Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

Watanzania 27 wanamiliki mabilioni Uswisi

Hakuna mwandishi wa habari wa kweli na jasiri kama KUBENEA. Mpaka sasa angeshataja majina, account namba za wahusika na balance kwenye kila account. Miss U Mr Kubenea.
 
Wanabodi,

Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012

kwangu mimi hii si habari,,,,,NAHITAJI HABARI,HABARI YENYE MAJINA YA WALIOFICHA,,,,NA SI KUWATAJA PIA WAFIKISHWE MAHAKAMAN,NA SI TU KUWEKWA MAHAKAMAN PIA WAPOKWE HAYO MAHELA,NA SI KUPOKWA TU WANAPASWA KUHUKUMIWA JELA,NA SI KUHUKUMIWA TU PIA WAFILISIWE
 
Watanzania tumegeuka watu wa kulalamika zaidi kiasi hata wale waliopewa madaraka nao wanaongoza tena kulalamika badala ya kutatua matatizo
 
Hakuna mwandishi wa habari wa kweli na jasiri kama KUBENEA. Mpaka sasa angeshataja majina, account namba za wahusika na balance kwenye kila account. Miss U Mr Kubenea.

wapo mazuzu wanaomwita ni mfitin na mchonganishi,,,,ila pia wapo ambao watasema hajasomea habari,,,,,,,,lakini mwisho wa siku nao wanamkubali kiaina,,,,kwani hata hapa jf members wanaotupatia habar na matukio toka sehem mbalimbali wamesomea????na mbona wengi wao wanaeleweka???
 
I cant believe, tunaomba serikali ithibitishe hili, nimemkumbuka Nyerere alisamee pension yake kwa kuwa nchi ni maskini, kumbe kuna nyang'au walikuwa wanasubiria aondoke waanze kuamisha hizi fedha. Mimi nawaomba wananchi tuamke nakulipigania hili. Hata kama serikali itakataa kuwataja na kuwachukulia hatua kali ikiwemo kufilisiwa, sisi tukutane jangwani kuelekea ikulu kumshinikiza rais arudishe hizo fedha au ajiuZulu. Currently we are talking inflation which is 20%+ shame on CCM

yawezekana kabisa kwamba system inawalinda watu hawa. Katiba pia yaweza kuwa sehemu ya kuwaumbua lakini vilevile 2015 yaweza kuwa mwanzo mwema kwa kuanzia yaani kuwaondoa kwanza kwenye system na baadaye taratibu nyingine kufuata
 
Mbona mnamtigatinga ritz ......mwenye macho haambiwi tazama. Mwenye hekima na welevu atafaham kuwa mleta maada alichelewa kidogo huko ccm akitafakali kama ingejirekibisha.

Ritz kalibu mkuu tusaidiane kuwakosoa wanaopora raslimali zetu. Uzao wako, uzao wangu na uzao wake wote wanategemea ww, mm na yule kuwandalia tanzania yenye aman na maisha bora kwa kila mtanzania atakaezaliwa.

Ccm wameshindwa tuungane kupata mbadala na inawezeka.

Karibu Ritz karibu sana mkuu. Sio lazima uvae gwanda hata skaf itatosha.
 
Wanabodi,

Watanzania 27 wakiwamo wanasiasa na wafanya biashara, imebainika kuwa ndio wameficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi, huku mmoja wao akiwa anamiliki Dola za Marekani milioni 56 (sawa na Sh89.6 bilioni).

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mbali na kigogo anayemiliki Sh90 bilioni, wapo wengine wanne, ambapo anayefuatia anamiliki Dola 30 milioni (Sh48 bilioni) mwingine Dola 20 milioni (Sh32 bilioni) na wengine wawili kila mmoja anamiliki Dola 10 milioni (Sh16 bilioni). Katika orodha ya walioweka fedha nchini humo, pia wamo wawili waliowahi kuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, ambao wanamiliki Dola 500,000 kwa kila mmoja.

Miongoni mwa wanaomiliki fedha hizo ni kiongozi wa juu nchini pamoja na aliyepata kuwa waziri katika Serikali ya Awamu ya Tatu iliyoongozwa na Rais Benjamin Mkapa.

SOURCE: MWANANCHI AGOSTI 18 2012

Hata wewe unawageuka magamba wenzio? Si nasikia katika vikao vyenu mmekubaliana kuwa kitu kimoja kwenye shida na raha?
 
hakuna mwandishi wa habari wa kweli na jasiri kama kubenea. Mpaka sasa angeshataja majina, account namba za wahusika na balance kwenye kila account. Miss u mr kubenea.

missing him so much. Where is freedom of press then?
 
Wekeni orodha, haitoshi kusema tu vigogo. Ni akina nani hao? Wekeni wazi majina yao humu.
 
Taarifa itakubalika pindi tutakapoona majina, lakini nashangaa tunae rais na hazungumzii suala muhimu kama ili na inatufanya tuamini na yeye yumo.
 
Jamani mimi naamini kuweka hela uswis si dhambi na si kosa! Mtu aweza tafuta fedha zake akaamua kuziweka uswis, so si tatizo. Kwa mantiki hii sioni haja ya kuficha majina ya wenye hizo fedha. Tukiwafahamu tuwahoji kutokana mapato yao ndo tuwahukumu...

Kinafuata nadhani ni serikali kuacha kuwa kama imemeza kaa la moto, come clean by mentioning them! Tujue kama wamezipata kihalali...
 
taarifa itakubalika pindi tutakapoona majina, lakini nashangaa tunae rais na hazungumzii suala muhimu kama ili na inatufanya tuamini na yeye yumo.

"mwanahalisi liko wapi"
 
Mleta uzi nikuulize mpaka dakika hii wewe bado unawashabikia hao wezi ccm,ama kweli shwetani amekumbatia mioyo yenu.

Kwenye jimbo la pinda niliona watu wanafuata maji km 10 .
shule wameezeka kwa torobali na wanakalia magogo .
Embu Mungu awashukie siku moja muelewe maneno ya dr slaa
 
Tatizo lako wewe ni Chadema Addicted kila sehemu unaleta ushabiki wa vyama unadhani watanzania wote ni wafuasi wa vyama vya siasa hapa tunaongelea maslahi ya Taifa.

Kwa hiyo na wewe siyo shabiki wa Chama chochote cha siasa nchini kwetu Tanzania? Na siyo Addicted? Kwa jinsi nijuavyo ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko Ritz wa JF kuikana CCM!

TUMBIRI (PhD, University of HULL - UK),

tumbiri@jamiiforums.com
 
Back
Top Bottom