Mwaka 2000 nikiwa Malaysia kwenye kongamano la dini ya Buddha pale Malaysia university nilikutana na mhindi mmoja tajiri aliyewahi kuishi na kutajirikia bongo.
Kwa utani unaouma na kuakisi ukweli akasema usipotajirika Tanzania ni ngumu kutajirika pengine Niliumia sana naye aliyaona maumivu yangu lakini huo ndio ulikuwa ukweli
Mkataba mbovu wa bandari zetu zote na kampuni kubwa ya DPW umeshapigiwa kelele na kila kaliba ndani ya taifa hili lakini bado kuna mazuzu wajinga wachache wanaona unafaa
Kati ya hao kuna wale walioko mamlakani ambao wamepata chochote ili kuutetea.. Hawa kwangu ni wahaini na wasaliti wakubwa na hukumu yao kuna siku itafika
Ninaowahurumia ni hawa wafuata mkumbo kwasababu za kiimani, itikati za kisiasa jinsia na wote wenye fikra finyu kwamba nwafrika hawezi kitu bila msaada wa ngozi nyeupe ama manjano..
Kinachopiganiwa ni kwa maslahi ya watoto, vijukuu, vitukuu na vining'ina vya taifa hili la Tanganyika.. Bila kujali
Imani zao
Rangi zao
Itikadi zao nk
Haya yote hawayaoni.. Inafika mahali unajiuliza je wana matatizo ya akili?
Mimi nikianza kufikiria hayo huwa nadhani kuna living zombies duniani wapo tunaishi nao.
Misukule mfu iliyotiwa roho na shetani kisha kuweza kuishi na kutenda kwa sura ya binadamu kumbe ipo!
Tena nikikumbuka na historia ya utumwa, ambayo kabla nilikuwa najiuliza ilikuwakuwaje wafanya biashara wachache kuweza kukamata na kisha mateka, kuwapiga cheni na kuondoka na watumwa wa kutosha kwa maelfu kirahisi rahisi tu, nilikuwa sipati jibu!
Lakini kwa stori hii ya Bandari namna ilivyoanza na tulipofikia tayari nimeunga dots na kupata majibu namna hata wewe mjanja wa kukwepa majanga ambavyo waweza kamatwa na kuhasiwa bila ya kujitetea wala kukimbia!
Kumbe hii kasumba ya kuwaamini viongozi wenye majina katika jamii ndiyo njia rahisi na nyepesi ya kutia watu utumwani!
Umoja tunaoimbishwa waTz kuwa tunao, kumbe haupo na chochote cha hovyo kinaweza kutendeka nchini mwetu na pasitokee pingamizi kutoka katika jamii kwa sababu umoja haupo, tulishagawanywa kwenye makundi mfu ya kidini, kichama na kikanda!
Ninasema tena umoja haupo kwa mfano wa mikataba yote mibovu, kuanzia ya Umeme wa Net group sln, Trl ya vijisenti(joka la makengeza), uchimbaji wa madini na gesi na mingine mingi ambayo siwezi kuitaja yote, imeingiwa na kuboronga si zaidi ya miongo mitatu na takribani watu wote wazima tulikuwepo na kushuhudia sakata zote hizo na hadi watu kugawania maburungutu kwenye viroba(kashfa ya Escrow)!
Iweje leo watu hao hao wasahu na waendelee kuamini uwekezaji wenye masharti mabovu waweza kuikwamua nchi kiuchumi?
Tukiendelea na ujinga huu huku tukiamini kuna umoja na mshikamano bila ya kumtafuta mchawi na kumtokomeza,Taifa litatugawanyikia mikononi mwetu kweli.