Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

turudishie mwanahalisi ona sasa majina hatuyajui,kubenea anzisha gazeti lingine kama wanakuzingingua na wafungie mpaka wachoke.
 
Hizi zinaitwa taralila. Watu wa magazeti wanatumia habari kama hizi kuuza magazeti yao. Kama kweli wana majina si wataje? Ni waongo hao hawana kitu.
 
turudishie mwanahalisi ona sasa majina hatuyajui,kubenea anzisha gazeti lingine kama wanakuzingingua na wafungie mpaka wachoke.

Kweli mkuu,afanye kama malaria sugu,akipigwa BAN id moja anafungua nyingine kumi na tatu! teh teh
 
Habari kama hizi zikikamilika, wene kupenda mabadilko wahakikishe zinawafikia wananchi wote mpaka vijijini ndani ili waelewe jinsi CCM inavyowasaliti siku zote. Huu ni mtaji mkubwa wa kuwafanya wanyonge wawe na ujasiri wa kuiondoa CCM madarakani tena kwa aibu kubwa. Mafedhuli CCM waondoke hawana maana kabisa. Aibu gani hii ee Mungu!
 
Wangumpa Kubenea dakika 1 tu alipoti details za kufa mtu juu ya hili then wamfungie tena........haya magazeti yaliyobaki ni ma-kanjanja
 
toa majina ritz leo nimeona umeanza kuwa mzalendo katika post zako zote leo umenifurahisha naomba uchukue kadi ili tukutambue mpiganaji wa kweli
 
Kumiliki si hoja, hoja ni zilipatikanaje. kama wana shughuli halali nje ya nchi, kwani kuna kosa hapo?????????????
 
Tatizo lako wewe ni Chadema Addicted kila sehemu unaleta ushabiki wa vyama unadhani watanzania wote ni wafuasi wa vyama vya siasa hapa tunaongelea maslahi ya Taifa.

Kumbe Huna ata shin'g kumi kwenye acc ya nje!!!. Ndio maana kimekuuma wewe wanakutuma wao wanachuma. hilooooo!!:loco:
 
zitto-kabwe-top-safi.jpg


KASHFA YA MABILIONI KUFICHWA USWISI: Watanzania 27 wahusikaMMOJA AMILIKI SH90 BILIONI,WENGINE WANNE WAFICHA SH112 BILIONI
WATANZANIA 27 wakiwamo wanasiasa na wafanyabiashara, imebainika kuwa ndiyo wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).Katika uchunguzi wake, Mwananchi imebaini pia kuwa kiasi cha fedha kilichothibitishwa kumilikiwa na Watanzania hao ni jumla ya Dola za Marekani 186 milioni (Karibu Sh300 bilioni) kwa viwango vya sasa vya kubadilishia fedha ambavyo ni Sh1600 kwa Dola ya Marekani.

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni), mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni).

Kwa kuangalia fedha hizo ni dhahiri kwamba vigogo watano tu kati ya kundi la Watanzania 27, wanamiliki Dola 126 milioni (Sh201.6 bilioni) sawa na asilimia 67.74 ya fedha hizo, wakati wengine 22 waliobaki wanamiliki Dola 60 milioni (Sh96 bilioni) sawa na asilimia 32.25.

Kwa hesabu za kawaida, kiasi cha Sh300 bilioni, kinaweza kugharimia ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 33,300, ikiwa chumba kimoja kinaghirimu kiasi cha Sh9 milioni.

Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wafanyabiashara wanaomiliki kiasi cha dola kati ya milioni mbili na milioni saba. Kadhalika wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao akaunti zao zina kiasi kisichozidi Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Kashfa ya kuwapo kwa vigogo walioficha fedha zao nchini Uswisi iliibuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini mwezi Juni mwaka huu, na baadaye mwangwi wake kulitikisa Bunge katika mkutano wake wa nane uliomalizika juzi mjini Dodoma.

