There you are MKUU, mambo ya maigizo tu ya kujaribu kujijenga kisiasa by all means - hooks or crooks everything goes! Mimi binafsi nina imani kwamba JK ana nia thabiti ya kukomesha janga hili la ulaji wa kupindukia - tatizo ni kwamba sasa hivi ana wakati mgumu wa kujuwa amuamini yupi ahache yupi, akipata ushahidi wa kutosha hata huwe rafiki yake kivipi atakutia ndani - mifano tunayo; wakati wa enzi za Kambarage sio kwamba ubadhilifu haukuwepo - ulikuwepo sana lakini sikuwahi kumsikia anamtia former Waziri au katibu mkuu mahabusu au kumfungulia mashitaka! Swali ni kwa nini? sana sana alichokuwa anafanya ni kuwahamisha hamisha na wakati mwingine kuwatelemsha vyeo basi.
Chukulia mfano wa vita vya wahujumu uchumi, nini kilitokea baada ya kukamatwa ndugu yangu marehemu Mzee Barongo, Nyerere kahamuru the late Sokoine amuachie huru Barongo mara moja bila ya kutoa sababu za kulidhisha kwa wananchi, wananchi walipo mzonga zonga Nyerere kuhusu suala la mzee Barongo kuachiwa huru, Nyerere alijibu "Hee ban hee, yaani mtu ukipewa gari kuendesha kwa kasi kwenye barabara ya mashimo atafanyaje? si lazima upunguze mwendo unapofikia kwenye mashimo" kaulihiyo ya Nyerere ilikuwa na dhamila ya kumkingia kifua rafiki ya Barongo!! Nafikili jibu hilo lilimkata maini Mzalendo Sokoine akapunguza kasi ya kushughulikia suala la uhujumu uchumi.
Mimi nikisikia watu wanasema JK ni dhaifu nashanga sana! Hivi angekuwa dhaifu au mtu ambaye hawezi ku-make decision mbona Mh. Lowassa ambaye ni rafiki yake wa karibu na JK angukuwa bado ni Wazari mkuu, wewe unafikili JK angechukuwa simu akampigia SITA kwamba hataki suala la Richmond lijadiliwe Bungeni angeshindwa kuzima hoja ya R'mond? nini kilicho tokea kwa akina Yona, Mlamba, Mgonja na sasa hivi Mzee Iddi Simba - Nani anaweza kutoa ushahidi wa kuonyesha kwamba Marais walio mtangulia JK waliwahi kuwashughulikia marafiki zao bila woga, hakuna.
Nimezungumza mengi kidogo hili wakati mwingine tunapo walahumu watu tujaribu kulinganisha na historia ya tawala zilizo pita.