Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

watanyooka tu mpaka 2026 sio mchezo
Hayupo aliyeweza kumnyoosha binadamu, akili za kizamani na utashi wa uongozi wa kizamani, eti ulazimishe watanzania million 45 watii sauti ya mtu mmoja tu, haijawahi kutokea.

Wawaache watu watapike nyongo zao ndo kupumua kwa nchi huko, ukitaka kuwanyamazisha watu kwa lazima, watavunga wanakutii kwa mda kumbe wanakuvutia pumzi, Siku wakiamuwa utawauwa na bado wanasonga mbele.

Jifunze kitu kupitia japo tu familia ya baba ama mama mbabe, mwisho wake hiyo familia huwa haiwezi kumtii tena bali huwa wanazuga tu.

Binadam haonyooshi kwa mabavu, bali kwa akili.
 
mkuu tele nako si watatutia nyavuni? Au tele...ni secure
Tele unaweza hide no yako kama upo kwenye group chat haitajulikana kama imetoka kwako, pia msg,picha, video zinakua self-destructed baada ya dakika 5 hivi. Haiachi ushahidi
 
Kwa vyovyote vile,mamlaka iheshimiwe
Siku zote kumbuka neno hii, huwezi kumlazimisha binadamu mwingine akuheshimu wakati wewe hujamuheshimu' hata kama ni mwanao hatakuheshimu.

Kwa hiyo viongozi wajiheshim kwanza na kuwaheshimu RAIA na RAIA watawaheshimu tu bila kushurutishwa.

Usione akina Nyerere, Mandela, Nkuluma...nk..walikuwa wakipita kila mahara wanapigiwa vigelegele na kushangiliwa ukahisi walikuwa wakiwashurutisha watu kuwashangilia, no waliwaheshimu na kuwathamini sana RAIA wao, na kuwafanya kuwa wao ndiyo kila kitu kwao.

Ndo maana ktk hotuba zao walizitoa kwa hekima na busara za hali ya juu, na kwa tahadhali ya kutowakwaza RAIA wema wa nchi zao.

Usimshurutishe mtu akuheshimu, bali mfanye mtu ajisikie kukuheshimu.
 
Sheria Kali za Mtandao tii sheria bila shurti SAA mbaya hii ukileta za kuleta jela inakukaribisha
Kwenda jela kunamfanya mtanzania mwingine azidi kulipwa mshahara kupitia kosa lako, watu wasipo tenda mkosa, mawakili, mahakimu, majaji na askari magereza hawatokuwa na kazi tena.
 
Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.

Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.

Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.

Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.

Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.

Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”

Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.

Hapo kwenye BLUE naomba kueleweshwa kosa lipo wapi
 
WAWAFUNGE TU KWANI MTU ANATUKANA KAMA VILE HANA BUSRARA ZA KUFIKILIA KUDHALILISHA KUNAKUFANYA HATA WEWE MWENYEWE UONEKANI HUNA UBINADAMU
Vipi yule aliyewaita watoto wa wenzie villaza ana ubinadamu???
 
Sheria ya mitandao imeendelea kung’ata, baada ya wakazi wa Dar es Salaam kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashtaka tofauti ya kumdhalilisha Rais na Jeshi la Polisi kwenye mitandao.

Katika kesi ya kwanza, Dennis Temu (26), ambaye ni fundi magari anayeishi Tabata, alisomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye mtandao wa WhatsApp.

Wakili wa Serikali, Salum Mohammed alidai mbele Hakimu Mkazi Mkuu, Emilius Mchauru kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 30, 2016 akiwa Tabata Bima, wilayani Ilala kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kusambaza ujumbe usemao; “Nipo tayari kwa Ukuta naomba wanikabidhi askari 10 nipambane nao wakinishinda Mungu anihukumu. Tupigane mkono kwa mkono ‘pumbav’... zao”.

Temu amekana shtaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao walisaini dhamana ya Sh500,000. Kesi hiyo itatajwa tena Oktoba 12.

Katika kesi nyingine, Suleiman Nassoro (20) fundi umeme anayeishi Kigogo Mbuyuni, amesomewa mashtaka ya kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Mshtakiwa huyo anadaiwa kuandika ujumbe usemao; “safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi. Halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au” ambao aliutuma Agosti 25.

Lakini Nassoro amekana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka ulisema haujakamilisha upelelezi, jambo lililofanya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 27 itakapotajwa tena.

Mwingine ni dereva Juma Mtatuu (19) anayedaiwa kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp kwa kuandika; “huyu hata akifa ataenda peponi na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala. Mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama. Tarehe 1 Naelekea Kahama kwa Ukuta mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta. Kifo kipo tu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha?”

Pia, mkazi wa Tegeta kwa Ndevu, Shakira Abdallah Makame amefikishwa mahakamani hapo akikabiliwa na shtaka la kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kutumia WhatsApp.
Duu sasa hivi Serikali itatumia resource za kutosha kudeal na kesi, hivi ni kwanini kwasasa watu wanamshambulia sana Rais huyu? naona kama kipindi hiki kesi zimekua nyingi sana
 
End to end encryption ni kwamba ili msg isomwe mtu anatakiwa awe na special key km ata intercept. Kwahiyo msg hiyo ataiona yule tu aliyetumiwa. Wale hackers au wengine ni ngumu kuiona. Kwahiyo hata wakifanikiwa kuifungua hawatakuta kitu. Ndio maana baadhi ya hard drive watu wana encrypt hata computer ikiibwa, hakisomeki kitu.
Je waki decrypt
 
Eli79,

..umesema wa Tz tungekuwa tunajua Kiingereza tungefanya vurugu kuliko Wanigeria.

..kuna advantage na disadvantage kwa waTz kutokuimudu lugha ya Kiingereza.

..moja ya disadvatage ya Kiswahili ni jinsi kinavyofunika kauli za hovyo-hovyo, vitisho, na ubabe, zinazotolewa na viongozi wetu dhidi ya wananchi.

..kauli hizo zingekuwa kwa Kiingereza wengi huko nje wangeelewa kinachoendelea humu nchini.

..zaidi mijadala ya kiuchumi kisiasa na kijamii nayo inafunikwa humuhumu nchini kwasababu ya lugha hii ya Kiswahili.
 
Ulimi ni kitu hatari sana. ...sasa inabidi aache mambo yake muhimu ya kujali family yake na kwenda mahakamani kila inapoitwa leo. ..EHH MAULANA WANGU NAKUOMBA UNIPITISHE KATIKA NJIA YA HEKIMA NA BUSARA MILELE MIMI NA FAMILIA YANGU. ...ASANTE MOLA WANGU. ..
Kwani hao walioshtakiwa wametumia ulimi au pc/simu zao..?!
 
swali la kijifikirisha tu kila anayeshitakiwa ni Whatsapp hivi Facebook, Twiter na nyingine hakuna matusi?
 
Back
Top Bottom