Habari hizo zilikuwa zikinukuu taarifa ya Benki Kuu ya Uswisi iliyoitoa na kuonyesha kuwapo kwa kiasi cha Sh315.5 bilioni zilizotoroshwa Tanzania na kufichwa nchini humo na vigogo ambao ni wanasiasa pamoja na wafanyabiashara.

Jumatano wiki hii, tuhuma hizo ziliibuka bungeni ambapo Kambi ya Upinzani ilidai kwamba inawafahamu wahusika wa ufisadi huo na kutishia kuwataja ikiwa Serikali haitawataja.

Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kambi yake kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Fedha na Uchumi alisema, miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni
kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

“Kambi ya Upinzani bungeni imepata taarifa mmoja wa viongozi wa juu kabisa wa Tanzania na baadhi ya mawaziri wa awamu zilizopita ni miongoni mwa watu wenye fedha hizi,” alisema Zitto huku akiitaka Serikali kuliambia taifa ni hatua gani itakazochukua kurejesha fedha hizo pia kuwataja wamiliki wake.

Baada ya Zitto kumaliza kuwasilisha hotuba yake, Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole-Sendeka aliomba mwongozo wa Spika kuhusu suala hilo, akisema kuwa tuhuma hizo ni nzito, hivyo kumwomba Naibu Spika, Job Ndugai amtake kutoa ufafanuzi ama ikiwezekana kuwataja wahusika.

Hata hivyo, Ndugai baadaye alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi kwani Zitto hakuwa na ushahidi wa kuthibitisha kauli yake wala kuwataja wahusika kama ambavyo alidai, huku akimtuhumu kwamba anautumia vibaya Ukumbi wa Bunge kwa kutoa tuhuma nzito bila kuzifanyia utafiti.


Uchunguzi zaidi
Katika hotuba yake bungeni, Zitto alidai kuwa fedha hizo zinatokana na biashara (deals) zilizofanywa na watendaji wa Serikali na wafanyabiashara kwenye sekta za nishati na madini na kwamba sehemu kubwa ya fedha zililipwa na kampuni za utafutaji mafuta na gesi katika Pwani ya Mkoa wa Mtwara zilizopewa mikataba kati ya mwaka 2004 na 2006.

Hata hivyo, uchunguzi zaidi wa gazeti hili umebaini kuwa fedha zilizopo kwenye akaunti za vigogo wanaohusishwa na ufisadi huo, mara ya mwisho ziliwekwa kwenye akaunti husika mwaka 2005.

Taarifa zaidi ambazo Mwananchi limezipata zinadai kuwa taarifa za kufichwa kwa mabilioni hayo ya shilingi nchini Uswisi zimekuwa zikipatikana kwa msaada wa Mbunge mmoja wa zamani wa Afrika Kusini, (jina tunalihifadhi kwa sasa).

Akizungumza jana Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) anasisitiza kuwa walioweka fedha hizo nchini Uswisi wanafahamika na kwamba ikiwa Serikali haitawataja na kuwachukulia hatua, wao (Chadema) watawataja wakati mwafaka ukifika.

“Kama nlivyowahi kusema, tufanye kama nchi ya India, wenzetu hawa walitangaza kwamba watu wote walioweka fedha nje ya nchi kwa njia isiyo halali, wazirejeshe. Walifanikiwa sana, na sisi tunapaswa kufuata nyayo hizo, fedha hizo tunazitaka ili zitusaidie katika kuendesha uchumi wetu,” alisema Zitto.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Je, katika bank accounts hizo kulishafanyika transactions zozote za kutoa pesa? au kufanya manunuzi makubwa kupitia bank account hizo? si ajabu kila mmoja alishachota bulungutu la nguvu au kununua assets mbali mbali kama vile magari ya bei mbaya, Apartments, nyumba kule Dubai, Rio De Janeiro, London, Paris, Hong Kong, New York, Washington, Los Angeles, San Diego, Amsterdam n.k.
 
