Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Mkuu kuna mtu aliniambia kuhusu hicho kitu, hivi inasaidia vipi?
End to end encryption ni kwamba ili msg isomwe mtu anatakiwa awe na special key km ata intercept. Kwahiyo msg hiyo ataiona yule tu aliyetumiwa. Wale hackers au wengine ni ngumu kuiona. Kwahiyo hata wakifanikiwa kuifungua hawatakuta kitu. Ndio maana baadhi ya hard drive watu wana encrypt hata computer ikiibwa, hakisomeki kitu.
 
End to end encryption ni kwamba ili msg isomwe mtu anatakiwa awe na special key km ata intercept. Kwahiyo msg hiyo ataiona yule tu aliyetumiwa. Wale hackers au wengine ni ngumu kuiona. Kwahiyo hata wakifanikiwa kuifungua hawatakuta kitu. Ndio maana baadhi ya hard drive watu wana encrypt hata computer ikiibwa, hakisomeki kitu.
Asante mkuu
 
Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.

Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.

Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.

Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.

Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.

Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”

Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.

Kesi zote hizi watashinda, itakuwa vizuri zikienda mpaka Court of appeal zikapata kuwa authority for future reference
 
Ushauri kama unajijua huwezi kuzuia hisia zako ondoka kwenye magrouop yote ya whatsapp kwa sasa si salama.

Askari, Usalama, Makada uchwara wamesambazwa sana kwenye magroup kuangalia nani anamtusi 'mtukufu Yohana'. Mahali salama ni hapa JF tu.

Hakuna anayemtukana. Watu wanafanya analysis of what is happening.
 
hivi hii sheria ya mitandoni mbona siisikii ikikamata watu wengine wanaopost ngono wengine wanapost picha za watu na kuibandika namba za simu kujifanya nihao watu wanauza tigo kuna mamitandao ya kiduwanzi na kimalaya mbona hawawakamati hao ,,,,,,,,,upo kati ya serikali na raia ama nini
 
Ulimi ni kitu hatari sana. ...sasa inabidi aache mambo yake muhimu ya kujali family yake na kwenda mahakamani kila inapoitwa leo. ..EHH MAULANA WANGU NAKUOMBA UNIPITISHE KATIKA NJIA YA HEKIMA NA BUSARA MILELE MIMI NA FAMILIA YANGU. ...ASANTE MOLA WANGU. ..

Kufa kupo pale pale, milele ipi unayoisema. Utaishi milele, acha woga. La kweli liseme na kweli itakuweka huru. Usiogope kusema 1+1=2, huo ni ukweli
 
sehem salama ni jf tu sababu tunatumia fake account hivyo ni ngumu kumshtaki mtu ambae jina sio lake kwa mfano mtu anaitwa mzizimkavu ni rahisi sana mtu huyu kukana sababu anatumia jina halali la ally juma na mtenda kosa ni mzizi mkavu
 
Kufa kupo pale pale, milele ipi unayoisema. Utaishi milele, acha woga. La kweli liseme na kweli itakuweka huru. Usiogope kusema 1+1=2, huo ni ukweli
Mimi siamini kwa hesabu hiyo. ..kwangu 1+1=1 I believe in miracles. ..huwa nina jipa positive thinking na sitaki kuendeshwa na hasira. ..maji yakichemka baadae yatapoa tu! Sio uwoga ni hekima ya MWENYE ENZI MUNGU. ..HERI YULE ANAYE WEZA KUTAWALA MOYO WAKE. .
 
Back
Top Bottom