miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,805
- 49,109
mi nimejifunza kujifungia chumbani nachukua picha ya mtu namtukana namsema vibaya mpaka nachoka aua nazima data naandika ya moyoni najifanya nimesahahu kutuma
Nani katukana apo wewe. Hebu nionyeshe tusi apo.Ukitaka kujua wabongo wanajua kutukana na hawana ustaarabu wa kwenye mitandao, basi ingia instagram kwenye page za hao wanaitwa wasanii, kuna matusi hujawahi kuyasikia utayaona huko
Ukituma kwenye group hauko safe hawa wote itakuwa wanachat kwenye groupsHivi ile end to end encryption ya whatsapp haiwezi kusaidia mtu asikamatwe na polisi au TCRA?
Kwenye magroup yenu ya wasapu mmepenyezewa maspy na informers.Hivi ile end to end encryption ya whatsapp haiwezi kusaidia mtu asikamatwe na polisi au TCRA?
Hakuna mahali anakopatikana mwanadam pakawa salama mkuuuUshauri kama unajijua huwezi kuzuia hisia zako ondoka kwenye magrouop yote ya whatsapp kwa sasa si salama.
Askari, Usalama, Makada uchwara wamesambazwa sana kwenye magroup kuangalia nani anamtusi 'mtukufu Yohana'. Mahali salama ni hapa JF tu.
Mpaka hapo mbona sioni kosa?Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.
Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.
Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.
Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.
Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.
Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.
Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.
Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”
Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.
hivi na ao wanangojea nini wasikamatwe? Jeshi la polisi hembu mtusaidie hao jamaa wakamatwe ili iwe fundisho kwa wasanii pia.Ukitaka kujua wabongo wanajua kutukana na hawana ustaarabu wa kwenye mitandao, basi ingia instagram kwenye page za hao wanaitwa wasanii, kuna matusi hujawahi kuyasikia utayaona huko
Hapo ni mtu ana screen shot hiyo text anatuna TCRA then wao ndio wanakutafutaHivi ile end to end encryption ya whatsapp haiwezi kusaidia mtu asikamatwe na polisi au TCRA?
Pole sana ndugu..... Ndiio unavyojidanganya kwamba hapa ni salama? PoleUshauri kama unajijua huwezi kuzuia hisia zako ondoka kwenye magrouop yote ya whatsapp kwa sasa si salama.
Askari, Usalama, Makada uchwara wamesambazwa sana kwenye magroup kuangalia nani anamtusi 'mtukufu Yohana'. Mahali salama ni hapa JF tu.
Mkuu kwani uko whatsapp na facebook wanatamka au wanaandika hizo ujumbe?Ulimi ni kitu hatari sana. ...sasa inabidi aache mambo yake muhimu ya kujali family yake na kwenda mahakamani kila inapoitwa leo. ..EHH MAULANA WANGU NAKUOMBA UNIPITISHE KATIKA NJIA YA HEKIMA NA BUSARA MILELE MIMI NA FAMILIA YANGU. ...ASANTE MOLA WANGU. ..