Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Cha msingi watu wawe makini tu kwenye hizo groups.
Kuna watu walikuwa wana tabia ya kutukana lakini baada ya kuona wenzao wameshikwa wameacha tena wengine ni mwendo wa kusifia tu
 
Sheria hii ya makosa ya mtandao inalenga hasahasa kulinda dola.

Mwanzoni inaweza onekana ni "kunyoosha" watu kama wanavyosema lakini baadae itakandamiza uhuru kukosoa waziwazi na mwisho watu watakuwa kondoo.

Mtu dhaifu ataogopa sana kukosolewa kwasababu anaona maneno yataweza kumfanya awe kama watu wanavyodhani. Ni suala ya psychology zaidi. Je institutions nazo zinayumbishwa na maneno/mawazo ya vijana wetu wa miaka 17,18,19,20.....?

Tukiendelea kushughulia mambo ya muhimu ndio la maana zaidi.
 
Sema watakupotezea muda, lkn kushinda siyo rahisi, lbd uhuru wa mahakama uingiliwe
Retired kusema ukweli mimi binafsi mahakamani mahospitali ni mahali ambapo namwomba MAULANA aniepushe navyo. ..mambo ya polisi ndiyo kabisa. ....KWA HIYO KILA ASUBUHI NAMSHUKURU MOLA WANGU KWA KUNIPA UHAI MIMI NA KIZAZI CHANGU....MAANA NINA TAMBUA NI KWA NEEMA NA REHEMA ZA MWENYE ENZI MUNGU. ..TUNAISHI NA TUNA AFYA NJEMA!
 
VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.

Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.

Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.

Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.

Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’

Chanzo: Mpekuzi
 
Baada ya kuangaika na mikataba mibovu kama IPTL wanaagaika text za whatsapp
 
Amedharilishwa kajidharilisha wewe mtu anatoa ahadi hewa hataki kuambiwa uchumi ameuwa umoja wa kitaifa,ameua, amevunja upatano, moroli yakila mtu, kwenye nchi hii amevunja, ametengeneza mtandao wa mchwa,wanajiita mawaziri wanazurura nchi nzima, kujionyesha hakuna majibu wataoayo kuboresha hali za wananchi ,anashindwa kukabiliana na majanga wananchi wanauliwa mto kagera, magari ya wafanya biashara watanzania yanachomwa moto Congo,watoto bado wanasoma chini ya miembe, sasa akiambiwa ukweli anapeleka watu mahakamani anajichanganya mapema sana huyu
 
VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.

Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.

Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polis
i’.

Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.

Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’
mag2.jpg
 
ha
Maxence Melo utulinde, usije kumpa mtu yeyote password ya saver yetu
hahaha wakija humu wengi tutakuwa ndani ya nondo ............ kifupi epuka kutaja jina la jpm............... hapo utasalimika ukilitaja tu linasoma kwenye saver huko tiss na tcra................
 
mods futeni post zangu zote nimekoma sirudii tena kusema mambo ya chama tawala.😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
stay tuned
kwa wasio jifunza kwa kusikia bali wanajifunza
kwa kuona....ukiona picha nayo ukishindwa
kusoma usilaumu UPOFU WAKO...
 
Mambo mengine, kwa maoni yangu, ni mambo madogodogo mno na yanaigharimu serikali. Polisi na masnitch ni vema wakawa wavumilivu; waache wau wahisi na kuonyesha wanavyohisi kwa maana hisia zao hazina madhara kwa yeyote. Mtu akikuita "mbwa" au "Mpumbavu" inakudhuru nini kama wewe si "mbwa" au "mpumbavu".

Mambo mengine kwa kweli ni ya kupuuzwa tu!

Anyway hayo ni maoni yangu tu!
 
Ulaya kama unadhani Rais au W/mkuu ni mpumbavu unasema waziwazi,hakuna WA kukubughudhi
 
Back
Top Bottom