Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Tumezoea kuropoka mno. Kuna jamaa mmoja aliwahi kuniambia 'wa Tanzania wangekuwa wanazungumza kiingereza kwa ufasaha, hata wanaijeria wasingetukuta', thank goodness wengi wetu lugha ya malkia inatupiga chenga.
kama naniliu yuleee ... mheshimiwaa.. sijawahi kumsikia akionge kikilistu
 
Kwani hao walioshtakiwa wametumia ulimi au pc/simu zao..?!
Duh! Take a wild guess. .huo si mwili mmoja au fikra nyingine zinatoka nje ya mwili. ...maswali mengine dah! Wallahi!
 
Ukitaka kujua wabongo wanajua kutukana na hawana ustaarabu wa kwenye mitandao, basi ingia instagram kwenye page za hao wanaitwa wasanii, kuna matusi hujawahi kuyasikia utayaona huko
Mbona matusi waasisi na watukanaji wakuu wa nchi hii ni wana ccm......?????.....REJEA KWENYE KAMPENI WANAVOPANIC KWA KUKOSA HOJA NA KUANZA KUTUKANA OVYO.....Ni malezi mabaya ya viongozi wa ccm ndo yamezaa haya matusi.
 
Tumia open source halafu kuwa na Tor browser ,cyber ghost ,kali Linux simple like that
 
Watu wanashindwa kutii sheria bila shuruti na badala yake wanatoa matusi hovyo bila kujielewa. Sheria ichukue mkondo wake maana hata humu wapo wengi wanawatukana wenzao bila sababu
 
Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.

Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.

Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.

Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.

Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.

Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”

Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.
WANGEMCHANGANYA NA NGOYAI NA ILE KAULI YAKE KWENYE BBC KISWAHILI
 
Nasikia yule Dada anayeitwa mange Jamaa walitaka kuruhusiwa wamkamate wakaambiwa ni raia wamarekani na serikali ya marekani haihangaiki na umbeya wa kwenye mitandao hivyo asikanyage mtu marekani wasubiri aje atukanie huku Tanzania ndo wamkamate kule marekani kukosoana ni jambo la kawaida.
 
Mbona haki za binadamu zinavunjwa? Bunge limeridhia mikataba mingi juu ya haki za binadamu na haitaekelezi?
 
Kwenda jela kunamfanya mtanzania mwingine azidi kulipwa mshahara kupitia kosa lako, watu wasipo tenda mkosa, mawakili, mahakimu, majaji na askari magereza hawatokuwa na kazi tena.
mkuu jela sio kuzur,sio sehem ya kumuombea mtu aende
 
Rais mwenyewe anatumia vibaya media mbona?Aliwaita wanafunzi wa UDOM vilaza na hakushtakiwa popote

Hata ukiona hayo wanayo ita matusi wala sio matusi bali watz wanao onyesha frustration zao kwa utawala na vyombo vyake vya dola
 




VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.

Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.

Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polis
i’.

Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.

Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’
 
we mbona uko nyuma unaishi sayari gani? kila Uzi unaoibuka nao umeshawekwa humu na kajadiliwa kitambo. lofa kweli wewe
 
Ushauri kama unajijua huwezi kuzuia hisia zako ondoka kwenye magrouop yote ya whatsapp kwa sasa si salama.

Askari, Usalama, Makada uchwara wamesambazwa sana kwenye magroup kuangalia nani anamtusi 'mtukufu Yohana'. Mahali salama ni hapa JF tu.
Hata hapa JF sio salama kama unavyofikiria. Waulize wadau watakuhabarisha.
 
Back
Top Bottom