Ukiona mtu hajadili hoja akaanza kumzodoa mtoa hoja, akaanza tafuta makandokando ya hoja, basi jua hoja hiyo ina mashiko na mjibu hoja ameshindwa.
Mtu anaanza tafuta vyuo vilivyopo malaysia, maana yake hoja kuu imemshinda kujibu.
Mtu akianza tafuta dini ya mleta hoja, basi hoja kuu imemshinda.
Uzuri Samia ameshasikia hoja, na hili tamko la TEC ndio msumali wa mwisho, watayazingatia tu matakwa ya Watu.
Sisi waislam tuache kujitoa akili. Hakuna anayepinga hili suala sababu ya dini. Waturuki wanajenga reli hakuna aliyewapinga. Wairan wanamashirikiano na jeshi letu, toka enzi za Jakaya na haijawahi kuwa shida.
Mkataba wa Richmond tuliupinga si kwa sababu wazungu ni wakristo.
Juzi nasikia wale waimba mapambio wa wasafi, wanasema kama kuna mapungufu yarekebishwe maana muwekezaji hawezi fanya kazi ikiwa wananchi hawataki-wameanza legea.
Samia ameshasikia, atatii tu, hawa court jesters wa mitandaoni ni vifuata upepo tu.