Watangazaji Paul James (PJ) na Gerald Hando watua rasmi E-Fm

fina katoka magic kaenda clouds, captain katoka efm kaenda clouds, dina, maestro, hando na pj wametoka clouds wameenda efm, kitenge na mwenzake wametoka radio1 wameenda efm, hapo clouds mtangazaji kiwango aliyebaki naona ni ayo tu, kweli huu mchezo hauhitaji hasira!
 
Ivi usajiri huu ni dirisha dogo au?maana naona redio stesheni busy kusajili watangazaji soon utasikia wanamuziki nao wameanza kuhama hama duh Bongo kweli nyoso.
 
msaada wa kifaa cha kuvuta frequency kwenye gari,maana hivi vivitz vya mjapani mwisho 90 havifiki 93.7,siwezi kuwamiss hawa majamaa aisee.ikishindikana ntatafuta kiredio cha battery nakuwa nakiwasha kwenye gari
Funga redio nyingine Mpya ya kisasa yenye kukamata frequency zote.....ila pouwa kama huna hela nunua FM CONVERTER ufunge utapata frequency zote.
 
Kupitia kisimbusi cha Azam naipata Efm bila chenga.......na kwa sasa nahamia rasmi kusikiliza kipindi cha joto la asubuhi......
 
7d7f40c54ff0e0c0917c2593807cd234.jpg

Wale waliokuwa watangazaji wa kipindi cha Power breakfast cha Clouds Fm, Gerald Hando na Paul James "PJ" Hatimaye wametua Efm. Kama wanavyoonekana katika hiyo picha
 
E-fm iko juu mno kwa sasa. Clouds taratibu inaanza kupotea hewani.
Najiuliza sana kwanini mtu akitoka Clouds ana enda E-fm Kuna vipindi gani vizuri huko kwa mfano na mimi nikapata kuisikiliza maana bado sijaielewa vipindi vyake ila mimi ni mdau wa Bongo fleva na ma dj wakali na kile kipindi kinachotangazwa na mpoki ni saa ngapi?
 
Kwani wamefukuzwa au wameondoka kwa hiari yao?

Wala hawakufukuzwa na hawakuondoka kwa hiari yao Mkuu isipokuwa tu Mikataba yao ilifika ukingoni na uongozi ulipofanya perfomance assessment yao ukagundua kuwa they under performed na kuwaambia kuwa hawataongezewa tena mikataba na kuwatakia kila la kheri huko waendako. Nimeshangaa sana na kusikitika kuona kuwa hadi sasa Watu jambo dogo tu hili la kufanya competency ya Clouds FM na E FM linawashinda. Technically E Fm inahitaji miaka mitano ( 5 ) katika field kuja kuanza kuikuta Clouds Fm na hili litafanikiwa tu endapo Clouds Fm nao watalala usingizi ila kwa moto huu ninaouona wa Clouds Fm itawahitaji E Fm kusubiri miaka kama 10 ijayo ndiyo kidogo waje kuwakaribia Clouds Fm. Isipokuwa E Fm wameanza vyema na wakijipanga vyema hasa KIMKAKATI katika masuala ya uboreshaji wao wa vipindi, kujitanua zaidi na kuwa creative naona huko mbeleni watakuja kutisha lakini kwa sasa kusema E Fm itaitisha Clouds Fm kwa kuwapata hao akina PJ, Hando na Abel Onesmo ni kichekesho kwa wenye TAALUMA zetu zilizotukuka za hiyo TASNIA. Nawaheshimu E Fm ila nawapigia salute Clouds Fm na tujifunze kufanya kitu kiitwacho PROFESSIONAL INTELLECTUAL ANALYSIS ili tuwe vizuri pale tunapokuwa tunajenga HOJA na siyo KUHEMKA.
 
Najiuliza sana kwanini mtu akitoka Clouds ana enda E-fm Kuna vipindi gani vizuri huko kwa mfano na mimi nikapata kuisikiliza maana bado sijaielewa vipindi vyake ila mimi ni mdau wa Bongo fleva na ma dj wakali na kile kipindi kinachotangazwa na mpoki ni saa ngapi?
Kpindi kinaitwa Ubaoni kinaanza saa 10.
 
Najiuliza sana kwanini mtu akitoka Clouds ana enda E-fm Kuna vipindi gani vizuri huko kwa mfano na mimi nikapata kuisikiliza maana bado sijaielewa vipindi vyake ila mimi ni mdau wa Bongo fleva na ma dj wakali na kile kipindi kinachotangazwa na mpoki ni saa ngapi?
Cha mpoki ni saa 10!
Wana vipindi vingi vizuri tuu..
 
Wala hawakufukuzwa na hawakuondoka kwa hiari yao Mkuu isipokuwa tu Mikataba yao ilifika ukingoni na uongozi ulipofanya perfomance assessment yao ukagundua kuwa they under performed na kuwaambia kuwa hawataongezewa tena mikataba na kuwatakia kila la kheri huko waendako. Nimeshangaa sana na kusikitika kuona kuwa hadi sasa Watu jambo dogo tu hili la kufanya competency ya Clouds FM na E FM linawashinda. Technically E Fm inahitaji miaka mitano ( 5 ) katika field kuja kuanza kuikuta Clouds Fm na hili litafanikiwa tu endapo Clouds Fm nao watalala usingizi ila kwa moto huu ninaouona wa Clouds Fm itawahitaji E Fm kusubiri miaka kama 10 ijayo ndiyo kidogo waje kuwakaribia Clouds Fm. Isipokuwa E Fm wameanza vyema na wakijipanga vyema hasa KIMKAKATI katika masuala ya uboreshaji wao wa vipindi, kujitanua zaidi na kuwa creative naona huko mbeleni watakuja kutisha lakini kwa sasa kusema E Fm itaitisha Clouds Fm kwa kuwapata hao akina PJ, Hando na Abel Onesmo ni kichekesho kwa wenye TAALUMA zetu zilizotukuka za hiyo TASNIA. Nawaheshimu E Fm ila nawapigia salute Clouds Fm na tujifunze kufanya kitu kiitwacho PROFESSIONAL INTELLECTUAL ANALYSIS ili tuwe vizuri pale tunapokuwa tunajenga HOJA na siyo KUHEMKA.
Mkuu asante kwa majibu ya swali la awali nililouliza.

Ila haya maelezo ya ubora wa clouds inabidi pia uyatazame katika kipindi ambacho imekuwa na kukomaa. Ni kipindi cha magumashi sana katika nchi yetu kama vile ukwepaji wa kodi, urafiki baina ya vyama vya siasa na vyombo vya habari n.k.

Ebu fuatilia haya uone the rise of that particular station
 
Back
Top Bottom