Job Ndugai ni mhuni! Amefanya utafiti gani ambao kwao anasema kuwa Zitto ni mwongo?
Viongozi hawa ni aina ya 'Bora liende' na anahisi akiruhusu mjadala wa jambo hilo SERIKALI itamwona hafai, kumbe hajui kuwa analipeleka Bunge Mabwepande, pamoja na serikali ya JK.
 
Job Ndugai ni mhuni! Amefanya utafiti gani ambao kwao anasema kuwa Zitto ni mwongo?
Viongozi hawa ni aina ya 'Bora liende' na anahisi akiruhusu mjadala wa jambo hilo SERIKALI itamwona hafai, kumbe hajui kuwa analipeleka Bunge Mabwepande, pamoja na serikali ya JK.

Sishangai Ndugai kujibu hivyo kwani CCM ni kulinadana, na wakati wanajua mhusika mkuu aliye na pesa nyingi katika maficho hayo ni kiongozi wa juu kabisa serikalini, kwa vyo vyote wanafanya kila liwezekanalo kumlinda na kulindana.
 
Je, katika bank accounts hizo kulishafanyika transactions zozote za kutoa pesa? au kufanya manunuzi makubwa kupitia bank account hizo? si ajabu kila mmoja alishachota bulungutu la nguvu au kununua assets mbali mbali kama vile magari ya bei mbaya, Apartments, nyumba kule Dubai, Rio De Janeiro, London, Paris, Hong Kong, New York, Washington, Los Angeles, San Diego, Amsterdam n.k.

Kama utakumbuka pesa za EPA na nyinginezo zilizotuingiza madarakani 2005, zilikuwa nyingi kwani hizi ni change iliyobaki baada ya kuhitimisha zoezi la kuingia madarakani, na pia miradi imeshasimama, hizo tu wametushtukia wazungu wakati tunaendelea kupitisha bakuli sasa wazungu wanajiuliza kwa nini tusitumie hizo tulizozificha kwao?
 
Job Ndugai ni mhuni! Amefanya utafiti gani ambao kwao anasema kuwa Zitto ni mwongo?
Viongozi hawa ni aina ya 'Bora liende' na anahisi akiruhusu mjadala wa jambo hilo SERIKALI itamwona hafai, kumbe hajui kuwa analipeleka Bunge Mabwepande, pamoja na serikali ya JK.

Kilaza, hajui kinachoendelea!
 
Mkuu TUMBIRI,

Heshima ni kitu cha bure kuwa wewe mfuasi wa Chadema aikupi nafasi kutukana wenzako JF ni sehemu ya mijadala tujaribu kueshimiana na kuvimiliana ndio ungwana tupambane kwa hoja sio kwa lugha ya kudhalilishana.

JF Daima.
 
Last edited by a moderator:
Hawa Wazungu nao ni tatizo maana wanaona madudu chungu nzima kila kukicha lakini bado wanaendelea kutoa "misaada" tu na mikopo ambayo maendeleo yake hayaonekani zaidi ya deni la Taifa kuongezeka kwa kasi ya kutisha. Wakisitisha misaada na mikopo yote ili kupambana na hii Serikali dhalimu hapo watakuwa wametusaidia sana Watanzania maana hata pesa ya kwenda kubembea au kutibiwa nje kwa mafisadi itakuwa hakuna.

Kama utakumbuka pesa za EPA na nyinginezo zilizotuingiza madarakani 2005, zilikuwa nyingi kwani hizi ni change iliyobaki baada ya kuhitimisha zoezi la kuingia madarakani, na pia miradi imeshasimama, hizo tu wametushtukia wazungu wakati tunaendelea kupitisha bakuli sasa wazungu wanajiuliza kwa nini tusitumie hizo tulizozificha kwao?
 
Back
Top Bottom