Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watu wasome alama za nyakati.

Kama democrasia na uhuru wa kutoa maoni unasiginwa au kukandamizwa...
Je huo uhuru wa kuwakilisha mawazo\hisia utakuwepo?!

Ni mapito tu.
 
Ulimi ni kitu hatari sana. ...sasa inabidi aache mambo yake muhimu ya kujali family yake na kwenda mahakamani kila inapoitwa leo. ..EHH MAULANA WANGU NAKUOMBA UNIPITISHE KATIKA NJIA YA HEKIMA NA BUSARA MILELE MIMI NA FAMILIA YANGU. ...ASANTE MOLA WANGU. ..
Mola alishakufaga kitaaambo,..Alafu tunapo-comment hatutumii ULIMI mzee!
 
Watu wahamie telegram tu ndiyo habari ya mjini.
 
Mambo mengi unakuta ni misimu tu yaani lugha za mawasiliano baina ya watu fulani zinaweza kuwa za utani mwingi au maneno yasiyo rasmi. Nenda bandarini kwa makuli au kwenye ujenzi wa line za umeme usikilize lugha zinazotumika.
 
hivi hii sheria ya mitandoni mbona siisikii ikikamata watu wengine wanaopost ngono wengine wanapost picha za watu na kuibandika namba za simu kujifanya nihao watu wanauza tigo kuna mamitandao ya kiduwanzi na kimalaya mbona hawawakamati hao ,,,,,,,,,upo kati ya serikali na raia ama nini
Kwa sasa tunadili na wachochezi tu hata kama wanachokiongea kina ukweli na wana haki ya kukiongea, hao wanaopost ngono hata kama ni kinyume cha maadili hatuna haja nao
 
Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.

Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.

Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.

Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.

Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.

Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”

Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.

WAWAFUNGE TU KWANI MTU ANATUKANA KAMA VILE HANA BUSRARA ZA KUFIKILIA KUDHALILISHA KUNAKUFANYA HATA WEWE MWENYEWE UONEKANI HUNA UBINADAMU
 
Dawa ni kuwa bize na mambo ya maana hata hapa JF sio salama pia,kuna Mtambo ya wa Israel inaingia popote,hata hiyo end to end encryption mnajidanganya tu,jamaa wa blog ya Ze Utamu alimtukana JK,na Alikuwa akipost vitu akiwa UK-London,walipoingilia kati wataalamu wa technolojia,walimchimbua mpaka chumbani kwake UK.Serikali ipo kazini kama unabisha ropoka tu popote uone.
 
Hivi kati ya hao waliokamatwa kuna tusi hata moja?
Hivi wewe askari wameuawa 4 na majambazi wenyewe siraha,anatokea mwananchi anapongeza majambazi akidai wangeua hata ishirini,unamtetea kweli??.. Na watafungwa watu very soon ndo utapata akili
 
Hivi wewe askari wameuawa 4 na majambazi wenyewe siraha,anatokea mwananchi anapongeza majambazi akidai wangeua hata ishirini,unamtetea kweli??.. Na watafungwa watu very soon ndo utapata akili
aliyesema hivyo kaonyesha tu jinsi asivyothamini uhai wa binadamu wenzake, ni wa kumpuuza tu na wala si wakuhangaika naye
 
Hilo sio tusi,na lime expire,Toa tusi uone kama JF salama au la!??
Kwani lissu kesi yake mahakamani inahusu nini?Sio maneno hayohayo?Na wewe ni mchochezi,unanichochea kumtukana Rais klaza
 
Back
Top Bottom