongozi tunaowaombea ni wote yaani wanashika hatamu za nchi sambamba na wapinzani maana kila mmoja ana umuhimu kwenye siasa za nchi yetu.

Bandari Salama ibaki katika dhima ya jina lake. Tanzania ibaki salama, Amani yetu isalie kama tunu zetu, Tusiruhusu mazingira ya majeshi ya kulinda amani kupiga kambi ndani ya Tanzania yetu.

Tuwaombee ulinzi wa Mungu wale wote wanaopokea vitisho dhidi ya misimamo yao juu ya huu Mkataba. Mungu awalinde, awaepushe na mdomo wa mauti ama madhara yeyote yatokanayo na makusudio ya wanadabu na ibilisi.

Tuwaombee wenetu na watoto ambao bado hawajazaliwa ili wao nao wafaidi uhuru, haki na keki ya Taifa letu.

Tuwaombee wale wote wanaounga mkono Mkataba huu kama una tija kwa Taifa basi misimamo yao iweze kueleweka kwa Watanzania, kama ni mkataba unaoliingiza Taifa katika sintofahamu basi shauri lao likageuzwe ili kuutupilia mbali huu mkataba.

Naandika haya nikiwa na wivu mkubwa na mahaba tele kwa Taifa letu sote la Tanzania.

Msanii wa JF
CCM wafanye maombi wenyewe. Wananchi wengine wote wapo sawa hiko kikundi kinatafuta shari isiyo ya lazima.
 
Back
Top Bottom