Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

Kuna watu Wanamwambia wanataka waikomboe nchi

Au wanataka waendelee kuiba
 
Safi sana endeleeni kutuibia kwa kuwa hatujielewi,ikifika kipindi tutakachojielewa tutafanya maamuzi sahihi kwa ajili ya nchi yetu.
Nalog off
 
Mimi nitamuelewa zaidi JPM akituwekea hadharani majina ya hawa watu.

Pia waeleze vyanzo vya pesa hizo na ksma havieleweki azitaifishe.
 
Wanabodi,

Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012
Hizi ni porojo zisizo na mashiko kwa wananchi. Kwasababu hata iweje wahusika hawawezi kujulikana.
Kwanza kuna sheria inayolinda au kuzuia mtu yeyote kujua siri za mtu, halafu kwa viongozi ndio zaidi, huwezi kujua hata benki gani alikoweka akiba yake.
Benki hazitoi kiholela majina ya wateja au namba za account zao, labda hapa nchini lakini huko Switzerland no hawakupi jina kabisa.
Mabenki ya nje pia yana utaratibu wa kutumia namba badala ya majina. Hata uwe nani huwezi kumjua mwenye "numbered account".
Kwahiyo bora tuachane na tuhuma zisizo na ushahidi kamili. Hii kitu ilishamshinda Dr. wa zamani wa CDM ambaye sasa hivi utashangaa nini akijiwekea akiba aliko? Ni haki yake.
 
Labda ziliwekwa huko wakati nchi yetu ilipokuwa haina benki imara...mwisho wa kunukuu.
 
Kwenye hiyo list utakuta wote ni makada watiifu wa Lumumba.
 
Back
Top Bottom