Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.

Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.

Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.

Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.

Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.

Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”

Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.
 
Hivi ile end to end encryption ya whatsapp haiwezi kusaidia mtu asikamatwe na polisi au TCRA?
 
Tumezoea kuropoka mno. Kuna jamaa mmoja aliwahi kuniambia 'wa Tanzania wangekuwa wanazungumza kiingereza kwa ufasaha, hata wanaijeria wasingetukuta', thank goodness wengi wetu lugha ya malkia inatupiga chenga.
 
Ukitaka kujua wabongo wanajua kutukana na hawana ustaarabu wa kwenye mitandao, basi ingia instagram kwenye page za hao wanaitwa wasanii, kuna matusi hujawahi kuyasikia utayaona huko
 
Ushauri kama unajijua huwezi kuzuia hisia zako ondoka kwenye magrouop yote ya whatsapp kwa sasa si salama.

Askari, Usalama, Makada uchwara wamesambazwa sana kwenye magroup kuangalia nani anamtusi 'mtukufu Yohana'. Mahali salama ni hapa JF tu.
 
Mkuu kuna mtu aliniambia kuhusu hicho kitu, hivi inasaidia vipi?
Kinafanya unavyokuwa unachati na mtu WhatsApp mtu mwengine yeyote hapo katikati asiweze kusoma au kuhack hizo sms zako zaidi ya yule unayemtumia.
 
Ulimi ni kitu hatari sana. ...sasa inabidi aache mambo yake muhimu ya kujali family yake na kwenda mahakamani kila inapoitwa leo. ..EHH MAULANA WANGU NAKUOMBA UNIPITISHE KATIKA NJIA YA HEKIMA NA BUSARA MILELE MIMI NA FAMILIA YANGU. ...ASANTE MOLA WANGU. ..
 
Back
Top Bottom